Dudus,
Mwalimu Nyerere hakupokelewa Dar es Salaam na mzee yeyote alipofika mwaka wa 1952.
Hii ni katika moja ya makosa yaliyomo katika historia ya TANU.
Nyerere mtu aliyekuwa najuananae kwa karibu sana alipofika Dar es Salaam ni Joseph Kasella Bantu.
Kasella Bantu akiishi Temeke.
Kasella Bantu ndiye aliyempeleka Nyerere kwa Abdul Sykes.
Abdul Sykes alikuwa ndiye Secretary na Act. President wa TAA.
Hicho chama cha TAA kimetokana na African Association chama ambacho baba yake Abdul, Kleist Sykes alikuwa katibu muasisi mwaka wa 1929.
Hakuna mzee yeyote aliyempokea Nyerere Dar es Salaam wala kumkabidhi TANU.
Wala Mwalimu hakupata kujulikana hadi pale alipokuja kusuhubiana na Abdul Sykes.
Katika historia ya TANU kutokea TAA wazee waliokuwa ndani ya uongozi wa TAA na wao kushiriki katika kuweka msingi wa kuunda TANU walikuwa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Said Chaurembo.
Hawa walikuwa wajumbe katika TAA Political Subcommittee.
Wala si sawa kusema kuwa Nyerere aliunda TANU.
Historia ya TANU inaanza mbali sana kwa karibu ni mwaka wa 1945 Abdul Sykes, Ally Sykes na askari wenzao katika 6th Batallion KAR Burma Infantry wakiwa Kalieni Camp Bombay hapo ndipo katika mkesha wa Christmas, 1945 walipoamua kuunda TANU kudai uhuru wa Tanganyika na jina hili lilitolewa huko.
Hapo Kalieni Camp askari Waafrika kutoka Afrika ya Mashariki walikuwa wanasubiri kurudishwa makwao baada ya WWII.
Urafiki wa Nyerere na wazee wa Dar es Salaam ulianza baada ya TANU kuundwa 1954 na mzee aliyekuwa karibu sana na Mwalimu alikuwa Mzee Mshume Kiyate mwaka wa 1955.
Ukipenda unaweza ukawaongeza na wengine kama Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Jumbe Tambaza, Mwinjuma Mwinyikambi na Max Mbwana.
Historia hii nimeiandika kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes (1998).
View attachment 2116833
Kulia ni Mzee Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Mzee Max Mbwana na Mzee Mwinjuma Mwinyikambi.