GE2025 Khadija Mfaume achukua fomu kuwania ubunge viti maalum Mwanza

GE2025 Khadija Mfaume achukua fomu kuwania ubunge viti maalum Mwanza

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Khadija Mfaume Liganga, maarufu kama Dida, ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa anayewakilisha Mkoa wa Mwanza, amechukua fomu kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum vya Wanawake kupitia Mkoa wa Mwanza.

Dida ni mwanaharakati mashuhuri wa haki za wanawake nchini, anayefahamika kwa mchango wake mkubwa katika kuinua sauti na nafasi ya mwanamke kwenye jamii. Kupitia juhudi zake, ameweza kuandaa na kuratibu makongamano mbalimbali ya kuwawezesha wanawake, pamoja na kuwa muasisi na muandaaji wa Tuzo za Mwanamke Kinara – tuzo maarufu zinazotolewa kwa wanawake waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii ndani ya Kanda ya Ziwa.

Kupitia hatua hii ya kuchukua fomu, Dida ameonesha dhamira yake ya kuendeleza harakati za kuwatetea na kuwawezesha wanawake kwa kutumia nafasi ya uwakilishi bungeni, endapo atapata ridhaa ya chama chake
1751194006615.png
 
Maelezo mengi kuhusu yeye ni dalili za kumpigia kampeni
 
Back
Top Bottom