Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Duh sijui ni ugeugeu au ni ufyatu... hazikupita siku nyingi watu walisema lugha ya "wanyonge" haipo. Na kuwa ni lugha mbaya... mara hii watu wameanza kusema kuna wanyonge? kha!! Watu walikuwa wanatakiwa kuwa wazalendo na waoneshe uzalendo; sasa wanalipishwa kodi ya "uzalendo" wanang'aka! uzalendo kumbe mchungu.
Sijui kwanini isiwe kodi ya "kuwa Mtanzania"? Binafsi sijaielewa na sijataka hata kuchukua muda kuielewa... kama uzalendo unaweza kuundiwa kodi kwanini tusije na kodi ya wanaozungumza sana.. halafu ianzie Bungeni... Halafu iwepo kodi ya watu wanaosema "serikali imepanga" kila anayesema hivi analipa kodi. Au kodi ya watu wanaosema "Serikali imedhamiria kujipanga"... au "Serikali iko mbioni kuanzisha mchakato".
Labda tuwe na vikodi vingine vingine vidogo vidogo maana hatujui kama kila anayelipa mihamala hii kweli ni mzalendo na si fisadi... AAh! labda tuwe na kodi ya wasio mafisadi (hili neno sitashangaa litaanza kurudi tena). Mafisadi.
Mafisadi Wazalendo? Well!! halafu tunawalima kodi... Ila labda liwekwe punguzo la "wanyonge" kama hawa watu bado wapo Tanzania.