Kwa maneno haya au maandiko haya Da Mkubwa ni kuwa tunarudi kule kule kuwa kwa kuwa tumelelewa, na kuaminishwa kuwa it is impossible kwa Mwanaume kuwa Saint, so kucheat ni hulka ya mwanaume? Je tuikubali hali hiyo?? Kama tunafikia hatua ya kupenda with reservation basi ni wazi kama alivyosema Soulmate wangu kuwa tunajikubalisha baadhi ya matendo mabovu ya waume zetu!
Na je ni kweli hatuweziibadilisha hii? Maana inawezekana kuamini kwetu na kujikubalisha kwetu kuwa mwanaume haweziishi bila kucheat ni sie tunawapa wenyewe screw drivers!!
Ifike sehemu tuseme NO, ukicheat (kama mie sicheat) sitokuadhibu kwa kucheat kama wewe wala kukaa kimya na kunyenyekea bali ni kukutema kimoja!!( Hapa mtaniuliza nitatema wangapi, as long as I feel kuwa hakulithamini penzi langu)
Mimi nilicheatiwa, nikaonyeshwa tena kwa kashfa za wazi zile za ..wakiitwa wanawake nawe utatoka? ? (hapa nkajiuliza kama si mwanamke ilikuwaje ukanioa!!) ...mwanamke usiejua kuzungusha kiuno (as if aliponioa ilikuwa najua kukizungusha!!) nikachukua darasa maalumu la kiuno, mtoto wa kike wapi!
Ilinichukua muda kuitambua thamani yangu na kuujua wajibu wa mwenzangu kunithamini, nikafunguka, nikajitambua, ajabu sasa ananiona wa thamani na am sorry kibao!! Kuna anayeambua thamani ya penzi langu, kama ni kuzungusha kiuno, atanisaidia kunifundisha, atanipa nafasi ya kujieleza wapi napenda wapi sipendi na kwa nini............................nafasi ambayo katu nisingeipata kama singesema no to the first!