Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 23,566
- 24,891
Haya ni maneno mazito ya Khalid Aucho, Mchezaji wa Yanga kwenda kwa mashabiki wa Soka Tanzania akiongea na Waandishi wa Habari baada ya kukabidhiwa Kombe la Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League. Aucho aliulizwa baadhi ya maswali ikiwemo ni nani anatamani kucheza naye na kumtaja kiungo wa kimataifa Zambia Clatous Chota Chama, lakini pia akaulizwa kuhusiana na mchezaji gani wa Kitanzania anayemkubali zaidi na kumtaja Feisal Salum (Fei Toto).
"Namkubali sana Fei Toto siyo kwasababu yuko Azam lakini ni mchezaji mzuri sana, nadhani Watanzania mnapaswa kujivunia kipaji hicho badala ya kumkosoa na kumzomea, mnapaswa kumpa moyo na kumpamba kuliko kuwapamba wachezaji kutoka nje. Kwa mfano Mdathiri Yahaya ni moja ya wachezaji bora sana hapa Tanzania lakini hamumpi heshima kama mnavyowapa heshima wachezaji wa kigeni." - Amesema Khalid Aucho