Nyie mnaowaambia watu warudi wawe kama Kevin mnajua history ya Kevin, income bracket ya familia yake, family connections zake na mengine kama hayo?
Hata kama Kevin hana degree, anayo pedigree, sasa waswahili wana msemo "ukitaka kumuiga Tembo kunya utapasuka msamba". Kuna wengine hatuna pedigree bongo wala backing ya Holy Roman Empire, tupo huku tumejibanza, na hata kama tungekuwa nayo hatuhusudu michongo ya migongo ya pedigree. Si kweli kwamba mtu yeyote mwenye jitihada anaweza kufanya hizi kazi, bongo kuna unwritten rules, ndiyo maana BOT walijazana kama ng'ombe mnadani.
Kwa hiyo tupe mfano wa mtoto wa Uswazi aliyefanza vitu, hapo kidogo utawagusa watu, ingawa mimi nasimama pale pale kwamba kila mtu kivyake vyake.
Lakini hawa watoto wa Upanga / Oysterbay friji open wameenda kwenye parties za Mkapa wakati Mkapa Waziri wa Utamaduni early 1980s huwezi kujilinganisha nao kabisa. Wengine majina yetu hayajulikani Rotary Club, Lions Club wala networks za Gymkhana Club sasa hatuwezi kujilinganisha na wenye networks za nchi.
Si mnaona wenyewe, huku Kevin Twisa sijui, huku nani Makamba sijui, hata wewe uje na videgree vyako vya Ivy League unaweza kuwa frustrated tu. Ndio maana kwa usawa huu tunajikita tu, Ma-Wall St, Ma-Silicon Valley, Ma-dirty basements, ma nursing homes, Ma-Batani, ma-Buruda, usawa wa Twiga mnyonge minazini hatutaki kuusikia mpaka kieleweke vizuri, humrudishi mtu.Na hivi rais ndiyo huyo officially taahira ndiyo kabisaaaaa.
Kama vile visoda vilivyokuwa vinasema, nakwambia "Jaribu Tena".