Kesi za Maslahi ya Umma Nchini Tanzania: Uchambuzi na Maoni

Kesi za Maslahi ya Umma Nchini Tanzania: Uchambuzi na Maoni

Irene Gudu

New Member
Joined
May 6, 2024
Posts
2
Reaction score
1
Muhtasari
Kesi za maslahi ya umma ni moja ya silaha ya kupambana na malalamiko kama vile uvunjifu wa haki za Binadamu unaofanywana serikali au taasisi zisizo kuwa za kiserikali. Mashauri hayayamekuwa yakitumika kushinikiza upatikanaji wa haki pamoja na Ulinzi wa haki za watu masikini na nakundi Maalumu ndani ya Jamii, kama vile Wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.

Andiko hili limelenga kuchambua sheria na changamoto zilizopokatika ufunguaji wa kesi za maslahi ya umma nchini Tanzania, kwa kuchambua na kubainisha matokeo ya Mabadiliko ya sheria yaliyofanywa kupitia Sheria ya Mabadiliko Na. 3 ya mwaka 2020. Mabadiliko haya yalifanyika kwa kuongeza kifungu ndani ya Sheria ya Kuweka Utaratibu wa Utekelezaji wa Haki na Wajibuwa Kimsingi wa Kikatiba, na kumtaka kila anaepeleka kesimahakamani kupeleka hati ya kiapo akionesha ni kwa kiasi ganikitendo anachokilalamikia yeye ndiye ameathirika nacho mojakwa moja.

Mabadiliko haya ni kinyume na Ibara ya 26(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ambayoinaruhusu mtu yeyote bila kuwa na maslahi binafsi, kugongamlango wa mahakama na kutafuta haki kwaniaba ya watuwengine wasiojiweza Kufanya hivyo. Kwahivyo, ni Hitimisho la Andiko hili kwamba, haki ya kufungua kesi kwa maslahi ya ummanchini Tanzania imepokwa.

1.0 Utangulizi
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa nafasi kwa mtu yeyote ya kufungua Shauri mahakamani kwa maslahi yakemwenyewe au kwa maslahi ya watu wengine kama mmoja wa wwnajamii. Lakini, Sheria ya Kuweka Utaratibu wa Utekelezaji wa Haki na Wajibu wa Kimsingi wa Kikatiba, imefanyiwaMarekebisho ili kuondoa uwezekano wa mtu kufungua aina ya kesi hizi za kikatiba. Mabadiliko hayo yanamtaka mtu yeyoteambaye anafungua Shauri la kupinga kuvunjwa kwa haki za Binadamu, kueleza ni kwa kiasi gani kuvunjwa kwa haki hizokunaathiri maslahi yake mweneyewe.2 takwa hili la kisherialinaondoa haki ya watu kufikia mahakama ili kuhakikisha haki za Binadamu zinalindwa. Lakini pia, Mabadiliko haya yako kinyumena Ibara ya 26(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaruhusu mtu yeyote ndani ya Jamii kufunguaShauri kwa maslahi ya umma ili Kulinda haki za Binadamu na piaKulinda Katiba, bila kujali maslahi binafsi ndani ya kesi hiyo. Andiko hili linachambua sheria hii ili kubainisha changamotozinazokabili ufunguaji wa kesi kwa maslahi ya umma nchiniTanzania.

2.0 Kesi kwa Maslahi ya Umma Tanzania
Nchini Tanzania, kesi kwa maslahi ya umma zilianza kutumikabaada kuundwa kwa Katiba ya mwaka 1977 na kujumuishwa kwa haki za Binadamu ndani ya Katiba Mwaka 1984, ambapo kanuniza haki ya kupeleka kesi mahakamani, au kusimama mahakamanizilipanuliwa. Baada ya haki za Binadamu kujumuishwa kwenyeKatiba, mahakama zilikuwa mstari wa mbele katika kutambuahaki hii. Mahakama zilibadili mtazamo wake kwenye haki ya kufungua kesi kwa maslahi ya umma na zilianzisha Mfumo Huria katika kesi za aina hii huku zikikataa msimamo wa zamaniuliorithiwa kutoka kwa mkoloni na ulionekana kuwa umepitwa na wakati.

Kumekuwa na kesi mbalimbali, ambapo mahakama zilitambua aina hii ya Mashauri na zilitoa mazingatio maalumu kwa waletaMashauri walioonyesha maswala ya muhimu ambayo yalikuwana matokeo chanya kwenye maisha ya watu. Majaji wamekuwawakiitafsiri Katiba kwa kuruhusu ufunguaji wa Mashauri na mtuyeyote ambaye kwa moyo thabiti anataka kufungua Shauri hilo, hata kama hana maslahi binafsi kwenye kesi hiyo, ili kulinda hakiza raia pamoja na Katiba.

Maamuzi haya yalikuwa na umuhimu kwasababu katika kesi nyingi, waathirika ikiwa ni pamoja na masikini na watu wasiojiweza, hawakuwa katika nafasi ya kupeleka Mashauri hayo mahakamani kwa niaba yao wenyewekutokana na sababu mbalimbali za kiuchumi na kijamii kama vile ujinga, umasikini, na ulemavu. Kuruhusiwa kwa kesi za maslahiya umma kulitoa nafasi kwa raia kulinda na kudai haki zaowenyewe na za wengine wasioweza kujisemea wenyewe na kuiwezesha mahakama kutenda haki katika mazingira ambayomtu wa kawaida anaweza kuyafikia. Wanaharakati wa haki za Binadamu wengi walifungua Mashauri kuishitaki serikali kwa kuvunja haki za Binadamu na Katiba pia, ambapo walishinda na kuleta Mabadiliko ya kisheria na kisera kwenye Jamii.

Miaka zaidi ya 20 baadaye, tarehe 10/06/2020, Bunge la Tanzania lilichapisha mswaada wa sheria uliopendekeza kurekebisha Sheria ya Kuweka Utaratibu wa Utekelezaji wa Haki na Wajibu wa Kimsingi wa Kikatiba, ili kuzifanya mahakama zisisikilize kesiyoyote ambayo mleta shauri hajatimiza masharti chini ya Ibara ya 30(3) ya Katiba ambayo inataka mtu anayataka kufungua kesi ya Kikatiba, kuthibitisha kwamba maslahi yake binafisi au haki yakeimevunjwa na si ya mwingine.

Mswaada huo ulipitishwa na kuwasheria tarehe 15/06/2020. Kufuatia Mabadiliko hayo, mleta Shauri lazima awe na maslahi binafsi kwenye Shauri hilo ili kuifanyamahakama iingilie. Hata hivyo, kutokana na ukweli kwambawatanzania wengi ni masikini na wasiokuwa na uelewa wa mambo mengi, wengi wao hawatambui haki zao na namna ya kudai haki hizo pale zinapovunjwa. Pia kutokana na umasikini, watu wengi hawawezi kulipa gharama za wakili hata pale wanapokuwa na uelewa juu ya uvunjifu wa haki zao. Hivyo, njiaya kesi za umma ilikuwa njia nzuri ambayo ilitumika Kulinda Katiba na pia haki za umma.

3.0 Mapendekezo
Baada ya kuona namna kesi za maslahi ya umma zilivyokuwa naumuhimu pamoja na athari zilizoletwa na Mabadiliko ya sheria mwaka 2020, yafuatayo ni mependekezo ya nini kifanyike ilikusaidia umma katika vita dhidi ya uvunjwaji wa haki za Binadamu pamoja na Katiba.

(i) Sheria inayotoa nafasi ya mtu kufungua Shauri mahakamani inapaswa kulegezwa ili kuruhusu mtuyeyote kufungua kesi kwa maslahi ya umma itakuwa sio sahihi ndani ya Jamii ya kidemokrasia kama yetu, kuleta vikwazo vingi juu ya kesi za maslahi ya umma, hasa kesi za haki za Binadamu na za Kikatiba. Hali hii inatutenga mbali namataifa mengine yanayoendelea (kama Kenya) ambayoyanaruhusu kesi za aina hii. Hivyo basi, kutokana na umuhimu wa kesi za maslahi ya umma, ambapo haki za watu wengi zinalindwa, sheria haipaswi kuweka vikwazo kwa kuzuia aina hii ya kesi.

Kwa kuzingatia uhalisia wa Jamii yetu, ambapo waathirika wa uvunjwaji wa haki kama vile masikini na wasiojiweza, ambao kwa sababu ya umasikini, kuwa nyuma kieleimu au ulemavu, wanaweza wasiwe katika nafasi ya kwenda mahakamani na kupeleka kesi kwa ajili ya ulinzia wa mahakama kwa uwezo waowenyewe pale haki zao zinapovunjwa. Ni lazima sheria iruhusumtu yeyote ambaye ni mwanajamii hata bila kuwa na maslahibinafisi kwenye suala hilo, kwenda mahakamani kutafuta hakikutokana na uvunjifu wa haki uliofanywa kwa watu wengi ndani ya jamii.

4.0 Hitimisho
Andiko hili lililenga kuchambua matokeo ya Mabadiliko ya sheria ya mwaka 2020 yaliyofanywa kwenye Sheria ya KuwekaUtaratibu wa Utekelezaji wa Haki na Wajibu wa Kimsingi wa Kikatiba, yakilenga kuzuia kesi za maslahi ya umma na kesi za Kikatiba nchini Tanzania. Imeonekana kwamba njia ya kufikiamahakama kupitia kesi za maslahi ya umma imefanywa kuwafinyu kama sio kufungwa kabisa na Mabadiliko haya. Na hivyo, mtu mwenye maslahi binafsi kwenye kesi ndiye anayeruhusiwakufungua Shauri mahakamani. Hali hii imesababisha watuwasiojiweza kubaki bila mtu wa kuwasemea pale wanapoonewa.
 

Attachments

  • 1719294458240.png
    1719294458240.png
    297 bytes · Views: 4
Back
Top Bottom