Kevin De Bruyne: Mpishi wa mabao ya Man City EPL asiyeimbwa

De Bruyne jamaa fundi sana.. Huwa sichoki kumtazama na kumfuatilia..

Ananifurahishaga huyu fundi wa kiBelgiji jinsi anavyokuwaga mwekundu baada ya mechi!!!
 
Yeah huyu kijana anasakata kabumbu kinoma.
Afu hata hazungumziwi kivile kama kina Labile n.k
 
huyu alikuwa mchezaji bora wa mwaka pale ujerumani baada ya kutokea pale darajani mimi nafurahi sana huyu mchezaji akipangwa namba 10 ni hatari lakini pep anampanga katikati duu naumia sana anavitu vya kutisha halafu anakitu cha ziada yaani miguu yote ni balaaa
 
Sawa, sisi washabiki tunaumia MNO alivyotua darajani, LKN mbona msimu uliopita hazard alifunika vibaya
 
Umemaliza kila kitu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…