stakehigh
JF-Expert Member
- Aug 9, 2019
- 40,702
- 41,213
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha NRA, Khamis Faki, amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Serikali yake itaweka sheria itakayowataka vijana wa Kizanzibari kuoa wake zaidi ya mmoja.
Faki ameeleza kuwa kijana yeyote atakayekaidi agizo hilo na kubaki na mke mmoja pekee atakabiliwa na adhabu ya kifungo jela, akisisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha familia na kupunguza changamoto za kijamii.
Aidha, Mgombea huyo ameahidi kuwa Serikali yake itaanza kulipa mishahara kwa Wazanzibari wote bila kujali kama wana ajira rasmi au la, akibainisha kuwa lengo ni kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na matunda ya uchumi wa Taifa.
Khamis Faki alitoa kauli hizo wakati akijinadi kwa wananchi, akiwataka kumpa kura ili aweze kutekeleza sera hizo ambazo amesema zitawaletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi wananchi wa Zanzibar