Elections 2010 Khanga, Tshirt za CCM zakwama bandarini

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
4,974
Reaction score
785
CCM imeshindwa kukomboa makontena mengi yenye khanga, tshirt, vitambaa, kofia na mabango. Baada ya TRA kukataa katakata kuyatoa hadi yalipiwe kodi. Kila mkoa ulipangiwa kupewa makontena mawili ya futi 20, hali hiyo imefanya baadhi ya wilaya kukosa kabisa khanga na kofia, na mikoa mingi kupata kiasi kidogo sana kuliko mahitaji halisi.

Sasa hivi ccm wanahaha kutafuta pesa za kulipia TRA ili waondoe mizigo yao bandarini.
 
Hii itakuwa tetesi mbona mzigo upo uswazi siku nyingi na watu wanagawiwa kama kawa...
 
Mkuu zimeishatolewa acha uongo

CCM walitegemea yangepita bila kulipiwa kodi hivyo katika bageti yao kodi ya serikali haikuwepo, hata hivyo tuna wasiwasi bado kuwa makontena yaliyabaki huenda yakatolewa bila kulipiwa kodi, au kulipiwa kodi isiyolingana na gharama halisi ya mali iliyoagizwa.
 
Mkuu zimeishatolewa acha uongo
Mkuu
ina maana mliprint nje? naamini from CHINA
kama chama kinachoongoza serikali hakiamini tariffs na ubora wa viwanda vyake nchini hatuhitaji ushahidi mwingine wa kuinyima kura.
Tuna viwanda vya nguo kibao nchini ina maana ccm imeamua kusupport ajira za nchi walizoprint hizo rushwa zao?
 
marando alishindwa kukomboa mzigo kama huo toka afrika kusini those days
 
Hivi kwa nini hii tenda hawakuvipa viwanda vyetu vya nguo viwatengenezee hizo khanga, ama kweli awa jamaa si wazalendo!
 
Hivi kwa nini hii tenda hawakuvipa viwanda vyetu vya nguo viwatengenezee hizo khanga, ama kweli awa jamaa si wazalendo!

Viwanda vya hapa nchini wagumu sana kutoa 10% wewe unafikiri akina Makamba, Amos Makalla watakulaje?
Bora wawapelekee wa China huko sio wazito kutoa 10%
 
Ata viwanda vya ndani hawaviamini wanaenda nje mbaya zaidi wanatumia forex.
Alafu mnasema Tz masikini?
 
Hivi Tanzania hatuna viwanda vya kutengeneza kanga,T-shirt na kofi mpaka waka tengenezee nje...hawaoni kama wangeongeza ajira Tanzania kama wange fanya hivyo...ua wana kwepa garama...na huyu mkuu wa TRA hapendi kazi anakataza nguo za Mafisadi anahatarisha ajira yake au danganya toto....Kama akiendele hivyo big up kwake...
 
vipo lakini ni very expensive kutengeneza khanga na vitenge ukilinganisha na singapore, china, cambodia etc. the main reason ni kwamba sisi hatuna umeme ulio robust [pesa zote ndo hizo wanakula na ndugu zao], pia kodi za malighafi ziko juu na generally we like buying from outside hata kama ni malawi...


wewe unadhani ulaji wa kampeni menejaz unatoka wapi? si ndo vitu kama hivyo?
 
marando alishindwa kukomboa mzigo kama huo toka afrika kusini those days
huyu naye sisi tunaongelea leo wewe unatuletea mambo ya enzi za mawe, kweli huwa nakuangalia kama zezeta fulani hivi la CCM sorry to say that.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…