Kesi za watu maarufu duniani na hukumu zake

Kesi za watu maarufu duniani na hukumu zake

Lavan Island

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2015
Posts
2,377
Reaction score
2,048
Visa na mikasa ya kesi maarufu duniani na hukumu zake

Visa na Vikasa ya Kesi Maarufu Duniani na Hukumu Zake ni mwanzo wa vitabu nitakavyokuwa nikivitoa kwa awamu ambapo vitabu hivyo vitakuwa na mkusanyiko wa kesi mbalimbali zilizowahi kutokea katika nchi mbalimbali duniani na kuvuta hisia za watu wengi.

Katika kitabu hiki cha toleo la kwanza kuna kesi nyingi za mauaji ambapo mengi yanahusisha masuala ya mapenzi na mahusiano pamoja na sababu nyingine za kibinadamu.
Mojawapo ya kesi hizo ni ile ya Vincent Brothers wa New York nchini Marekani ambapo profesa wa wadudu alifanikisha upelelezi wa kesi ya mauaji ya familia yake dhidi yake.

Vincent alifunga ndoa na Joanie Harper. Hata hivyo, ndoa yao ilivunjika mwaka mmoja baadaye kutokana na kile kinachodaiwa Vincent kutokuwa mkweli kwa Joanie aliyedai mumewe huyo hakumweleza kuhusu ndoa zake mbili zilizovunjika huko nyuma. Hata hivyo, walioana tena mwaka 2003, lakini Vincent alihama katika nyumba waliyokuwa wakiishi na mkewe huyo, April 2003.

Maisha yao ya ndoa hayakuwa ya amani, ingawa Joanie Harper alikuwa akimpenda sana Vincent na alitamani siku moja ndoa yao iwe imara.

Inadaiwa Vincent aliua wanafamilia wake. Kitendawili ambacho wapelelezi wa kesi hiyo walitakiwa kukitegua ni kuthibitisha kama Vincent alikuwa Bakersfield, California wakati mauaji ya familia yake yakitokea au alikuwa Ohio kama alivyodai. Polisi walikuwa na uhakika Vincent ndiye aliyeua familia yake na hiyo ilitokana na taarifa kutoka kwa jirani yake mmoja aliyedai kumuona Vincent akiwa nje ya nyumba inapoishi familia yake hapo Bakersfield muda yalipotokea mauaji.

Askari upelelezi walianza kufuatilia safari ya Vincent kutokea Barkersfield hadi Columbus Ohio. Askari hao waliamini Vincent alipanga safari hiyo makusudi ili kutengeneza mazingira kwamba wakati mauaji yanatokea hakuwapo katika mji husika.

Waligundua Vincent alisafiri kwa ndege hadi Ohio Julai 2, 2003, alikodi gari aina ya Dodge Neon katika Kampuni ya Doller Rent –A-Car. Polisi walipofuatilia kampuni hiyo waligundua wakati gari hilo likiwa mikononi mwa Vincent liliendeshwa umbali wa maili 5,400, umbali ambao unatosha kabisa kwa Vincent kwenda Bakersfield na kurudi Ohio na ziada. Pia Polisi hao walibaini Vincent aliendesha gari hilo kwa umbali wa maili 4,500 kwa siku tatu.

Lakini Vincent alizidi kusisitiza hakuwahi kutoka nje ya Ohio. Vincent alidai wakati mauaji yanatokea alikuwa umbali wa zaidi ya maili 2,300 na kuhoji ingewezekana vipi awepo katika mji wa Bakersfield mchana wa Julai 6, 2003 auwe familia yake na kisha kurudi Ohio jioni ya Julai 7, Julai wakati hata kaka yake anakiri siku hiyo ya mauaji alikuwa Ohio?

Iliwachukua Polisi takriban miaka mitatu kukusanya ushahidi wa kumtia hatiani Vincent. Askari wawili wa FBI walikuwa na uhakika Vincent ndiye muuaji, lakini ilikuwa vigumu kwao kuthibitisha Vincent alikuwa Bakersfield Califonia siku yalipotokea mauaji na si Ohio.

Ilibidi kumhusisha Profesa wa wadudu katika upelelezi. Askari wa upelelezi wa FBI walipata wazo la kupeleka rejeta na air filter ya kuchuja hewa ya gari alilokuwa amekodi Vincent alipokuwa Ohio kwenye kituo cha uchunguzi wa wadudu cha Bohart Museum Entomology ambako Profesa Lynn Kimsey, aliongoza kazi hiyo ya uchunguzi ambao ndio uliotegua kitendawili hicho.

Katika ripoti yake Profesa Kimsey alibaini baadhi ya wadudu waliokutwa kwenye vifaa hivyo wanapatikana eneo la Magharibi, na wengine waliokutwa katika vifaa hivyo hupatikana kwa wingi katika eneo la California.

Kuonekana kwa wadudu hao kulibainisha kwamba gari hilo liliendeshwa usiku kuelekea California na si mchana. Kwa ujumla Profesa huyo alikamilisha ripoti yake kwa kusema, hakuna wadudu wanaoruka mchana waliokutwa kwenye vifaa hivyo.

Huo ulikuwa ni ushahidi wa kitaalamu ulisababisha Vincent kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa kosa la kuua familia yake. Matukio yote haya na mengine yamekuwa na mvuto mkubwa na bila shaka, yataendelea kubaki katika mvuto wake kwenye kitabu hiki.

Jipatie nakala yako mapema kwa kuwasiliana na muandishi 06931311
 
Back
Top Bottom