kesi za maandamano ya Oktoba 29 yatamatika Bunda na kuachiwa huru kwa watu 30

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ya Musoma, imemwachia huru George Mapuli Bukingi na kuhitimisha rasmi mfululizo wa kesi za vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, wilayani Bunda.

Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Kakolaki, aliyekubali rufaa ya Bukingi iliyokuwa ikipinga hukumu ya kifungo cha miaka mitano jela iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Bunda. Jaji Kakolaki alibainisha kuwa ushahidi uliotumiwa na mahakama ya chini kumtia hatiani haukujitosheleza kisheria, hivyo kuamuru aachiwe huru mara moja.
Akizungumza kuhusu uamuzi huo kupitia mtandao wa X, Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA, Wakili Gaston Garubindi, amethibitisha kuwa kuachiwa kwa Bukingi kunahitimisha rasmi mashtaka dhidi ya raia wote waliokamatwa wilayani humo.

Bukingi alikuwa miongoni mwa raia walokamatwa kufuatia vurugu za Oktoba 29. Awali, alikabiliwa na mashtaka ya uhaini kabla ya mashtaka hayo kubadilishwa na kushtakiwa kwa kosa la kumjeruhi askari polisi.
Kufutiwa kwa hukumu hiyo dhidi ya Bukingi kunaifanya idadi ya raia wote 30 waliokuwa wakishtakiwa kwa kuhusika na vurugu za Oktoba 29 wilayani Bunda kuwa huru.

Ushindi huo wa rufaa katika Masjala ya Musoma ulipatikana kupitia usaidizi wa kisheria kutoka kwa Mawakili wa CHADEMA, Wakili Alex Massaba pamoja na Wakili Aloyce Kajitamusi

Chanzo:Gaston shundo ,Royal tv
 
ok.
well done mahakama huru ya Tanzania 🐒
 
Wassira atakuwa anatamani awalambe chuma
 
Hilo ni pigo kwa mashoga ya ccm tunasubir tena tarehe 6/11/2026 kuyapa stress pindi jiji la daresalama litakaposimama siku Lissu anaachiwa.
 
Back
Top Bottom