Khalid Abeid- Mchezaji wa Sunderland, Simba na Timu ya Taifa

Khalid Abeid- Mchezaji wa Sunderland, Simba na Timu ya Taifa

Dah! Tumeupoteza wapi mpira TZ? Mijitu kama Mwameja, Said Mwamba 'Kizota' Hamis Gaga 'Gagarino' wako wapi? Vijitu kama Morrison, Chama, Niyozima etc lazima wangesubiri benchi.
Chama ni daraja tofauti sana na kina Niyonzima na Morisson.

Ifikie wakati mmheshimu Clatous Chota Chama.
 
Mohamed, Msaidie kuandika kitabu cha kumbu kumbu yake ya soka.

Umenikumbusha mengi, kubwa ni vijana kutotambua timu za Ghana, Misri, Nigeria n.k zilikuwa katika usawa wetu.

Akina Mehal el Kubra, AccraHearts of oak, KCC, Abaluhya, Gormahia, Nkana, Enugu n.k. walikuwa wetu tu.

Tuikuwa na heshima kubwa katika soka. Timu zilikicheza nchi inazizima.

Pamoja na uliowataja, kuna waliotangulia mbele ya haki akina Omar Zimbwe, Maulid Dilunga, Gibson Sembuli, Shaaban Baraza n.k

Mohamed Chuma alichezea timu ya Taifa kwa miaka 10 mfululizo, akiwa mchezaji wa Bandari Mtwara
Akina Salhina na Nassoro Mashoto hawa ni Navy ya Zanzibar wakilitandaza gozi vema

Kama sitakuwa nimekosea, Khalid Abeid ndiye aliifunga Yanga 1973 goli moja lililohitimisha utawala wa Yanga katika medani ya soka. Kuanzia hapo ikawa kupokezana tu.
Mkuu mbona sasa hivi hizo timu ulizotaja zote ziko daraja la chini kuliko timu zetu mbili za kariakoo?
 
Shukraani mno hiki ndio kipindi ambacho nchi ilikua na heshima na adabu,tunawana JF humu wanaojifanya wajuaji sana na middle class wakati they achieved nothing kwenye maisha yao,ninazisoma mada zako humu mkuu ,Shukraani sana
Mkuu kwani huwezi kumsifu Mzee Mohamed Said bila kuwebeza wengine?

Anyway wewe umelifanyia nini taifa ?
 
SIKU MOJA NA KHALID ABEID MCHEZAJI WA SUNDERLAND, SIMBA NA TIMU YA TAIFA

Huwezi kuchoka kumsikiliza Khalid Abeid mchezaji wa Sunderland mwishoni mwa miaka ya 1960 na mwanzoni mwa 1970 baada ya Sunderland kuwa Simba.

Mimi na Khalid Abeid tuna ndoto ya muda mrefu ya kuandika kitabu chake katika maisha yake ya mpira kuanzia kwao Mwanza hadi anakuja Dar es Salaam kujiunga na Wekundu wa Msimbazi kisha kuondoka na kwenda kucheza mpira Arabuni katikati ya miaka ya 1970.

Maktaba ya Khalid Abeid imesheheni kumbukumbu ambazo kama una moyo hafifu utajifuta machozi kila dakika achilia yala maneno ya Khalid Abeid ambayo anaangalia mpira wa leo ulioko Tanzania na anafananisha na enzi zao

Khalid anasema, ''Washabiki wa leo wanashangaa wakimuona Morisson anapanda juu ya mpira.

Sunday Manara alikuwa akifanya sana hii tena yeye akipiga na saluti akiwa juu ya mpira na kafanya haya tukiwa katika timu ''combine,'' na tumeshashinda.''

Khalid Abeid ananikumbusha anasema, ''Yanga waliweka heshima Ghana kulikokuwa na timu za kutisha Afrika.

Yanga imekwenda sare na Asante Kotoko, kwao, Dar es Salaam na Addis Ababa

Ghana ilikuwa inaiheshimu Yanga.

Simba tumewafunga Hearts of Oak kwao timu kali kabisa Afrika katika wakati wao.''

Mimi na Khalid Abeid tumekaa tunasikitika kuwa hatuna Football Museum na sote tuna hofu kuwa historia ya mpira wa Tanzania itapotea.

Ukiangalia Maktaba ya Mpira ya Khalid unaweza kumwaga machozi.

Utamuona Shida Stua "full back," mstaarabu mwenye, "ball control," ya mchezaji wa mstari wa mbele.

Shida katangulia mbele ya haki.

Utamuona Abbas "Sungura" Dilunga "winger" mwenye kasi kubwa.

Abbas na yeye ametangulia.

Kuna picha ya Khalid na Nahodha wa Sunderland kaka yangu Yusuf Salum Maleta yeye na wenzake kama Arthur Mambeta walitokea Kahe Republic timu za mitaani zilikzokuwa na mpira wa viwango.

Nikiitazama picha hii Khalid mtoto mdogo nadhani haja fika hata miaka 20.

Khalid kanionyesha mkusanyiko wa picha za Timu ya Taifa akina Gulam, Nassor Mashoto, Salhina, Omar Zimbwe, Mohamed Chuma Omar Mahadhi.

Raha ya hizi picha ni pale ninapofananisha umri aliokuwanao Khalid na wachezaji wengine ambao walikuwa wamempita umri kwa mbali sana.

Khalid Abeid amenifungulia hazina yake ya picha ambazo zilitakiwa ziwe katika Museum ya Mpira kwa kuhifadhiwa kwa ajili ya kizazi kijacho.

Ukweli ni kuwa siku moja ni ndogo sana kwa yeyote yule kupitia Maktaba ya Mpira ya Khalid Abeid.

View attachment 1546315View attachment 1546316View attachment 1546317View attachment 1546318
Mzee mohamed! Karibu al khasusi!
 
Back
Top Bottom