Khaa! ..Hebu na Tujitambue...


Msisahau nyumba ndogo nyingine hupata promotion ya nguvu na hatimaye kuwa nyumba kubwa...hivyo msibweteke na kujiamini kupita kiasi na hatimaye kusahau wajibu wenu kama nyumba kubwa.....Nimekusikia Kaunga 🙂🙂

 
Last edited by a moderator:

Ndugu yangu Dark City, nakubaliana na wewe ila kuna kitu napenda nikukumbushe. Hivi unajua umoja ni nguvu? kama ndiyo inamaana once women decide to be together definately huyu mwanamume hata pata nafasi ya kuingilia kati.

labda niseme to me sitak hata kuju huyu mume wangu anacheat wapi na nani, na mimi siyo kwamba sitongozwi la, tena muda mwingine na watu ambao wanauwezo na ambao they can take me anywhere, but mimi msimamo wangu unabaki kuwa kwanini nimuumize mwanamke mwenzangu?

je mwanaume huyu nitatembea naye mara ngapi, ili nipate nini na kwa wakati gani? You know ukikaa na kufikiri utagundua kuwa hata kama huna hela au kazi au chochote kile kutembea na mume wa mtu hakutamaliza kiu ya tatizo lako hata kidogo na siku ukiwa na shida ambayo hataweza kukutimizia basi utatafuta mwingine awezaye kufanya hivyo. Hapo hivyo utajiuliza tena nitatembea na wanaume wangapi, kwa muda gani, ili nipate nini?

Pia kuna kitu ambacho mimi huwa nakisema sana, yakwamba, simuonei huruma mtu anayecheat kwasababu ta tabia kama wafanyavyo wanaume walio wengi. Hawa kwao ni tabia na kama tujuavyo tabia haina dawa. On the other hand namwonea huruma sana yule afanyaye uzinzi kwasababu ya vitu anavyovikosa kama wafanyavyo wanawake walio wengi. Hawa kwao wakipatiwa wanavyovikosa basi hawata fanya hayo.

nihitimishe kwa kusema ni kitu kibaya sana kwa mwanaume au mwanamke kupanda kitanda cha mwenzio. Huu ni unyanyasaji ambao dhmbi yake lazima itakumaliza tu. Nawatia moyo akina mama wanaopitia katika hali hii jamaani msiumie zaid, hata Mungu anakubali kutalikiana iwapo mmoja atakamatwa kwenye uzinzi. So usiangalie mazingira decide from there kisha uone lazima utatoka tu. Ila siwez kukutia moyo eti uvumilie hata siku moja usiumize moyo wako kwaajilia ya jitu lisiloona thamani yako.
 
Last edited by a moderator:
Duuuuhhhhh,

Kaka hapa naona umeamua kuhamisha magoli......Cheating haivumiliki ndiyo, ila wewe huoni tofauti kati ya kwenda kujificha kichakani (enzi zetu) na kufanyia lounge (bed room)???

Babu DC!!

.....kaka, mwizi ni mwizi tu! ....ukiniuliza wa afadhali nitakwambia kwangu mie aheri huyo aliyefanya hadharani na kunisaidia maamuzi,
Kuliko yule anilambaye kisogo.

I have lived the experience bro, am talking thru facts not myths. Ni aheri nijijue naishi kwenye hizi "Open Marriages" kuliko kusaidiwa vichochoroni...
 

Kamanda, tupo pamoja.

Halafu kama twataka hukumu kiukweli kesi hii, tu assume upande wa mwanaume nae alifikiaje uamuzi huo.

Huenda (mwanaume) nae alijionea enough is enough, potelea mbali....psychological abused na the so-called mama mwenye nyumba yake ambaye mwanajamiiOne amejipa nafasi ya kumtimua mume kwa maneno ya "chukua virago vyako kwenda!"

Assume, huyo mume kwakuwa anaishi kwa mkewe, huyo mwanajamiiOne anamkosea adabu, heshima, utii na haki zake. Assume, mke anarudi time anayotaka, mlevi, mzinzi, mwenye madharau nk....

What pushed that man to that 'extent?'
 

Ndugu yangu hakuna sababu yoyote ya msingi inayowapush kuamua kufikia hapo,
basi tu wame za watu (wengi wao) siku iz kama wamewehuka, macho juu juu kama wanachambua mchele wako na matamanio yasiyozuilika sijui aisee wanashindwa kujizuia kwa lolote nadhan wana mapepo kwa sababu hali zao ni tete, hawaheshimu ndoa zao, si wake zao wala familia zao.
 
Wengine akija kwako anakuja tu just kama sehemu nyingine yeyote ambayo angeenda.
Mtaani anaanza vijembe kitanda chenyewe kile mmh sijui mchina..anaringia sijui nini tumeshakilalia mpaka tumechoka
chumba chenyewe mmh...
..MJ1 hivi unadhani wanajali ni kwa sababu yeye hana uchungu na wewe hivo anafanya lolote
1. Anakuja pale akijua tayari kuna mwenyewe
2. Kama alivyosema Kongosho kuliko kwenda Guest leo ngoja niende pale pale anapolala mwenzangu
.Hadija Kopa aliimba.
Duniani kuna vioja sana.
 
Last edited by a moderator:

Soulmate bana hebu nisome tena hapo kwa uzuri. Hiyo ya fungasha mabegi ni tafsiri niipatayo mie toka kwa mwanaume afanyaye hayo. Kuwa akifikia hatua ya kumleta mwanamke mwingine kwenye matrimanial bed yetu atakuwa ananifikishia ujumbe wa ............Mama Chanja, sikuhitaji tena hebu fungasha vyako usepe.

Eti akili si zake, zaziazima?
 
Duuuuhhhhh,

Kaka hapa naona umeamua kuhamisha magoli......Cheating haivumiliki ndiyo, ila wewe huoni tofauti kati ya kwenda kujificha kichakani (enzi zetu) na kufanyia lounge (bed room)???

Babu DC!!

Babu DC, hapo kwenye red hapo ndipo panaponshangaza mie. Sawa Soulmate kasema kuwa saa nyingine akili huwa si zao basi hizo akili za kuazima huwa zina nguvu sana, maana zawezakumsaidia mtu kuendesha hata gari akatoka huko alikotoka na huyo mpenziwe wa siri hadi akampandisha kitandani mwenu!
 
Haya mambo ni complicated sana. Ni vigumu sana ku-generalize...kila uhusiano upo tofauti! Na pia ni vema tuka appreciate kuwa mwanaume na mwanamke wanalitizama 'tendo la ndoa' kitofauti sana na hata jamii kwa ujumla suala la mwanaume kuwa na multiple partners linatazamwa kitofauti ukilinganisha na mwanamke kuwa na multiple partners.

Na kwa kadri siku zinavyokwenda, uhusiano kati ya kupenda/kupendwa na tendo la ndoa unakuwa mdogo sana. Tendo la ndoa linajifungamanisha zaidi na suala la uchumi kuliko mapenzi. Ngono nyingi zinafanyika sio kwa sababu wahusika wanapendana bali ni biashara (mmoja anauza, mwingine ananunua) tu. Na sadly, katika hili zizungumzii machangu doa bali hata ndoa nyingi ukitizama deep down unaona zimejengwa katika msingi huu wa kiuchumi na sio mapenzi kwanza. Kwa hiyo kitendo cha mwanaume kushiriki tendo na mwanamke mwingine, si mara nyingi mke atakitafsiri kuwa hapendwi au huyo mwanamke mwingine anapendwa zaidi. Kwa wanaokumbuka manaweza kurejea ile kesi ya Clinton na Monica na comments ambazo Mama Clinton alizitoa kuhusu kadhia hiyo!
 

Aksante gfsonwin,
 
Anaefanya uzinzi ni mjinga,lakini anaelipa ujinga kwa ujinga ni mjinga zaidi!
kwani Eiyer COLD WAR NI UJINGA!??? hebu nifafanulie hapo ujinga unakujaje, kama nimeamua kuwa SILENT! lengo ni ujiulize mwenyewe, ujikalishe kikao mwenyewe, ujijibu mwenyewe, na kutafuta solution mwenyewe, Sababu kubwa ni kwamba, wakati unaanza ulianza mwenyewe na huyo nyumba ndogo yako, sasa iweje leo nimejua TUSHIRIKISHANE??? ulianza mwenyewe, basi MALIZA MWENYEWE! mimi ni MKEO na nitabaki MKEO MILELE!
 

SMU aksante nakubaliana na wewe kwa asilimia zote zilizomo lakini ndo amlete nyumbani, kitandani kwa mkewe/mumewe?

Kuna rafiki yangu ameniuliza kuwa tunaichukuliaje pia kima mama wanaotembea na vijana wao wa kazi, shambaboy au gardener katika vitanda vyao vya ndoa. Nadhani the feelings, blames are the same!

Tumeambiwa ndoa na ziheshimiwe siku zote, lakini kwa kuwa hali halisi inaonyesha kuwa hii imekuwa ngumu, basi hata vitanda vya ndoa tunaviabuse?

gfsonwin amesema cheat but nisijue wacheat!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…