Mpenzi wangu Zinduna, wa kufa na kuzikana
Moyo wangu waukuna, penzi lako ni mwanana
Wambea wameshanuna, kuona twavyopendana
Nakuahidi Zinduna, zaidi ya funza hakuna
Penzi tamu ulonipa, sijawahi kulipata
Pete ya ndoa kukupa, ilo nitafanya fasta,
Sitochelewa nahapa, nisije kutoka kapa
Nakuahidi Zinduna, zaidi ya funza hakuna
Usisikize ya watu, eti funza ni mchafu
Wanasema ni kijitu, kilichokosa sarafu
usiwaeleze katu, kuwa kitandani tafu
Nakuahidi Zinduna, zaidi ya funza hakuna
wanaulizia ubichi keini!!! kwa raha zenu jamani! napita tu hapa!Mpenzi wangu Zinduna, wa kufa na kuzikana
Moyo wangu waukuna, penzi lako ni mwanana
Wambea wameshanuna, kuona twavyopendana
Nakuahidi Zinduna, zaidi ya funza hakuna
Penzi tamu ulonipa, sijawahi kulipata
Pete ya ndoa kukupa, ilo nitafanya fasta,
Sitochelewa nahapa, nisije kutoka kapa
Nakuahidi Zinduna, zaidi ya funza hakuna
Usisikize ya watu, eti funza ni mchafu
Wanasema ni kijitu, kilichokosa sarafu
usiwaeleze katu, kuwa kitandani tafu
Nakuahidi Zinduna, zaidi ya funza hakuna
Mpenzi we funzadume, yeyote asikwambie,
Unanipa ufahari, na raha usisikie,
Nasi twombeane kheri, mapenzi yetu yakue,
Waambie hao wote, kuwa wanipenda mie.
Waseme hata wachoke, wacha tupendane sie,
Kote kote wazunguke, watashindwa wajijue,
Na watake wasitake, siye tuyafurahie,
Waambie hao wote, umenichagua mie.
Hata washikwe na wivu, wenyewe ndo waumie,
Sie twala zetu mbivu, watwache tufurahie,
Wayapate maumivu, mioyoni waumie,
Waambie hao wote, kuwa wanipenda mie.
Watayasema mchana, ngoja giza liingie,
Watalala tena sana, na ndoto ziwasumbue,
Tutazidi kupendana, watakoma wakomae,
Waambie hao wote, umenichagua mie.