Keto weight loss tablets mlio jaribu tupeni matokeo

Keto weight loss tablets mlio jaribu tupeni matokeo

Nahisi mnatafuta vidonda vya tumbo.

kuna mdada ninapofanyia kibarua kila siku anabadilisha mimaji ya sijui:-
Hiliki
Mdalasini
Mara matango
Mara diet
Mara malimao ajikondeshe lakini waaapi [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] anaendelea kuwa chibonge [emoji1][emoji1][emoji1] nidhamu ya kula hana atapunguaje??

Achaneni na hiyo midawa fanyeni mazoezi ya mepesi ya kukimbia kwa dk 20 huku umevaa jaketi siyo kawoshi wala singlendi ili mwili uvuje jasho la kutosha na kunywa maji ya mengi. Kula vyakula vyenye wanga kigodo na matunda mengi.

Menu ya mchana kama unafanya kazi ofisini kula matunda tu na maji mengi, usiku wanga kidogo na mbogamboga au white meat (kidongo) achana na bia, soda na juisi za viwandani ila vinywaji vikali ruksa kama ni lazima saaana

matokeo ni baada ya wiki 3 hadi 4,

Usisahau kikombe kimoja cha maji ya moto yenye limao kila asubuhi.
Nilijua K vant utaikataza kumbe yenyewe fresh tu
 
Kuna nyingine unakula kuku, samaki au mayai ya kuchemsha pamoja na salad 🥗 kwa lunch na dinner.

Breakfast ndizi mvivu moja na mayai mawili ya kuchemsha.

Maji ni muhimu.
hiyo ni kusema acha wanga wote na acha sukari zote, ni rahisi sana japo huwa watu huisi aiwezekani hiyo nimeona na nimeipata kwa bwana BOAZ MKUMBO na wengi wamepata matokeo makubwa na si katika uzito na vitambi tuu bali katika magonjwa yote ya lishe.
 
Looking forward to give out the feedback my love. Maji nakunywaga hata lita 3.5 per day.

Hapo nikiongeza na punje za vitunguu swaumu aaah, mambo safi[emoji28][emoji28]
Niliacha kutumia
-Soda/vinywaji vyote vya kiwandani
-Vitu vyote vinavyotengenezwa na ngano
-Wali
-juice yoyote ya matunda ya kutengeneza
-Vitu vyenye sukari nyingi (hii haikunisumbua maana hata mimi sivipendi)


Asubui nakunywa maziwa tu
Mchana nakula mboga za majani na ugali kidogo/Nyama ya kuku maana ya Ng'ombe pia niliiacha/Samaki
-Katika mboga siweki mafuta mengi

Usiku nakula Tango,Parachichi nalala

Katika kutwa yangu nzima lazima Maji lita2, machungwa mawili


Week1 tumbo lote likaisha .. nikivaa sasa hivi nakua kama nmevaa mkanda wa kubana tumbo
Toka kilo 70 mpk 62 now, najiskia mwepesi ajabu
 
Niliacha kutumia
-Soda/vinywaji vyote vya kiwandani
-Vitu vyote vinavyotengenezwa na ngano
-Wali
-juice yoyote ya matunda ya kutengeneza
-Vitu vyenye sukari nyingi (hii haikunisumbua maana hata mimi sivipendi)


Asubui nakunywa maziwa tu
Mchana nakula mboga za majani na ugali kidogo/Nyama ya kuku maana ya Ng'ombe pia niliiacha/Samaki
-Katika mboga siweki mafuta mengi

Usiku nakula Tango,Parachichi nalala

Katika kutwa yangu nzima lazima Maji lita2, machungwa mawili


Week1 tumbo lote likaisha .. nikivaa sasa hivi nakua kama nmevaa mkanda wa kubana tumbo
Toka kilo 70 mpk 62 now, najiskia mwepesi ajabu
Umetuokoa wengi, nina kilo 20 za kuziondoa ngoja nifanye hii mpaka Dec natumai zitakua zimetoka.
 
Hii ndiyo habari ya mjini, mlioijaribu tuelezeni matokeo.
View attachment 1144865
Siamini katika hili kbs;
Binafsi ni shuhuda wa mazoezi na diet,
Nimeanza mazoezi Jan 12 2019 nikifanya jogging 3kms baadae 8-12 kwa siku. Nimefanikiwa kupunguza 12 Kg.

Nimepunguza kula vyakula vya sukari, wanga na mafuta. Kimsingi portion ya menu pia nimepunguzq kbs na usiku mara nyingi nakula matunda au glass ya mtindi.

Kinywaji ni wine hasa Drosthoff tena occursionally mara 1 baada ya wiki mbili.

Kila ninaposafar nahakikisha nina nguo zangu za jogging na najutahidi kufanya hivyo nikiamimi ndio mafanikio ta afya yangu.

Nimepunguza kabisa mwili hususani tumbo sema hasara ninayokutana nayo ni nguo nyingi kunipwaya nalazimika kununua nguo mpya zinazonitosha.

Wana-encourage mazoezi kuliko hizo keto sijuiii...

Nawasilisha!
 
Stress huwa zibanipa challenge sana. Nikiwa na stress ninakula na kunywa mpaka msala uishe ninajikuta niko kwenye 88-90 kg mbaya zaidi BP inakuwa juu lakini nikishuka kwenye 75-80 BP is normal.
Pole sana jitahidi kupata mda wa kutembea tu angalau dk 30 kwa siku utakuwa sawa kabisa
 
Back
Top Bottom