Kiama cha mafisadi chafikia ukingoni

Ochu

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2008
Posts
976
Reaction score
47
Kiama cha mafisadi chafikia ukingoni

2008-10-20 11:29:33
Na Simon Mhina

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah, ametangaza kiama cha vigogo wanaotuhumiwa kwa rushwa kwa kusisitiza kuwa taasisi hiyo itawashukia na kuwaburuza kortini kwa kasi inayozidi ya mwewe.

Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum baada ya kufunga warsha ya siku mbili iliyohusu rushwa katika chaguzi, Mkurugenzi huyo, alisema siku ya kuwaburuza vigogo hao mahakamani, imekaribia.

Alisema kama ambavyo kiama hakifahamiki kitakuja lini na kitamkuta binadamu akiwa wapi, ndivyo taasisi hiyo itakavyowadokoa mmoja baada ya mwingine, kisha kuwaburuza mahakamani.

``Kama ambavyo watu watashtukia tu baragumu au parapanda limelia na kiama kimewadia, ndivyo ambavyo vigogo hao watashtuka kujiona wapo kizimbani muda mfupi kuanzia sasa,`` alisema na kuongeza kuwa:

``Najua mna wasiwasi, lakini napenda kuwahakikishia Watanzania kupitia kwenu (vyombo vya habari) kuwa, hatuna masihara kwa jambo hili, hatuwezi kusema tutawafikisha watu mahakamani halafu tusiwafikishe...mambo yameshaiva, kesi zipo tayari watajikuta tu wapo kizimbani.``

Alipoulizwa kama kesi hizo zitafunguliwa mwezi huu au ujao, alisema kilichofanya mambo `yasilipuke` ni maandalizi ya kongamano hilo, lililoandaliwa na ofisi yake pamoja ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Alipohojiwa ni kwanini watuhumiwa hao washukiwe ghafla, Hosea alisema inatokana na ukweli kwamba, sheria inamzuia kuzungumzia kesi ambayo hajaifikisha mahakamani.

Hivi karibuni, Dk. Hoseah alinukuliwa akisema kwamba kuna kesi tano zinazohusu mafisadi na muda wowote wangeweza kufikishwa kortini.

Hata hivyo, zaidi ya siku 20 zimekwishapita bila taasisi anayoiongoza kufanya hivyo.

``Siwezi kutaja hapa kwamba mtu fulani amefanya hivi au vile, nitakuwa nakiuka sheria iliyounda Takukuru, hawa watafikishwa mahakamani tu, hatuwezi kutania,``alisema.

Naye Mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Maswa, John Shibuda, alisema taasisi hiyo hivi sasa inaonekana kama chafya cha mtoto mchanga, ambayo haiwezi kumuamsha baba mlevi usingizini.

Ili kuondokana na dhana hiyo, ameitaka Takukuru kuchukua hatua kali dhidi ya wala rushwa wote kwani kufanya hivyo itajisafisha kwa Watanzania.

Alisema hakubaliani na watu ambao kila mara wanaishutumu taasisi hiyo na Mkurugenzi wake, kwa vile imezingirwa na sheria mbovu.

``Takukuru inabanwa sana, wakisema wanaonekana kama chafya ya mtoto mdogo ambaye hata akipiga chafya mara tano chafya hiyo haiwezi kumuamsha usingizini baba mlevi aliyelala kitandani,``alisema na kuongeza kuwa:

``Tunaimba wimbo wa rushwa kila siku, lakini lazima tujiulize nani katufikisha hapa. Rushwa imeota mizizi kwa vile kuna viongozi wanaifuga na kuitunza kuliko familia zao.``

Naye Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, alisema kwa sasa haihitajiki utafiti, maazimio au ngonjera yoyote kuhusu rushwa, bali kinachotakiwa ni vitendo.

``Ukisoma tafiti, sheria na mipango ya kupamba na na rushwa ni kubwa kuliko msahafu, hatuhitaji maneno maneno sasa tunataka vitendo. Tunahitaji watu wanaowachukulia hatua wala rushwa,``alisema.

Warioba, alisema kuna malalamiko ya kweli ambayo yamejitokeza kwamba wakubwa wakila rushwa, wanaundiwa tume kuchunguzwa, lakini wadogo wanapelekwa moja kwa moja polisi.

Alisema Takukuru ina nafasi ya kujisafisha juu ya tuhuma hizo kwa kuwaburuza Mahakamani wala rushwa wote bila kujali nyadhifa na uwezo wao.


* SOURCE: Nipashe
 
Wewe Hosea hebu acha mzana wakijinga.. hakuna mtu alie kwenye utani hasa nyakati hizi... umkamate nani wakati wewe binafsi ni mchafu unaenuka.... give me a break...!!!!!
 
Christmas nyingine inakaribia, Mheshimiwa atawapa tene muda wa kusheherekea sikukuu.
 
Kaka Hosea inamaana vijisenti vyote vimeisharudi? au mnataka kujinufaisha na maneno yenu? hebu acha mzana wakijinga.. hakuna mtu alie kwenye utani hasa nyakati hizi.Utamkamata nani wakati watu bado mko kwenye mpini,achieni ili mkamatane vizuri !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!...!!!!!
 
hizo porojo za Hosea tumezizoe wakuu. Na akadanganye wajinga kwa nyimbo zake hizi
 

Issue ya mafisadi imejulikana lini?, kwanini hawajakamatwa mpaka sasa?, kwanini wakamatwe sasa?, ili iweje?.

Sikiliza Hosea, wewe na mafisadi wenzako mnacheza na moto, lakini iko siku ambayo si mbali toka sasa huo moto utawauunguza nyinyi na famila zenu.

Mmeigeuza Tanzania ni ya kwenu (kundi la walaji wachache) na mnafanya vile mnavyotaka. Siku ya siku mtakuja kujua kwamba nyinyi mlipewa dhamana na wananchi na mnalipwa mishahara.

Hosea, Tafadhali acha kuongea upumbavu na pia acha kutukana watanzania, bila kujua unatukana na wazazi wako.

Kauli zako (utumbo uliongea) umenikasirisha mno.
 
Hivi kwanini wasifunguliwe mashitaka kwa kusema uongo?
Tena uongo wa kurudia rudia huo ni wa kunuia...Wafunguliwe mashataka ya kuwaongopea wananchi na kusababisha upotevu wa amani.
 
Hivi kwanini wasifunguliwe mashitaka kwa kusema uongo?Tena uongo wa kurudia rudia huo ni wa kunuia...Wafunguliwe mashataka ya kuwaongopea wananchi na kusababisha upotevu wa amani.

Mai wasu weeee jimbafu jani.Hahahahhahahahahahaha.Yaani nimeamini waTZ wamechoka sasa
 
Mbona watu hamuelewi Kiswahili?Kiama kufikia ukingoni maana yake ni mwisho wa kiama!Yaani hakuna kiama/tamati tena!Kwa lugha nyingine, hakuna tena kiama hapo - kimeisha!
 
Mi naona Hosea ametugeuza wa TZ wote kuwa wake zake, kama anaweza akatoa maneno ya uongo kila kukicha. Ningemshauri anyamaze tu maana maneno yake ya kila siku yasiyokuwa na vitendo ni ubatili mtupu na matusi kwa watanzania waliochoka na maisha kiasi cha kutaka kumalizia hasira zao kwa JK!!!
 
Mai wasu weeee jimbafu jani.Hahahahhahahahahahaha.Yaani nimeamini waTZ wamechoka sasa

Ni kweli tumechoka na wala siyo siri tena...Tumechoka na madhalimu na uongo unaosababisha vifo na hasara na utumwa...Kweli tumechoshwa...Lakini wapumbavu...Hapo sidhani....Upumbavu uliobaki utaendelea kumalizwa kwani ufisadi hata kipofu anauchukia.
 

Consider Gender.
Not necessarily kuwa wakeze hata wanae pia ingesound vyema.

Ila huu ni mzaha. Kama kuna mtu anaekumbuka maandishi kwenye bango La Takukuru dodoma kwenye offisi yao nafikiri yanaelezea vizuri uongo huu. Mdau anaeweza kupata picha atupe lina verry funny Message.

Nachokumbuka kuna maandishi kama haya

Haki Haina Bei
RUSHWA NI ADUI WA HAKI
USITOE WALA KUPOKEA RUSHWA
.

Kwangu i see like this billboard says

Ukipewa rushwa don't Burgain Just Take whatever is Available.

May be Hosea Is now Out for This.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…