Khaligraph Jones awaacha wengi midomo wazi kwa hili!

Khaligraph Jones awaacha wengi midomo wazi kwa hili!

Rosh Hashannah

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
3,415
Reaction score
2,043
Weekend hii rapper wa hapa nchini Kenya maarufu kama Kalighraph Jones, amewaacha wengi wakiwa midomo wazi. Hii nibaada ya staa huyu wa ”Unajuwa ni Mazishi”, alipoletwa jukwaani akiwa ndani ya jeneza. Jones amekua kwenye midomo ya wengi hivi majuzi, baada ya kujiingiza kwenye cheche za matusi na muigizaji na mcheshi mwenye hadhi za A list hapa nchini Kenya maarufu kama Eric Omondi. Hii nibaada ya Eric kupeperusha video iliyoonyesha kumkejeli rapper huyu.

Sasa baada ya mchepuko huo, rapper huyu ameaamua kurudi kwenye headlines tena na hili jipya, ambapo jumamosi hii, kwenye ukumbi wa Uhuru Gardens jijini Nairobi, Jones alipandishwa jukwaani akiwa kwenye ”Casket” ama jeneza la rangi nyeupe. Mashabiki na wadau wamuziki walioshuhudia hili, walishangaa kuona jeneza likiiingia jukwaani kitu kilichowafanya wote kuwa kimya kwa mda huku wakiwa na shauku kujua ninikilichokuwa kikiendelea. Lakini mwisho wa siku, mioyo iliwatua tu pale jeneza lilipofunguliwa na mara rapper huyo kutoka kwenye jeneza hilo huku akiwa ameshikilia kipaza sauti mkononi na kuanza kuimba wimbo wa unajua ni mazishi.
 
Hata richmavoko aliwahi kupanda jukwaani akiwa kwenye trunk la mwanafunzi... Hakuna jipya
 
Ubunifu sio Fiesta tu hata kwa wenzetu
 
hatari huyu jamaa alipewa collabo la KABABAYE kafunika vibaya
Mashabiki tunatofautiana kama vitasa na kofuli za solex. Kwangu hakuna msanii wa east africa aliyewahi kuchana kwenye trap beats nikaipenda track.

Kali nilikuwa nampenda saana na kumfuatilia kabla hajaingia kwenye trap ameingia kaniacha nyuma au labda wakati unaniacha nyuma.
 
Imebidi nimtafute na kupakua mangoma yake yuko vizuri
 
Picha vipi swahiba..?haukufanikiwa kuipata,nimekomaa mpaka mwisho sijaiona.
 
Mwenye ile rap anamdisi erick kuwa anapenda mamama na amekonda. Aitupie
 
Back
Top Bottom