Baraka Mina
JF-Expert Member
- Sep 3, 2020
- 586
- 590
Ni siku na wakati mwingine tena, poleni na majukumu ya kulijenga taifa hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waswahili walisema ni "Heri kujikwaa kidole kuliko kujikwaaa ulimi" Kuna viongozi wa kiserikali na viongozi wa CCM ambao wamepewa dhamana hawakukosea kutembea ila walitamka maneno ambayo yalisababisha mgogoro na kusahau kuwa ahadi namba tisa (09) ya mwanachama wa CCM inasema "Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika."
Leo ni siku ya pili (02) tangu 29/07/2021 Kamati Kuu Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kukutana na kufanya kikao chake pale Ikulu jijini Dar Es Salaam na ni siku ya nne (04) tangu 26/07/2021 Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu shaka kuutaarifu umma kuwa CCM inafuatilia kwa makini mienendo ya baadhi ya viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha umma na kwenda kinyume na maelekezo na maadili ya Chama. Moja ya maamuzi ya Kamati Kuu hiyo ni maelekezo ya kuanza kuchukuliwa hatua kwa wale wote wanaokiuka mienendo, taratibu na kanuni za madili na uongozi kwa mujibu wa katiba ya CCM.
Kufuatia maelekezo hayo inaonesha wazi kuwa kiama cha CCM ni halisi na kitaondoka na watu kwa kupewa adhabu kulingana na katiba ya CCM. Je ni kina nani kukutana na kiama hiki kama ilivyokuwa kwa kina Bernard Membe, January Makamba, Nape na wengine wengi? Hawa wanaweza kuingia katika orodha ya kuchukuliwa hatua.
Askofu Josephat Gwajima
Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima akiwa kanisani alidai kwamba chanjo ya korona iliyoletwa nchini ina madhara sambamba na kutoa kauli nyinginezo; kauli ambazo zilipingwa vikali na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg. Kenani Kihongosi kuwa hazikubaliki na hazivumiliki.
Gwajima alitoa kauli hizo siku moja baada ya Tanzania kupokea dozi zaidi ya milioni 1 za chanjo ya Korona kutoka Marekani kupitia mpango wa usambazaji chanjo ya Korona wa COVAX jumamosi ya Julai 24, 2021.
Dkt. Anthony Diallo
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dkt. Anthony Diallo akizungumza tarehe 09/06/2021 katika mahojiano ya kipindi cha The Big Agenda kinachorushwa na Star TV alisema kuna haja ya kuwa makini wakati wa kuchagua mtu atakayeiongoza nchi sambamba na kuukosoa utawala wa Serikali ya awamu ya tano akisema Tanzania ilipita kipindi cha giza (“Nadhani tumepata joto ya jiwe kipindi kilichopita. Sasa hivi tunaanza kuona raha, watu wana raha moyoni”). Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa CCM, Kanali Ngemela Lubinga alimjibu akisema CCM haijamtuma kufanya tathmini ya utawala uliopita. Pia Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg. Kenani Kihongosi alisema kauli iliyotolewa na kiongozi huyo ni msimamo wake mwenyewe na si wa CCM na kwamba jumuiya ya vijana inalaani kauli zinazotolewa na kiongozi huyo kuwabeza viongozi walioitumikia nchi, akitaka wastaafu hao kuachwa wapumzike.
Catherine Magige
Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige na baadhi ya Viongozi wa UWT Mkoa wa Arusha tarehe 27/05/2021 walifanya vurugu kwenye mazishi ya mfanyabiashara Kuzola Madoda. Vurugu hizo zilitokana na mvutano wa kugombea msiba wa mfanyabiashara Kudula Romanus Madoda kati ya mke wa ndoa Aziza Msuya na mbunge huyo. Ndg. Shaka Hamdu Shaka Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi alieleza kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechukizwa na kulaani kitendo kilichofanywa na kusema “CCM inaamini katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu, Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na Katiba ya CCM na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyokiuka katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM.”
Je ahadi namba tisa (09) ya mwanachama wa CCM ya kuwa mwaminifu kwa CCM, Tanzania na Afrika kuwahukumu wengi zaidi. Naendelea kusisitiza kuwa KIAMA CHA CCM NI HALISI KITAONDOKA NA WATU nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kazi Iendelee.