Kesi za uchaguzi wa Wabunge...................

Kesi za uchaguzi wa Wabunge...................

Kesi ya uchaguzi Segerea: Fred Mpendazoe aendelea kumng'ang'ania Dkt. Mahanga
Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA Kuu imetupilia mbali ombi lililowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea Dkt.Makongoro Mahanga na wakili wa serikali, Bw.David Kawaya, la kutaka
mahakama hiyo ifute kesi ya kupinga matokeo ya ubunge katika jimbo hilo.

Mlalamikaji katika kesi hiyo ni aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, Bw.Fred Mpendazoe.

Uamuzi wa mahakama ulitolewa jana mahakamani hapo na Jaji Profesa Ibrahim Juma.

Jaji Juma aliwapa muda wa siku 14 mawakili wa Bw.Mpendazoe kufanyia marekebisho hati ya madai ili kesi hiyo ianze kusikilizwa.

Marekebisho hayo ni pamoja na kuondoa vituo vya kupigia kura ambavyo vilikuwa eneo la Buguruni, Tabata na Kipawa ambavyo katika hati hiyo, havikutajwa mahali halisi vilipokuwa, ambavyo kasoro yake ilikuwa ni kutohesabiwa kura zake.

Ilielezwa kuwa katika hati ya madai kuna baadhi ya aya zimefumbwa hivyo itampa shida mlalamikaji katika kuandaa utetezi wake.

Kesi hiyo itajwa Juni 22, mwaka huu tayari kupangiwa tarehe ya kusikilizwa.

Mei 25, mwaka huu wakili wa Dkt.Mahanga ,Bw.Jerome Msemwa na Bw.Kawaya waliwasilisha mahakamani hapo maombi ya kutaka kufuta kesi hiyo kwa madai kuwa hati ya kesi hiyo ina kasoro za kisheria.

Bw.Mpendazoe katika madai yake anaitaka Mahakama Kuu itengue ushindi wa Dkt. Mahanga kwa kuwa taratibu za Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 hazikufuatwa.

Kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, yalitokea mabishano makali ya kisheria, ambapo, wakili wa Bw. Mpendazoe, Peter Kibatala na wa mlalamikiwa (Dkt.Mahanga), Bw.Jerome Msemwa ambaye aliiomba mahakama kufute shauri hilo.

Alidai kuwa Bw.Mpendazoe hakufuata taratibu wakati wa kufungua kesi hiyo, ambapo ilitakiwa ianze kusikilizwa kasoro zote za kisheria mbele ya Msajili wa Mahakama Kanda na baada ya hapo ifikishwe kwa jaji.

Alidai kuwa kutokufanya hivyo, kunakiuka kifungu cha 8 kidogo cha (1) cha sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010, ambapo jalada linatakiwa kufikishwa kwa msajili ili kusikiliza kasoro za kisheria au makosa mbalimbali ili yafanyiwe marekebisho kabla ya kufikishwa kwa jaji kusikilizwa.

Pia, wakili huyo alidai kuwa katika hati yake ya malalamiko Bw.Mpendazoe hakutaja majina ya vituo ambavyo anadai vilifanyiwa uchakachuaji wa kura na kwamba hakuna maelezo ya kutosha hivyo mahakama ifute kesi hiyo.
 
hizi kesi hivi sasa hazisikiki isijekuwa ni mbinu yakimahakama kuhakikisha maamuzihayatolewi wakati mwafaka.........................justice delayed is justice denied.....................
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Mpendazoe aruka kiuzi cha AG, Dk Makongoro [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Saturday, 17 September 2011 08:45 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

James Magai
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali pingamizi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG), alizoweka dhidi ya aliyekuwa mgombea Ubunge Jimbo la Segerea, Fredy Mpendazoe, katika uchaguzi mkuu mwaka jana.Katika kesi hiyo, Mpendazoe ambaye alikuwa akigombea kiti hicho kwa tiketi ya Chadema, anapinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa CCM, Dk Makongoro Mahanga.

Juni 6, mwaka huu Makakama iliamuru kesi hiyo iondolewe mahakamani hapo kwenda kufanyia marekebisho hati ya madai baada ya kubainika kuwa na dosari za kisheria, kisha kuiwasilisha tena.
Uamuzi wa mahakama ulitokana na maombi ya upande wa utetezi yaliyowasilishwa na Wakili Jerome Msemwa na Wakili wa Serikali, wakidai baadhi ya vituo vya kupigia kura havina majina, jambo ambalo litawafanya washindwe kujibu malalamiko hayo.

Hata hivyo, Mpendezoe kupitia kwa Wakili wake, Peter Kibatala, aliwasilisha mahakamani hati iliyofanyiwa marekebisho, AG ambaye ni mmoja wa walalamikiwa katika kesi hiyo akishirikiana na Wakili Msemwa walimwekea pingamizi wakidai marekebisho hayo hayaendani na maelekezo ya mahakama.

Walidai kuwa hati iliyofanyiwa marekebisho, mlalamikaji ameongeza madai mapya na kwamba, mpangilio wa aya umebadilika, hivyo wakaiomba mahakama itupilie mbali kesi hiyo kutokana na makosa hayo, jambo lililopigwa na Kibatala.

Jana, Jaji Profesa Ibrahim Juma, alitupilia mbali pingamizi hizo za AG na Makongoro na maombi yao yote.
Akitoa uamuzi huo, Jaji Juma alisema baada ya kuangalia hati zote za madai (ya kwanza na iliyofanyiwa marekebisho), amebaini kuwa pingamizi hizo hazina msingi na kwamba, hayakwenda kinyume na maelekezo ya mahakama.

Kuhusu mpangilio wa namba za aya katika hati iliyofanyiwa marekebisho, Profesa Juma alisema siyo la msingi kwa sababu baada ya kuondoa baadhi ya aya zilizobainika kuwa na dosari, ni dhahiri kuwa mpangilio wa namba hizo pia utabadilika.

Baada ya kutupilia mbali pingamizi hizo, Jaji Juma alipanga kesi hiyo kuendelea na usikilizaji wa awali Oktoba 27, mwaka huu.


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Mimi naona kuna matatizo kidogo katika kutoa taarifa za kesi za uchaguzi zinazoendelea mahakamani. Matatizo hayo kwa sehemu moja yanatokana na waandishi kutokuwa na taarifa ya kutosha juu ya madai ya msingi ya pande husika katika kesi na hoja za kisheria zinazotokana nayo. Upande wa pili ni baadhi ya waandishi kutoa taarifa zao kwa taathira ya ushabiki na misimamo yao ya kisiasa. Katika taarifa nyingi zilizoripotiwa na magazeti kama zilivyonukuliwa hapo juu kutoka katika vyanzo mbali mbali, kwa maono yangu ni kesi moja tu ndio imekuwa ikiripoiwa vizuri, yaani kesi ya jimbo la uchaguzi la Segerea. Kwa mfano, hamna hata kesi moja, kati ya kesi za majimbo ya Kawe na Ubungo ambapo kuna maombi ya kufuta kesi. Maombi yaliyoletwa kwa njia za mapingamizi ya kisheria yanataka baadhi ya aya katika Hati za Madai zifutwe kutokana na ima kutokuwa na taarifa za kutosha kuhusiana na tuhuma au hazina msingi wa kisheria. Pia kesi ya Ubungo haijawahi kutolewa maamuzi ya pingamizi kuhusiana na Hati kuwa batili zaidi ya kutolewa maamuzi ya kiwango cha dhamana ya gharama ya kesi muombaji anazopaswa kulipa. Muombaji hakuwa anaomba kusamehewa kutoa fedha hizo bali alikuwa anataka mahakama iamue ni kiwango gani?

Kwa mtizamo wangu, waandishi wetu wanatakiwa kuwa makini sana hasa katika kuripoti ukweli halisi wa tukio husika. Kama ni kuonesha msimamo au muelekeo wao katika tukio husika, haki yao ni kufanya hivyo kwa njia ya kutoa maoni na sio kuripoti tukio ndivyo isivyo.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Mgawo wakwamisha kesi ya ubunge Arusha [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Tuesday, 27 September 2011 19:50 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

Peter Saramba, Arusha
TATIZO la mgawo wa umeme umekwamisha kesi ya kupinga ubunge wa Godbless Lema, baada ya mawakili wa upande wa wadai, Alute Mughwai na Modest Akida, kushindwa kuandaa na kuwasilisha mahakamani na kwa mawakili wa utetezi muhtasari wa hoja zilizo kwenye hati ya madai.

Akiahirisha kesi hiyo juzi, Jaji Aloyce Mujulizi, aliagiza upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao kwa muhtasari ili kutoa nafasi kwa usikilizaji wa awali wa shauri hilo lililofunguliwa na wapiga kura watatu; Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo.

Hata hivyo, mawakili Mughwai na Akida wanaowakilisha wadai hao, aliieleza mahakama kuwa badala ya kuandaa na kuwasilisha muhtasari wa hoja zao juzi, walishindwa kufanya hivyo jana kutokana na umeme kukatika ofisini kwao.

"Ina maana waheshimiwa mawakili hamjafanikiwa kupata fedha za kutosha kununua majenereta kwa ajili ya tahadhari na dharura ofisini kwenu?" alihoji Jaji Mujulizi akikatiza maelezo ya Wakili Mughwai.
Akijibu swali hilo, Mughwai alisema anayo jenereta ofisini kwake, lakini kwa bahati mbaya mafuta yaliisha na hata alipohamia ofisini kwa mwenzake, nako ulikuwa umeme umekatika.

Kutokana na hali hiyo, Mughwai aliomba mahakama kuahirisha usikilizaji wa awali hadi siku nyingine, ili kutoa nafasi kwa upande wa utetezi kusoma na kujiandaa vyema kujibu hoja zao, huku pia akibainisha kuwa atakabiliwa na kesi nyingine Mahakama ya Rufaa kati ya Oktoba 7 na 11, mwaka huu.

Kutokana na mawakili wa utetezi, Method Kimomogoro na Timon Vitalis, kutokuwa na pingamizi kuhusu ombi hilo, Jaji Mujuluzi aliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 17, mwaka huu itakapokuja kwa usikilizaji wa awali na kumwagiza Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, George Hubert, kuanza mchakato wa kuomba muda wa kusikiliza na kuamua shauri hilo kutokana na kipindi kilichobaki kisheria kuwa kifupi.

Kwa mujibu wa kifungu cha 115, kifungu kidogo cha V ya sheria ya uchaguzi, shauri linatakiwa kusikilizwa na kuamuliwa ndani ya mwaka mmoja tangu kufunguliwa, hivyo kufanya kesi hiyo iliyofunguliwa Novemba mwaka jana kubakiwa na miezi miwili.

Pia, Jaji Mujulizi aliagiza upande wa utetezi upatiwe nakala ya kumbukumbu na mwenendo wa mahakama tangu kuwasilishwa kwa shauri hilo, usikilizaji na uamuzi wa pingamizi zilizowasilishwa na wajibu madai

Lema na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (CAG), huku msajili akiagizwa kutangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo ya mahakama siku, muda na mahali kesi hiyo itakaposikilizwa.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Mgombea wa CCM agonga mwamba kortini [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Saturday, 15 October 2011 07:53 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

Mwanja Ibadi, Kilwa
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, imetupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti cha ubunge wa Jimbo la Kilwa Kusini kupitia tiketi ya CCM, Ramadhani Madabida ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi, Selemani Bungara ***** wa CUF.Uamuzi huo umekuja baada ya mahakama kutoridhishwa na madai ya mlalamikaji katika kesi hiyo kuwa uchaguzi haukuwa wa haki na kwamba ulitawaliwa na vitendo vya wizi wa kura.

Madabida alidai kuwa wizi huo ulichangiwa na kukatika kwa umeme katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.Madabida pia alidai kuwa baadhi ya wapigakura wake halali, walizuiwa kupiga kura na kwamba katika kampeni zake, Bungara alidai kuwa yeye (Madabida) si mzawa wa jimbo hilo na kwa hiyo hastahili kuchagulia kuwa mbunge.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo katika ukumbi wa Mahakama ya Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, Jaji Fatuma Massengi, alisema baada ya kupitia ushahidi, amejiridhisha kuwa madai ya Madabida hayana msingi.

Alisema kwa msingi huo, mahakama imetupilia mbali kesi hiyo na kumtambua Bungara kuwa mbunge halali wa Jimbo la Kilwa Kusini.Jaji huyo pia alimwamuru mlalamikaji kulipa gharama zote za uendeshaji wa kesi hiyo.

Hata hivyo alisema mlalamikaji yuko huru kukataa rufaa katika mahakama ya juu, kama atahisi kuwa hakutendewa haki.Baada ya hukumu hiyo, wanachama, washabiki na wapenzi wa CUF,) walioonyesha vituko vilivyoambatana na maandamano huku wakiwa kutembeza jeneza la kuzikia walilodai kuwa ni kifo cha CCM, katika jimbo hilo.

Kwa upande wae, Bunga alitokwa na machozi ya furaha baada ya kutangazwa kuwa ni mbunge halali wa Kilwa Kusini.Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa Septemba 19 na kumalizika Oktoba 13 mwaka huu, ilikuwa na mashahidi 39.

Mashahidi 20 kati hao walikuwa wa upande mlalamikaji na 19 wengine walikuwa wa upande wa mlalamikiwa, [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
KESI ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa Jimbo la Ilemela ambayo ilikwama kuanza kusikilizwa jana, leo itaanza kusikilizwa mchana majira ya saa 8 mahakama kuu kanda ya Mwanza.

Kesi hii ambayo itasikilizwa leo mbele ya Jaji Gadi Mjemas inamkabili Mbunge Jimbo la Ilemela Highness Samson (Chadema) ambaye atasimamiwa na wakili Tundu Lissu. Tayari Lisu amewasili Mwanza na asubuhi hii amefika Mahakamani na kukutana na mawakili wa pande zote mbili ambapo baada ya kujadilia mambo kadhaa ya kisheria, walikwenda kuonana na jaji na waliporejea walieleza Kesi imepangwa kuanza Majira ya Saa 8 mchana.

Katika kesi hiyo, Namba 12/2010 walalamikaji wanaopinga matokeo ya uchaguzi ni wakazi watatu wa Ilemela Yusufu Masegeja Lupilya, Nuru Ramadhani Nsubugu na Beatus Martin Madenge washitakiwa wakiwa ni mbunge Highness Samson, msimamizi wa Uchaguzi wa jimo la Ilemela ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Willson Kabwe na Mwanasheria mkuu wa serikali.


Matokeo ya uchaguzi huo yanayopingwa ni kuwa Highness Samson aliweza kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo la Ilemela kwa kumshinda Anthony Diallo wa CCM kwa kura 31,269 dhidi ya kura 26,270 hii ikiwa ni tofauti ya kura 4,999.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]KESI ZA UCHAGUZI MKUU:CUF wabwagwa, Chadema, CCM wakwama [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Tuesday, 18 October 2011 21:08 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

Abdallah Bakari, Mtwara na
Frederick Katulanda, Mwanza
WANAODAIWA kuwa wafuasi wa CUF wamefanya vurugu mahakamani, kuvamia maduka na kuiba mali na kutaka kuichoma moto nyumba ya Mwenyekiti CCM Mkoa wa Mtwara, kwa kile kilichoelezwa kuwa kutoridhishwa na hukumu ya Mahakama Kuu iliyompa ushindi Mbunge wa CCM, Asnain Murji, dhidi ya mpinzani wake, Hassan Uledi wa CUF.

Uledi alifungua kesi mahakamani hapo kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana Jimbo la Mtwara Mjini, yaliyompa ushindi Murji wa CCM. Baada ya kusikilizwa kwa takriban mwaka mmoja, kesi hiyo jana ilitolewa hukumu na kumhalalisha Murji.Muda mfupi baada ya kutolewa hukumu hiyo jana, wafuasi wanaodaiwa kuwa wa CUF walijikusanya kuelekea ofisi ya chama hicho wakiwa njiani, inadaiwa waliishambulia nyumba ya kada huyo wa CCM iliyopo karibu na ofisi hiyo kwa kurusha mawe.

Tukio hilo lilifuatia na kitendo cha wafuasi hao kwenda dukani kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara, Dadi Mbullu, ambako walipora mali na kumwaga dizeli kwenye kuta za nyumba hiyo kwa lengo la kuichoma moto.
Hata hivyo, wafuasi hao hawakufanikiwa kuchoma moto nyumba hiyo baada ya polisi kuwasili dakika chache baadaye na kuwatawanya kwa risasi za mpira.

Mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa, alisema wafuasi hao wa CUF, walianza kwa kurusha mawe dukani humo jambo ambalo lilimfanya muuzaji kukimbia, hali iliyotoa upenyo wa kuingia ndani na kupora mali.
"Walianza kwa kurusha mawe, muuzaji akakimbia ndipo walipoingia dukani na kupora bidhaa mbalimbali. Wengine walikuwa na madumu ya mafuta… polisi ndiyo waliowatawanya kwa kupiga risasi hewani," alisema.

Vurugu hizo zilisababisha maduka yaliyopo karibu na eneo hilo likiwamo duka la Murji kufungwa kwa hofu ya kuporwa. Wakati hayo yakiendelea, baadhi ya magari ya polisi waliobeba silaha za moto, yalikuwa yakizunguka na kusababisha hofu kwa wananchi.
Wakati tukio hilo linatokea, Mbullu hakuwapo nyumbani kwake na taarifa zinasema alikuwa safarini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.
Jithada za kuwapata viongozi wa CUF wa Mtwara mjini kuzungumzia tukio hilo hazikuzaa matunda, baada ya simu zao kutopatikana na hata mwandishi wa habari hizi alipofika ofisini kwao zilikuwa zimefungwa.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Masoud Mbengula, alieleza kusikitishwa kwake na tukio hilo na kutupa lawama kwa polisi kwa kutozifanyia kazi kwa umakini taarifa ambazo chama hicho kiliripoti mapema.

"Nawalaumu polisi katika hili, sisi (CCM) tuliripoti juu ya kuwapo kwa vurugu iwapo wangeshindwa kesi hii siku mbili kabla…walikuwa wakihamasishana kwenda kwa wingi mahakamani na kuwa tayari kwa lolote iwapo watashindwa," alisema Mbengule na kuongeza:
"Hizi si siasa, huu ni uhalifu ambao unapaswa kupingwa kama uhalifu mwingine …wameiba mali za dukani, wamemwagia mafuta ukuta kwa lengo la kuchoma moto unawezaje kuita hizo ni siasa?"

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maria Nzuki, alisema asingeweza kuzungumzia tukio hilo kwa sababu alikuwa safarini Dar es Salaam.Awali, akisoma hukumu hiyo iliyochukua saa moja na nusu, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Seleman Kihiyo, alisema mlalamikaji ameshindwa kuthibitisha madai yake, hivyo ameamua kutupilia mbali ombi lake la kutaka kutengua matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 31, mwaka jana na kumpatia ushindi Murji.

Miongoni mwa hoja ambazo mlalamikaji aliwasilisha Mahakamani hapo ni madai kuwa, walinyimwa haki ya kuhesabu kura, kucheleweshwa kutangazwa kwa matokeo na baadhi ya fomu za matokeo kutosomeka vizuri.

Jaji Kihiyo alisema madai hayo yote yameshindwa kuthibitika mbele ya mahakama, hivyo ameamua kulitupilia mbali shauri hilo na kuamuru mlalamikaji kumlipa mlalamikiwa gharama zote za uendeshaji kesi na kwamba, anaweza kukata rufaa iwapo hajaridhishwa na uamuzi huo.

Umati wa watu ulihudhuria mahakamani hapo, kusikiliza kesi hiyo yenye mashahidi watatu, wawili wakiwa wa upande wa mlalamikaji na mmoja upande wa mlalamikiwa. Hata hivyo, hawakupata fursa nzuri ya kusikiliza hukumu hiyo kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya vipaza sauti vilivyofungwa nje.
Wakati hayo yakiendelea mkoani Mtwara, kesi namba 12/2010 ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa Jimbo la Ilemela jana ilishindwa kuanza kusikilizwa baada ya mashahidi wawili kushindwa kufika mahakamani.

Wakili wa Mbunge Highness Kiwia (Chadema), Tundu Lisu, alisema jana baada ya kuahirishwa kesi hiyo kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na kukosekana kwa mashahidi wa upande wa walalamikaji.

Alisema kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Oktoba 21, mwaka huu.
Msajili wa Mahakama Isaya Arufani, alieleza kuwa kesi hiyo imeahirishwa hadi Ijumaa itakapoanza kusikilizwa na Jaji Gadi Mjemas.Katika kesi hiyo, walalamikaji wanaopinga matokeo ya uchaguzi ni wakazi watatu wa Ilemela, Yusuf Lupilya, Nuru Nsubugu na Beatus Madenge.

Washitakiwa ni Kiwia, Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Willson Kabwe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).Katika matokeo hayo yanayopingwa mahakamani, Kiwia alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 31,269 dhidi ya mpinzani wake, Anthony Diallo wa CCM aliyepata kura 26,270.


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Kwa kauli ya Jaji Kiongozi kwamba Mahakama haijawezeshwa fedha za kuendesha kesi za uchaguzi nini itakuwa hatima ya kesi hizi? Waziri wa Sheria ameshaziongezea kesi hizi muda wa ukomo na miezi miwili imeshaisha. Kisheria Waziri hana tena uwezo wa kuongeza ukomo baada ya miezi hii sita ya nyongeza kuisha.

Kwa upande wa Dar Es Salaam tu kuna kesi tatu za kupinga matokeo ya uchaguzi wa wabunge. Jimbo la Kawe, Mr Mbatia anapinga kwa sababu, pamoja na mambo mengine kwamba kulikuwa na ukiukaji mkubwa wa sheria ya uchaguzi kwa upande wa Mndee na Tume ya Uchaguzi kwa kumuachia Mh. Mdee kutumia lugha ya kashfa dhidi ya Mbatia pamoja na fujo.

Katika jimbo la Segera mheshimiwa Mpendazoe anapinga matokeo ya uchaguzi kwa sababu mbalimbali za ukiukaji wa sheria ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kutumika fomu zisizo rasmi katika kujumulisha matokeo ya uchaguzi, uwepo wa idadi hewa ya wapiga kura pamoja na vituo hewa. Ubungo, Ngumbi anapinga matokeo ya uchaguzi kwa sababu mbalimbali ikiwemo makosa ya msingi katika kurekodi na kujumlisha idadi ya kura kulikofanya jumla ya kura alizopata Mnyika na Ngumbi kuzidi kura zote halisi zilizopigwa, uingizwaji wa laptop kumputa zisizorasmi katika ukumbi wa kujumlisha kura na kuingia watu wengi katika ukumbi wa kujumlisha kura wasioruhusiwa kisheria.
 
Na Happiness Katabaza

JAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam John Utamwa , jana ilishindwa kutoa uamuzi wa ama hati ya madai katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 iliyofunguliwa na aliyekuwa Mgombea Ubunge(NCCR-Mageuzi) dhidi ya mbunge Jimbo hilo Halima Mdee(Chadema) ifanyiwe marekebisho au la kwa maelezo kuwa bado hajakamilisha kuandaa uamuzi huo.

Wakili wa Mbatia, Mohamed Tibanyendera aliikumbusha mahakama hiyo kuwa jana kesi hiyo ilikuja kwaajili ya mahakama kutoa uamuzi huo na kwamba pande zote mbili zipo tayari kwaajili ya kupokea uamuzi huo.

Hata hivyo kwa upande wake Jaji Utamwa alisema hataweza kutoa uamuzi huo jana kwasababu bado hajamaliza kuandaa uamuzi huo hivyo akaiarisha kesi hiyo ya uchaguzi hadi Septemba 29 mwaka huu, ambapo atakuja kuitolea uamuzi.

Hatua hiyo ya mahakama kutaka kutoa uamuzi kuhusu hati hiyo ya madai, kunafuatia pingamizi lilowasilishwa na wakili wa Mdee, Edson Mbogoro la kuiomba mahakama hiyo imwamuru mlalamikaji aifanyie marekebisho hati yake ya madai na kuyaondoa baadhi ya madai ambayo Mbatia anadai kuwa katika mikutano ya kampeni Mdee alimwita yeye kuwa ni Fataki anayefanya mapenzi na watoto wa shule, kibaraka wa CCM na kila wiki analipwa sh milioni 80 na CCM hivyo kuwataka wapiga kura wa jimbo la Kawe wasimchague Mbatia.

Mdee anadai tuhuma hizo zilizoelekezwa kwake na Mbatia ndani ya hati hiyo ya madai zinamletea kinamkera na hataweza kuziandalia utetetezi na kusisitiza kwa kuomba mahakama hiyo imwamuru Mbatia aondee hizo tuhuma kwenye hiyo hati ya madai.

Novemba 25 mwaka 2010 Mbatia alifungua kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo ambayo yalimtangaza Halima Mdee(CHADEMA) kuwa ndiye aliyeshinda na ataliongoza jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mitano.

Chanzo:Chazeti la Tanzania Daima la Septemba 22 mwaka 2011.
 
Na ndio maana kakimbilia vunjo,na kule mrema anampiga tena
 
Acheni UJINGA hii habari ni ya zamani sana,mleta uzi anajaribu kuwavuruga ukawa
 
Asubiri viti maalum,hata mrema alimuambia!Ila sasa cjui kama mzee wa viwango atamfikiria??
 
Habari ya 2011, Mbatia alishafuta hiyo kesi zamani sana na kukubaliana na ubunge wa Mdee. Mleta mada anajaribu tu kuvuruga watu na inaonekana anafanikiwa kidoogooo. Mbatia Novemba ataingia bungeni kuwakilisha jimbo la Vunjo. Tulieni daawa iingie khaaa
 
Back
Top Bottom