Usiri wa taarifa za mgonjwa atoapo akiwa maeneo ya kutolea huduma za afya
Leo napanda jukwaani na andiko langu kuhusu kero inayotupata wagonjwa hasa tunapotoa maelezo kuhusu maradhi yanayotusumbua pindi tuendapo hospitalini
Kikawaida taarifa atoazo mgonjwa inabidi ziwe za siri baina yake na mtoa huduma kama ni dakitari ama ni nesi lakini ukienda katika vituo vya kutoa huduma hali ni tofauti ambapo unakuta mgonjwa anachukuliwa taarifa zake sehemu ya uwazi nikimaanisha hata asie husika anaweza kuzisikia na kumwondolea mgonjwa uhuru wa kutoa taarifa zote muhimu zinazo husiana na ugonjwa wake
Kipengele hiki kinaenda sambamba na kiapo waapacho watoa huduma ya afya pale wanapoanza masomo yao na pale wanapohitimu wao wenyewe wanaita Hippocratic oath kuhusu kuficha taarifa za mgonjwa(confidential)
Nimeandika andiko hili pengine serikali kupitia wizara ya afya inaweza ikaliona na kuchukua hatua ya kujenga vyumba maalumu katika hospitali hasa zinazolaza wagonjwa kwa sababu hii ni haki ya msingi ya mgonjwa kuhakikishiwa kuwa taarifa zake zinabaki kujulikana kati yake yeye na mtoa huduma.
Uhuru wa mgonjwa katika kuyakatisha Maisha yake hasa kwa wale wanaougua magonjwa sugu kama kansa n.k(euthanasia)
Sayansi na teknolojia inazidi kukua na kila sekta inafaidika na kuathirika kwa namna yake na inapokuja katia sekta ya afya kuna hiku kitu kinaitwa euthanasia yaani uhuru wa mgonjwa kuyakatisha Maisha yake pale aonapo tumaini la kupona ugonjwa wake ni dogo mno.
Katika baaadhi ya nchi zilizoendelea wameipitisa hii sheria na ikizingatiwa pia katika kiapo waapacho watoa huduma kuna kipengele kinazingatia uhuru wa mgonjwa wanaita patient autonomy lakini kwa sheria za Tanzania sheria hii bado haijawekwa wakfu.
Nimeipandishaa hii jukwaani kuilenga hasa wizara ya afya kuleta mwafaka kwa sababu kwa wagonjwa waliowengi maamuzi mengi yanakuwa chini ya ndugu zao hivyo mgonjwa ananyimwa haki yake ya Msingi ijapokuwa hata kama ikiruhusiwa itaenda kinyume na matakwa ya dini na tamaduni lakini vipi kwa mzee wa miaka miamoja, anasumbuliwa na kansa iliyoambatana na maumivu makali kwanini asipewe uhuru wa kuamua nini kifanyike?
Hivyo ni wakati sahihi kwa serikali kuweka wazi hatua zipi zichukuliwe endapo mgonjwa akiomba kufanyiwa hivyo lakini ikumbukwe kuwa daktari kushiriki kutoa uhai wa mgonjwa atakuwa anaenda kinyume na kiapo chake abacho kinasema asidhuru, asiue wala asiumize mgonjwa
Uhuru wa mgonjwa na daktari na kazi yake
Wakati wa kula kiapo madaktari wote wanatumia kiapo kinaitwa Hippocratic oath, na kiukweli wengi wanakiapa na wanakitumia hasa wawapo eneo la kazi. Lakini vipengele vyake ni chanagamoto kwa pande zote mbili mfano linapokuja swala la kutoa mimba. ikumbukwe kuwa kwa sheria za Tanzania mimba itatakiwa kutolewa pale tu hali ya mama itaonekana kuwa hatarini kwa sababu ya hiyo mimba.
Mfano, amekuja binti wa miaka kumi na saba analalamika amebakwa lakini ni baada ya mwezi sasa anapokuja kugundua hapati siku zake tena ndipo anapoamua kununua kipimo cha mimba na kujikuta ni mjamzito, anakuja kwa mtoa huduma na kuomba mimba ile itolewe (uhuru wa mgonjwa) na ikumbukwe kiapo hicho hicho kinasema daktari usidhuru je ikiwa wewe ndiwe mtoa huduma ungefanyaje?
Kwanini nimeandika hili, nahitaj kuwasilisha maoni yangu kwa wadau wa afya na elimu kuona namna ambavyo tunaweza kuboresha kiapo ambacho kitakuwa na maana ya moja kwa moja na kutoleta ukakasi kwa mtoa huduma na mgonjwa mwenyewe ikizingatiwa kiapo hiki kililetwa miaka mingi iliyopita na huenda kilikuwa kinastahili kutumika katika jamii ya huko kilipogunduliwa kwa dhana hiyo, kuna mantiki kubwa endapo sisi kama Taifa huru tukawa na kiapo chetu ambacho watoa huduma wataapa na kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Je mtaala wa elimu katika vyuo vya afya uhusishe ufundishwaji wanafunzi kuhusu kuwatibu watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja kama wagonjwa wengine?
Ukienda katika suala zima la dini sijapata kuona sehemu inayohalalisha swala hili la mapenzi ya jinsia moja hata nilipopata wasaa wa kuzungumza na wazee wangu kuhusu suala hili nao wakasema hata wakati huo wa jando na unyago suala hili halikuwepo kabisa hivyo halifai kabisa kuwepo inchini wala kuzungumziwa lakini nilipowaambia sasa tayari suala hili lipo na watu wapo wanaoyafanya haya ,sasa tunafanyaje wakakosa majibu japo wengi wanaitaka serikali kuwawajibisha kama kuwachukulia hatua za kisheria.
Nimeandika andiko hili ili kuona namna gani linavyomwathiri mtoa huduma wa afya na jamii inavyolichukulia. Katika kiapo kuna kipengele kinasema tibu wagonjwa wote kwa usawa bila kujali jinsia, rangi, kabila au utaifa.
Kumgundua mgonjwa kama huyu anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja sio rahisi ukimwona kwa macho mpaka pale yeye mwenyewe atakapo amua kuweka wazi lakini kwa mtoa huduma ya afya kuna namna anaweza akafanikiwa kugundua mfano mgonjwa akija na maambukizo ya magonjwa ya ngono sehemu ya haja kubwa hii inaweza ikampa uelekeo ya kuwa huyu anaweza kuwa anajihusisha , sasa kulingana na kiapo lichoapa jee amtibu? Jibu ni ndiyo lakini tamaduni yake inasemaje, hawa watu wamekiuka mila na desturi, je amripoti sehemu za mamlaka kama polisi?
Hivyo ni pendekezo langu kwa wizara hizi mbili za afya na elimu kuona namna bora ya kukiweka sawa hiki kiapo ili kiweze kuendana na mila na desturi za mwafrika.
Mawasiliano; 0745265780

Upvote
0