KIA i40 ya mwaka 2015

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Edit: Moderator naomba edit Hyundai sio KIA.

Katika kuzurura mitandaoni nikaonana na Hyundai i40 ya mwaka 2015.

Hyundai nimeziona ona Tanzania so sikua na wasiwasi kuhusu mafundi na spare.




Nadhani kwa wapenzi wa sedans watavutiwa nayo.

Ila bei yake sio mbaya sana kwa Beforwad:



Just Milion 8 hivi CIF unaipata Dar es Salaam.

Tatizo likaja TRA. Dah.




Milioni 24.7 duh. Sasa mbona tunatishana.

Ushuru mara 3 ya bei ya gari.
 
Hawa nyama hawa wanatufanya tukose vitu vizuri kwa nongwa zao..

Hii ni kama mahali ya kumuoa mke uambiwe laki 3 halafu mkaja wa bibi sijui uwe milioni na ushehe
Na kuna tetesi walipunguza mwezi April ila sioni unafuu.
 
Na kuna tetesi walipunguza mwezi April ila sioni unafuu.
Hakuna walichopunguza chochote.

Mijitu iliyokaa pale tra na kule tcra ni mihayawani, mishamba haijui kwenda ma wakati. Ipo ipo tu, aheri misukule watakufanyia hata kazi za shamba kwa malipo ya unga.

Watu wengi wamekaa serikalini wapo wapo tu.. Eti mpaka miezi miwili iliyopita(sijui sasa hv) huduma ya PayPal hamna nchini, si upopoma huu, sasa si bora tukaishi pluto huko

Kuna kigari(nissan leaf) nilikichungulia tra calculator, hakuna option ya gesi ala umeme wao ni petrol ama diesel tu basi, sasa hii si ni dunia ya 1950 kweusi huko.
 
Hakuna walichopunguza chochote.

Mijitu iliyokaa pale tra na kule tcra ni mihayawani, mishamba haijui kwenda ma wakati. Ipo ipo tu, aheri misukule watakufanyia hata kazi za shamba kwa malipo ya unga...
Waende na wakati Kuna vitu mtu unajiuliza Hadi unakosa majibu.

Ifike mda TRA wajirekebishe huu ushuru wa magari siyo poa Wala nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kuna tetesi walipunguza mwezi April ila sioni unafuu.
Walipunguza CIF za baadhi ya magari.

Ambayo inapunguza kodi.

Mf. Kama CIF ya Prado iliwekwa $60,000 inashushwa mpaka $45,000 au $50,0000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…