Kete ya mwisho ya medali kwa Tanzania Olimpiki 2024

Kete ya mwisho ya medali kwa Tanzania Olimpiki 2024

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274

Kama sio Alphonce Simbu ni Gabriel Geay ambao kesho Agosti 10 watakuwa katikati ya miamba ya dunia ya mbio ndefu kusaka medali ya Olimpiki msimu huu.

Nyota hao wa mbio ndefu nchini ndiyo tegemeo kubwa la medali kwa timu ya Tanzania ambayo kesho Jumamosi itakuwa barabarani ikichuana na magwiji wengine wa dunia huku 'dada' zao, Jackline Sakilu na Magdalena Shauri wakifunga hesabu Keshokutwa Jumapili upande wa wanawake.

Nyota hao wako mjini Paris Ufaransa tangu Agosti 7 wakiwa na kocha wao, Anthony Mwingereza, tayari kwa mbio hiyo itakayowashindanisha na nyota bora wa muda wote wa masafa marefu duniani, mhabeshi Kenenisa Bekele na Mkenya Eliud Kipchoge.

Simbu atachuana na Kipchoge kwa mara nyingine kwenye Olimpiki ya Paris baada ya ile ya Rio 2016 nchini Brazil alipokwenda naye sambamba na kuachwa mwishoni na Mkenya huyo aliyekuwa bingwa na Simbu kumaliza kwenye tano bora.

Akizungumza na Mwananchi, Simbu amesema nafasi ya medali kwa Tanzania msimu huu ipo, akiahidi mojawapo itakuwa ni yake, akitaka kuandika rekodi nyingine baada ya ile ya 1980 Tanzania ilipotwaa medali mbili za fedha kwenye Olimpiki ya Moscow, Russia.

Nahodha huyo wa Tanzania mwenye medali ya shaba ya dunia na ya fedha ya Jumuiya ya Madola anataka kuandika rekodi kwenye Olimpiki, japo hajasema ni medali gani kati ya dhahabu, fedha au shaba anaitaka kwenye Olimpiki hiyo.

Simbu atakayewaongoza wenzake katika kete hiyo ya mwisho kwa Tanzania amesema hawatarajii kurudi mikono mitupu msimu huu.
Snapinsta.app_454626329_1222344188763933_4000264187509448982_n_1080.jpg

 
Kama wamarekani na wajamaika wapo.......!!!!
 
Back
Top Bottom