Kiama cha CCM ni halisi kitaondoka na watu

Kiama cha CCM ni halisi kitaondoka na watu

Posho anayolipwa Bungeni jumulisha usumbufu na vitisho vya kumvua uanachama vimemfanya Gwajima ajitoe fahamu ili afukuzwe CCM abakie na injili kanisani kwake kwani inamlipa zaidi kuliko akiwa Bungeni
Duuuuuuuuh, Mkuu umewahi kupitia mapato na matumizi ya ofisi ya Mbunge wa Kawe na kanisa la ufufuo na uzima na kuyajua hayo?
 
Ni siku na wakati mwingine tena, poleni na majukumu ya kulijenga taifa hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waswahili walisema ni "Heri kujikwaa kidole kuliko kujikwaaa ulimi" Kuna viongozi wa kiserikali na viongozi wa CCM ambao wamepewa dhamana hawakukosea kutembea ila walitamka maneno ambayo yalisababisha mgogoro na kusahau kuwa ahadi namba tisa (09) ya mwanachama wa CCM inasema "Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika."

Leo ni siku ya pili (02) tangu 29/07/2021 Kamati Kuu Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kukutana na kufanya kikao chake pale Ikulu jijini Dar Es Salaam na ni siku ya nne (04) tangu 26/07/2021 Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu shaka kuutaarifu umma kuwa CCM inafuatilia kwa makini mienendo ya baadhi ya viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha umma na kwenda kinyume na maelekezo na maadili ya Chama. Moja ya maamuzi ya Kamati Kuu hiyo ni maelekezo ya kuanza kuchukuliwa hatua kwa wale wote wanaokiuka mienendo, taratibu na kanuni za madili na uongozi kwa mujibu wa katiba ya CCM.

Kufuatia maelekezo hayo inaonesha wazi kuwa kiama cha CCM ni halisi na kitaondoka na watu kwa kupewa adhabu kulingana na katiba ya CCM. Je ni kina nani kukutana na kiama hiki kama ilivyokuwa kwa kina Bernard Membe, January Makamba, Nape na wengine wengi? Hawa wanaweza kuingia katika orodha ya kuchukuliwa hatua.

Askofu Josephat Gwajima
Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima akiwa kanisani alidai kwamba chanjo ya korona iliyoletwa nchini ina madhara sambamba na kutoa kauli nyinginezo; kauli ambazo zilipingwa vikali na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg. Kenani Kihongosi kuwa hazikubaliki na hazivumiliki.
Gwajima alitoa kauli hizo siku moja baada ya Tanzania kupokea dozi zaidi ya milioni 1 za chanjo ya Korona kutoka Marekani kupitia mpango wa usambazaji chanjo ya Korona wa COVAX jumamosi ya Julai 24, 2021.

Dkt. Anthony Diallo
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dkt. Anthony Diallo akizungumza tarehe 09/06/2021 katika mahojiano ya kipindi cha The Big Agenda kinachorushwa na Star TV alisema kuna haja ya kuwa makini wakati wa kuchagua mtu atakayeiongoza nchi sambamba na kuukosoa utawala wa Serikali ya awamu ya tano akisema Tanzania ilipita kipindi cha giza (“Nadhani tumepata joto ya jiwe kipindi kilichopita. Sasa hivi tunaanza kuona raha, watu wana raha moyoni”). Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa CCM, Kanali Ngemela Lubinga alimjibu akisema CCM haijamtuma kufanya tathmini ya utawala uliopita. Pia Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg. Kenani Kihongosi alisema kauli iliyotolewa na kiongozi huyo ni msimamo wake mwenyewe na si wa CCM na kwamba jumuiya ya vijana inalaani kauli zinazotolewa na kiongozi huyo kuwabeza viongozi walioitumikia nchi, akitaka wastaafu hao kuachwa wapumzike.

Catherine Magige
Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige na baadhi ya Viongozi wa UWT Mkoa wa Arusha tarehe 27/05/2021 walifanya vurugu kwenye mazishi ya mfanyabiashara Kuzola Madoda. Vurugu hizo zilitokana na mvutano wa kugombea msiba wa mfanyabiashara Kudula Romanus Madoda kati ya mke wa ndoa Aziza Msuya na mbunge huyo. Ndg. Shaka Hamdu Shaka Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi alieleza kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechukizwa na kulaani kitendo kilichofanywa na kusema “CCM inaamini katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu, Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na Katiba ya CCM na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyokiuka katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM.”

Je ahadi namba tisa (09) ya mwanachama wa CCM ya kuwa mwaminifu kwa CCM, Tanzania na Afrika kuwahukumu wengi zaidi. Naendelea kusisitiza kuwa KIAMA CHA CCM NI HALISI KITAONDOKA NA WATU nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kazi Iendelee.

View attachment 1875390

View attachment 1875391
JamiiForums1550718452.jpg
 
Ukitaka wananchi wakupigie kura kwa wingi fanya kazi njema na yeye kuonekana machoni pao ili baadaye usije kulia. Hauwatumikii wananchi unashinda kupiga propaganda halafu unategemea upate kura?
Mkuu muda ni rafiki mzuri sana, subiri uone.

Dhalimu alijifanya anafanya kazi, dakika ya mwisho ilibidi anajisi uchaguzi ili atangazwe mshindi. Kibaya zaidi alifanya uporaji wa kishamba mpaka kila mtu akajua.
 
Gwajima yupo tayari hata akose ubunge kwani anaona kanisa kila week linamlipa pesa nyingi lina faida kubwa kuliko kukaa Dodoma kusubiria posho za bunge
Ahadi namba 5 ya mwanachama wa CCM inasema "Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu."

Hivyo Gwajima anatakiwa kujua kuwa ahadi namba 5 inasisitiza kuwa uongozi ni utumishi kwa wananchi na sio manufaa kwa mtu binafsi hivyo hatakiwi kutumia vibaya au kumshawishi kiongozi mwingine aitumie vibaya dhamana hiyo.
 
Akina Dialo na wengine waweza kuwa hofu lakini Gwajima yeye kaamua kutengeneza mazingira afukuzwe ili awe huru afanye kazi zake binafsi kwenye makanisa yake
Aliomba uongozi kwa sababu gani?
 
Wanadai pia Chalamila aliomba kuacha kuwa RC Mbeya wakamkatalia wakamuamisha Mwanza kwa lazima ndi akaanza vituko maksudi ili afukuzwe
Mkuu aliyekuambia alikulisha matango pori 😂😂😂😂
 
Ukitaka wananchi wakupigie kura kwa wingi fanya kazi njema na yeye kuonekana machoni pao ili baadaye usije kulia. Hauwatumikii wananchi unashinda kupiga propaganda halafu unategemea upate kura?
Mkuu muda ni rafiki mzuri sana, subiri uone.
Kura gani? Kama unazungumzia hili kura wazoiba Ccm kwa kushirikiana na tume ua uchaguzi na polisi haziitaji hayo uliyoyasema
 
Dhalimu alijifanya anafanya kazi, dakika ya mwisho ilibidi anajisi uchaguzi ili atangazwe mshindi. Kibaya zaidi alifanya uporaji wa kishamba mpaka kila mtu akajua.
Kazi iliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi ilikuwa ni kubwa sana na wananchi waliikubali. Baadhi ni
  1. Usambazaji wa umeme vijijini uliongezeka kutoka 16.4% mwaka 2015 hadi 67.1% mwaka 2020.
  2. Elimu bila malipo; idadi ya wanafunzi wa sekondari iliongezeka kutoka wanafunzi 1,648,359 mwaka 2015 hadi 2,185037 mwaka 2019.
  3. Vituo vya kutolea huduma za afya (zahanati, vituo vya afya na hospitali) viliongezeka kutoka 7,014 mwaka 2015 hadi 8,446 mwaka 2020.
 
Kura gani? Kama unazungumzia hili kura wazoiba Ccm kwa kushirikiana na tume ua uchaguzi na polisi haziitaji hayo uliyoyasema
Lissu na Sugu walikiri wazi kuwa uchaguzi ulienda vema na upigaji kura ulikuwa unaendelea vizuri siku husika.
Tafadhali weka vituo ambayo kulitokea hayo madai unayosema.
 
Kazi iliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi ilikuwa ni kubwa sana na wananchi waliikubali. Baadhi ni
  1. Usambazaji wa umeme vijijini uliongezeka kutoka 16.4% mwaka 2015 hadi 67.1% mwaka 2020.
  2. Elimu bila malipo; idadi ya wanafunzi wa sekondari iliongezeka kutoka wanafunzi 1,648,359 mwaka 2015 hadi 2,185037 mwaka 2019.
  3. Vituo vya kutolea huduma za afya (zahanati, vituo vya afya na hospitali) viliongezeka kutoka 7,014 mwaka 2015 hadi 8,446 mwaka 2020.

Kama hivyo ulivyotaja vinatoa kura, basi makaburu wa Afrika kusini wangekuwa madarakani mpaka leo maana walifanya mara elfu ya hayo ya ccm.
 
Lissu na Sugu walikiri wazi kuwa uchaguzi ulienda vema na upigaji kura ulikuwa unaendelea vizuri siku husika.
Tafadhali weka vituo ambayo kulitokea hayo madai unayosema.

Ule ushenzi, ukatili na uhayawani wa wazi tuliuona kwa macho yetu na wala hatuhadithiwi. Ingia kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi kama matokeo ya ule uchafu wamethubutu kuyaweka.
 
Kama hivyo ulivyotaja vinatoa kura, basi makaburu wa Afrika kusini wangekuwa madarakani mpaka leo maana walifanya mara elfu ya hayo ya ccm.
Mkuu tofautisha CCM na makaburu. CCM ni Chama kiongozi na mfano kwa vyama vyote vya Afrika; historia yake ya kuhakisha uhuru wa Afrika Kusini na nchi nyingine inafahamika.
 
Ule ushenzi, ukatili na uhayawani wa wazi tuliuona kwa macho yetu na wala hatuhadithiwi. Ingia kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi kama matokeo ya ule uchafu wamethubutu kuyaweka.
Tume ilitangaza na wananchi ndiyo tuliochagua.
 
Majambazi yakifarakana ni furaha kwetu, na katika mfarakano huo sisi tunajiandaa kuwapelekea moto mpaka tuwamalize wote
 
Back
Top Bottom