Kiambu County yapiga marufuku ukusanyaji wa chupa tupu za pombe

Kiambu County yapiga marufuku ukusanyaji wa chupa tupu za pombe

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314

Kaunti ya Kiambu imechukua hatua isiyo ya kawaida katika vita dhidi ya pombe haramu. Kamishna wa Kaunti hiyo George Matundura ameagiza watu wasio na leseni kuacha kukusanya chupa tupu za wine na spirits.

Agizo hilo limetolewa baada ya maafisa wa usalama kuvamia kiwanda kinachodaiwa kuwa cha kutengeneza pombe haramu Muguga, Kabete, ambapo mtu mmoja alikamatwa.

Lakini ni sababu kubwa ni nini?

Mamlaka zinasema baadhi ya chupa hizo zinauzwa kwa watengeneza pombe haramu, ambao huzitumia kupakia upya pombe zinazodaiwa kuwa haramu au bandia, na hivyo bidhaa hizo kuonekana kama pombe halali.

Vita dhidi ya pombe haramu si suala la kuvamia baa pekee. Mamlaka sasa zinaangalia pia mnyororo unaowezesha bidhaa hizo kuingia sokoni; yaani kutoka kwenye uzalishaji hadi ufungashaji na usambazaji. Kiambu tayari imeripoti operesheni kadhaa za kukamata pombe inayodaiwa kuwa haramu, huku Bunge la Kaunti hiyo likiendelea kuandaa marekebisho ya sheria za kudhibiti pombe.

Je, unadhani udhibiti wa chupa pekee utatosha bila kuziba mianya mingine katika uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa pombe bandia?
 
Back
Top Bottom