Kevin De Bruyne: Mpishi wa mabao ya Man City EPL asiyeimbwa

Kevin De Bruyne: Mpishi wa mabao ya Man City EPL asiyeimbwa

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
18,960
Reaction score
67,654
Bila shaka huyu ni kiungo mchezeshaji bora kwasasa katika EPL, huyu jamaa ndio injini ya Man City katika mabao.

Mpaka leo nashangaa ni kwanini Chelsea walikubali kumuuza kirahisi.

Kevin De Bruyne (KDB) anajua kupiga pasi za mwisho zenye macho kwenda kwa akina Aguero na Gabriel Jesus ambao kazi yao ya kupachika mabao inakuwa rahisi. Pia anajua sana kuanzisha mashambulizi ya hatari kwenda kwenye lango la adui.

KDB ndio injini ya mashambulizi katika kikosi cha Pep Guardiola kama ilivyokuwa kwa Xavi wakati Pep akiwa Barcelona. Kwasasa kama utacheza na Man City basi mtu wa kwanza kumchunga ni KDB vinginevyo utajitafutia matatizo .

Tuache unazi, tuache ushabiki ni wakati sasa wa kutambua mchango wa KDB kama mmoja ya viungo bora EPL kama si Ulaya nzima.
 
Mpaka leo nashangaa ni kwanini Chelsea walikubali kumuuza kirahisi..
By then kulikuwa na mtaalam Lampard, Hazard, Oscar na Willian alikuwa ndo kasajiriwa. Isingekwua rahisi kuwafurahisha wote na ilikuwa lazima mmoja asepe/asepeshwe. Pia KDB hakuwa kwenye level aliyonayo sasa by the time anaondoka Chelsea na labda ndio sababu walimuacha aende.
 
Huku kwetu tunamuita Albino
589692672-1170x677.jpg
 
By then kulikuwa na mtaalam Lampard, Hazard, Oscar na Willian alikuwa ndo kasajiriwa. Isingekwua rahisi kuwafurahisha wote na ilikuwa lazima mmoja asepe/asepeshwe. Pia KDB hakuwa kwenye level aliyonayo sasa by the time anaondoka Chelsea na labda ndio sababu walimuacha aende.
hoja mjarabu, naunga mkono!
 
Back
Top Bottom