Keto weight loss tablets mlio jaribu tupeni matokeo

Keto weight loss tablets mlio jaribu tupeni matokeo

Mrejesho nimetoa kilo 5 ndani ya wiki mbili
Breakfast:
two boiled eggs with fruit slices

Plenty of water to drink

Lunch @16:00
Any thing with salad .

Half an hour walk daily
umekazana kweli
hongera
mimi sasa hivi namaintain
 
Nahisi mnatafuta vidonda vya tumbo.

kuna mdada ninapofanyia kibarua kila siku anabadilisha mimaji ya sijui:-
Hiliki
Mdalasini
Mara matango
Mara diet
Mara malimao ajikondeshe lakini waaapi [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] anaendelea kuwa chibonge [emoji1][emoji1][emoji1] nidhamu ya kula hana atapunguaje??

Achaneni na hiyo midawa fanyeni mazoezi ya mepesi ya kukimbia kwa dk 20 huku umevaa jaketi siyo kawoshi wala singlendi ili mwili uvuje jasho la kutosha na kunywa maji ya mengi. Kula vyakula vyenye wanga kigodo na matunda mengi.

Menu ya mchana kama unafanya kazi ofisini kula matunda tu na maji mengi, usiku wanga kidogo na mbogamboga au white meat (kidongo) achana na bia, soda na juisi za viwandani ila vinywaji vikali ruksa kama ni lazima saaana

matokeo ni baada ya wiki 3 hadi 4,

Usisahau kikombe kimoja cha maji ya moto yenye limao kila asubuhi.
Wanga sio nzuri usiku. Unatakiwa kula wanga aidha asubuhi au mchana na usiku matunda au mtindi. Vingine ni sawa
 
Wanga sio nzuri usiku. Unatakiwa kula wanga aidha asubuhi au mchana na usiku matunda au mtindi. Vingine ni sawa
Wanga hasa ule asubuhi ikibidi, mchana wanga kidogo Protein nyingi jioni kipande cha kuku au samaki na matunda
 
Niliacha kutumia
-Soda/vinywaji vyote vya kiwandani
-Vitu vyote vinavyotengenezwa na ngano
-Wali
-juice yoyote ya matunda ya kutengeneza
-Vitu vyenye sukari nyingi (hii haikunisumbua maana hata mimi sivipendi)

Asubui nakunywa maziwa tu
Mchana nakula mboga za majani na ugali kidogo/Nyama ya kuku maana ya Ng'ombe pia niliiacha/Samaki
-Katika mboga siweki mafuta mengi

Usiku nakula Tango,Parachichi nalala

Katika kutwa yangu nzima lazima Maji lita2, machungwa mawili

Week1 tumbo lote likaisha .. nikivaa sasa hivi nakua kama nmevaa mkanda wa kubana tumbo
Toka kilo 70 mpk 62 now, najiskia mwepesi ajabu
Eeh Mungu nipe nguvu za kuacha wali.
Unavyofanya nafanya karibu vyote plus mazoezi lakini napungua taratibu sana labda wali ndio tatizo
 
Eeh Mungu nipe nguvu za kuacha wali.
Unavyofanya nafanya karibu vyote plus mazoezi lakini napungua taratibu sana labda wali ndio tatizo
kupungua taratibu ndo vizuri ili nyama zisitepete, ukitumia dawa zile zakuharisha unapungua faster but madhara ka yote nyama za mwili utazibeba kuziweka kwenye nguo hahaahaaaa
 
Eeh Mungu nipe nguvu za kuacha wali.
Unavyofanya nafanya karibu vyote plus mazoezi lakini napungua taratibu sana labda wali ndio tatizo
Wali/viporo
Juice/soda/bia
Mm nakulaga vijiubwabwa kiduchu mboga tele
Na hata ukila basi usishibe
 
kupungua taratibu ndo vizuri ili nyama zisitepete, ukitumia dawa zile zakuharisha unapungua faster but madhara ka yote nyama za mwili utazibeba kuziweka kwenye nguo hahaahaaaa
Mi sitaki sasa hivyo kupungua huku uso unakosa nuru na manyama kushuka
 
Wali/viporo
Juice/soda/bia
Mm nakulaga vijiubwabwa kiduchu mboga tele
Na hata ukila basi usishibe
Viporo sili ila wali nakula karibu kila siku na wala sili sana.
Bia sinywi na soda pia.
Nahisi mchawi wangu ni wali
 
Aisee Mie nilianza mazoezi ya kukimbia na kutembea Kila siku jioni ili nikonde ila niliishia njiani sababu sili mbogamboga zaidi ya kisamvu, pia ni muumini mzuri wa Wali na maharage sasa sijui itakuwaje
 
Eeh Mungu nipe nguvu za kuacha wali.
Unavyofanya nafanya karibu vyote plus mazoezi lakini napungua taratibu sana labda wali ndio tatizo
Mchawi wali tena wali wa usiku

Wali ndondo[emoji39]
 
Back
Top Bottom