Ndugu yangu
Dark City, nakubaliana na wewe ila kuna kitu napenda nikukumbushe. Hivi unajua umoja ni nguvu? kama ndiyo inamaana once women decide to be together definately huyu mwanamume hata pata nafasi ya kuingilia kati.
labda niseme to me sitak hata kuju huyu mume wangu anacheat wapi na nani, na mimi siyo kwamba sitongozwi la, tena muda mwingine na watu ambao wanauwezo na ambao they can take me anywhere, but mimi msimamo wangu unabaki kuwa kwanini nimuumize mwanamke mwenzangu?
je mwanaume huyu nitatembea naye mara ngapi, ili nipate nini na kwa wakati gani? You know ukikaa na kufikiri utagundua kuwa hata kama huna hela au kazi au chochote kile kutembea na mume wa mtu hakutamaliza kiu ya tatizo lako hata kidogo na siku ukiwa na shida ambayo hataweza kukutimizia basi utatafuta mwingine awezaye kufanya hivyo. Hapo hivyo utajiuliza tena nitatembea na wanaume wangapi, kwa muda gani, ili nipate nini?
Pia kuna kitu ambacho mimi huwa nakisema sana, yakwamba, simuonei huruma mtu anayecheat kwasababu ta tabia kama wafanyavyo wanaume walio wengi. Hawa kwao ni tabia na kama tujuavyo tabia haina dawa. On the other hand namwonea huruma sana yule afanyaye uzinzi kwasababu ya vitu anavyovikosa kama wafanyavyo wanawake walio wengi. Hawa kwao wakipatiwa wanavyovikosa basi hawata fanya hayo.
nihitimishe kwa kusema ni kitu kibaya sana kwa mwanaume au mwanamke kupanda kitanda cha mwenzio. Huu ni unyanyasaji ambao dhmbi yake lazima itakumaliza tu. Nawatia moyo akina mama wanaopitia katika hali hii jamaani msiumie zaid, hata Mungu anakubali kutalikiana iwapo mmoja atakamatwa kwenye uzinzi. So usiangalie mazingira decide from there kisha uone lazima utatoka tu. Ila siwez kukutia moyo eti uvumilie hata siku moja usiumize moyo wako kwaajilia ya jitu lisiloona thamani yako.