KHARUMWA POLICE POST kuna kesi za mchongo wanazobambikiwa watu

KHARUMWA POLICE POST kuna kesi za mchongo wanazobambikiwa watu

gwang taek

Member
Joined
May 5, 2014
Posts
76
Reaction score
123
Mkoa wa Geita wilaya ya nyan'gwale kata ya KHARUMWA kuna kituo cha polisi pale.

Watu wa Takukuru kama wanataka uwajibikaji mzuri kwa hiki chombo cha Dola ..

Basi waende pale kufuatilia kesi za mchongo wanazobambikiwa wasukuma wakazi wa nyan'gwale😭

Kile kituo wanathamini pesa na umaarufu wa mtu baaas🥺🥺 hasa wachimba madini (matajiri) na wachina.. inashangaza sana.

Unavamiwa na majambazi/wezi/vibaka/wahuni/wavamizi.
Unaamua kujipeleka huko KHARUMWA usaidiwe 🙄
Haki ya mungu utakachokutana nacho kama ikiwa mmoja wa hao wavamizi anatoa sasampa au ana umaarufu hiyo wilaya hesabu maumivu 🥺
UTAGEUZIWA KESI
UTAGEUZIWA KESI
UTAGEUZIWA KESI

Ndio UTAGEUZIWA KESI ndio michezo yao 😭
Unaenda umepasuliwa kichwa kinavuja damu,watakuandikia vizuri tu PF3
Lakini ukifunguwa kesi inakula kwako 😭
Utafunguliwa kesi na mtuhumiwa wako uliemfungulia kesi 🙄

Jalada lako linafichwa na wanajifanya hawalioni ili wakukatishe tamaa 🥺

Lakini mbali na madhaifu hayo yote pale kuna watu wema pia kama OCS mzanzibar na vijana wapya (makuruta🤷)
Hawa watu hasa huyo ocs makame wana sifa njema kila kaya kutokana na utendaji wao mzuri kazini.
Japo haibadilishi uozo uliopo kituo chao cha kazi.

TAKUKURU
#wizaraMamboYaNdani
 
Njaa kali hao Poli.CCM hao...
2012 -Nilishiriki Kampeni za Uchaguzi wa Marudio wa Mwenyekiti wa Kijiji Cha Kabiga,mpakani Mwa Mkoa wa Mwanza na Geita kupitia CHADEMA.
CCM Mwanza na Geita waliungana wakapiga Kambi pale na Land cruiser mpya kama 15,wanapomaliza Mikutano wanaenda kulala Gest hapo Kaharumwa na kula Bia sana.

Polisi wa Kharumwa Kituo hakikuwa na gari wakakerwa na matanuzi hayo ,wakaweka mgomo baridi wa kuwapa sapoti CCM.

Basi kwenye Magari yao walikuwa wanatembea na unga na Sukari wanagawa kwa Wanakijiji kama rushwa.
Enzi za RedBrage tuliiunda kikosi kazi cha Vijana wa hapo Kabiga ..maana sisi tulikuwa tunalala kwenye miji ya Wanakijiji tukila nao Viazi na kulalia ngozi.Tulikuwa tunapewa taarifa za wapi CCM walipo wanagawa Unga tunaenda wanatimuka wanaacha misosi tunabeba tunakuja kula na Wananzengo.
Wakipiga simu Polisi Kharumwa kwamba CHADEMA wanawafanyia fujo wanajibiwa Polisi hawana gari.

Tulitamba sana,tukiwa na Land Rover ya kizamani ambayo tulipewa na Mfanya Biashara mmoja pale Geita MjiniSasa Marehemu-R.I.P Kamanda).Tukiwa na Diwani Mahenge-Wa Kasamwa(Mjelajela) enzi hizo na Dada Neema Masumbuko-BAWACHA(amerudi CCM siku moja na Upendo Peneza) na mimi hapa
Tuliwapelekea moto CCM wakiwa na kila kitu tukidhibiti kila aina ya njama zao mbaya na tukashinda Uchaguzi huo kwa kura nyingi tu..Katikati ya Kampeni palitokea Msiba ,sisi tukawa sehemu ya Nzengo tukashiriki mazishi,mara ghafula CCM nao wakafika misibani na Jenezs Jipya na Cruiser zao..Nzengo ikakataa Jeneza lao wakaambiwa wakangojee Kharumwa wanakolala afe mtu ndiyo wawape hilo Jeneza.

CCM bila Polisi si lolote kabisa.
 
Nyerere aliwahi kusema adui wa tatu wa nchi hii ni ujinga, maradhi na umasikini ila ukweli ni kwamba adui watatu wa nchi hii ni polisi, green devils party na polisi tena.
Nikikumbuka niliibiwa simu bado polisi wakala pesa na simu sikupata na hela haijarudi🤔, lolote baya liwakute.
 
Back
Top Bottom