Khalifa: JAB wanatakiwa kukemewa na watu wote kwa ukandamizaji wanaofanya kwa waandishi

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Wakuu,

JAB mnaingia mpaka chumbani kwa watu mnataka nini? Hamuoni aibu kwa haya mnayofanya?

Afadhali kuna mwandishi yuko na ujasiri wa kuongea! Ni zaidi ya fezea kwa waandishi kukaa kimya kuwa na chombo kama JAB huku mnaona kipo kwaajili ya kuwakandamiza.

====

"Mambo vipi?

So, ukiwa mwandishi haimaanishi kwamba wewe siyo binadamu. Haimaanishi kwamba wewe siyo raia. Haimaanishi kwamba wewe siyo mtu. Imean, haimaanishi kwamba haki zinazoainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wewe hazikuhusu—kwamba zinawahusu watu wengine tu, wewe hazikuhusu. Unaona?

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu tumeona serikali kupitia Bodi ya Ithibati ikiwaonya na kuwakaripia waandishi wa habari kwa kutoa maoni yao kwenye mambo ya nchi yanavyokwenda. Tumeona ikitokea kwa Zungu ambaye alizungumza kuhusu ATCL akaitwa, akaonywa, akakaripiwa. Tumeona ikitokea kwa Fatma Karume na wengineo ambao walitoa maoni yao.

Sasa, ni muhimu sana kufahamu kwamba ukiwa mwandishi si kwamba huruhusiwi kutoa maoni. Na maoni haya unaweza ukayatoa kwenye mitandao ya kijamii, kwenye kurasa za magazeti, kwenye redio, kwenye TV.

Bodi ya Ithibati imepewa mamlaka ya kusimamia maadili ya uandishi wa habari. Maoni si uandishi wa habari. Wao wanatakiwa wasimamie maadili ya uandishi wa habari. Haya mambo ya kuwapa watu onyo, kuwakaripia, ni mwendelezo wa vitisho dhidi ya watu wanaotoa maoni yanayopingana na ya wale walioko madarakani.

Hiki si kitu kizuri, ni kinyume na sheria, ni kinyume na Katiba. Si kitu ambacho kinapaswa kufurahiwa; ni kwenda nje ya mamlaka ambayo Bodi ya Ithibati imepatiwa, na ni kitu ambacho kinapaswa kukemewa na watu wote."

Wakati nyie mnawakemea sisi huku tunawalaani nyie kwa uchawa wenu uliokithiri bila aibu, pambaneni wenyewe.
 
JAB ni upuuzi fulani uliokuja kudumaza fani ya uandishi na utangazaji wa habari. Ni chombo cha kijinga, badala ya kukuza na kundeleza taaluma, chenyewe kinaua huku kikijifanya kinajenga na kuheshimisha
 
Wanapenda tupost vitu Kama hivi! Hovyo kabisa
IMG-20260304-WA0059.jpg
 
JAB ni upuuzi fulani uliokuja kudumaza fani ya uandishi na utangazaji wa habari. Ni chombo cha kijinga, badala ya kukuza na kundeleza taaluma, chenyewe kinaua huku kikijifanya kinajenga na kuheshimisha
Fani ya uanahabari nchini Tanzania imetawaliwa na uchawa, mwanahabari anayetegemea bahasha na usafiri kutoka kwa anayekwenda kuandika habari zake, hutumia kalamu yake kumsifu bwana yake kuliko ukweli wa habari husika.
 
Ndo uone ule mfuko sijui wa kuwakopesha nia na madhumuni yake ni nini kuwaziba midomo wasema yanayowapendeza masikioni mwao?
 
Back
Top Bottom