Kiapo cha ndoa ya MC pilipili

Kiapo cha ndoa ya MC pilipili

Freightliner

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2013
Posts
720
Reaction score
527
mchungaji anaongea hiki na jamaa anaongea kile tofauti kabisa sasa sijui ni ushamba,ujinga au welevu mwingi au kwa makanisa ya wenzetu hiyo ni kawaida tu
 
Amefunga Ndoa Kanisa Gani
Huyo Mchungaji Anaitwa Nani
 
Ushamba na ujuaji hawa wagogo sio kabisa kuna wa jalalani na yule wa jana aliyemlawiti mamake mzazi
 
Labda Usupastaa wake unamfanya afanye mbwembwe mpaka kwenye mambo muhimu na ulimbukeni pia wa usupastaa
 
[emoji16][emoji16][emoji16]Siku zote Mungu husimamia maneno yako,wakati wa dhiki na tabu hawatakuwa nao.

sasa jiulize watakuwa na wakati gani,aither wakati uwepo wao wasiwe pamoja,au wawepo wao wakato usiwepo kitu ambacho hakipo.
 
Kiapo na ubatizo huwa ni vielelezo tu mbele ya macho ya watu na sio kwa Mungu!
 
Niliona nikacheka tu,ni upuuzi wa kiwango cha uprofesa,kufanya utani kwenye mambo ya muhimu
 
Jamaa Analeta mzaha na Mungu.

Anasahau kua ni Mungu alompa kipaji hiki ili kimtoe matopen hadi juuu juuu sana.

Maajabu amekua kama Shetan, aliyekua malaika bora kuliko wengine na wakipekee. Sababu ya uzuri wake. Akajikweza juuuu nakufikiria ukuu wa Mungu...hatimaye shetan akatupwa.

Huyu jamaa, asipotubu kuna siku atashangaa karudi kule alikotoka.
 
Ile ndoa imekosa baraka za Mungu na bila shaka itavunjika baada ya wiki chache
 
Biblia yenyewe inatambua maisha yetu ni kama maua, tutachanua lakini itafika Siku tutasinyaa na kudondoka kabisa.

Biblia yenyewe inatambua miaka yetu ya kuishi ni 70 zaidi ya hapo ni taabu na mateso. Zaburi90:10
AYUBU 14:1-2... Pamoja na kwamba ni miaka 70 lakini imejaa tabu ,magonjwa , dhiki nk.

Sasa yeye anamaanisha kwamba ataishi na mke wake wakati "Wamechanua tuu" na jua likiwa Kali uwa likianza kusinyaa lazima waachane kila mtu akapambane na hali yake.( Japo yeye aligeuza akitaka kumaanisha tabu , magonjwa umasikini hazitajitokeza).

Leo akipata ajali mke wake ana haki ya kumuacha kwa sababu kiapo chao cha ndoa ni kuwa pamoja wakati wa raha tuu na siyo shida dhiki na magonjwa.

Nikipata mtu wa kula kiapo kama hicho juu yangu, akifilisika tuu hanioni, akianza blah blah namrudisha siku ya ndoa namwambia ulisema tutakuwa pamoja kwenye raha tuu na siyo umasikini dhiki na magonjwa. Siwezi kwenda kinyume na kiapo.
 
[emoji16][emoji16][emoji16]Siku zote Mungu husimamia maneno yako,wakati wa dhiki na tabu hawatakuwa nao.

sasa jiulize watakuwa na wakati gani,aither wakati uwepo wao wasiwe pamoja,au wawepo wao wakato usiwepo kitu ambacho hakipo.
Mc Pilipili ji mweupe kabisa! Hajui neno ndio sababu ya yote yale. Lkn pia angefungia kwenye makanisa yenye heshima zake kama Catholic na KKKT sidhani kama angeleta ule ujuha wake.
 
Uzi bila picha au video ni sawa na demu mwenye dera bila tako.
 
Biblia yenyewe inatambua maisha yetu ni kama maua, tutachanua lakini itafika Siku tutasinyaa na kudondoka kabisa.

Biblia yenyewe inatambua miaka yetu ya kuishi ni 70 zaidi ya hapo ni taabu na mateso.

Sasa yeye anamaanisha kwamba ataishi na mke wake wakati "Wamechanua tuu" na jua likiwa Kali uwa likianza kusinyaa lazima waachane kila mtu akapambane na hali yake.( Japo yeye aligeuza akitaka kumaanisha tabu , magonjwa umasikini hazitajitokeza).

Leo akipata ajali mke wake ana haki ya kumuacha kwa sababu kiapo chao cha ndoa ni kuwa pamoja wakati wa raha tuu na siyo shida dhiki na magonjwa.

Nikipata mtu wa kula kiapo kama hicho juu yangu, akifilisika tuu hanioni, akianza blah blah namrudisha siku ya ndoa namwambia ulisema tutakuwa pamoja kwenye raha tuu na siyo umasikini dhiki na magonjwa. Siwezi kwenda kinyume na kiapo.
Yesu pia aliwaambia wanafunzi wake duniani kuna dhiki, na dhiki yenyewe ni pamoja na changamoto za ndani ya ndoa. Mc Pilipili hajui neno, makanisa yao wamezoea kuhubiriwa njoo upokee garii, njoo upokee baraka uende ulaya!
Lakini kufundishwa neno la Mungu liwe Msaada katika maisha yao kama wafanyavyo Wacatholic na KKKT hakuna.

Na uhakika yule mchungaji aliyefungasha ile ndoa angekuwa wa KKKT au padri wa Kikatiliki angemchapa Kofi.
 
Askofu alikuja kuongea kwamba watu kama hawawezi kufuata kiapo cha kanisani basi wakafungie ndoa sehemu nyingine.

Mlutheri lakini ana mapokeo kama anasali kwa manabii wanaohubiri pooookeaaa gari , poookeaaa afya njema bila maradhii, poookea kila kitu. Njoooo kanisani na suruali Mungu anaangalia Moyo. Na mambo kama hayo na wanasahau kufundishi Ukweli kuhusu Biblia , wanatafuta masomo ya kuwafariji na kupindua maandiko.

AYUBU 14:1-2... “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. 2 Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe”...

Mwanadamu hana siku nyingi za kuishi hata abweteke. Hata hivyo pamoja na uchache wa siku za mwanadamu, Ayubu anasema zimejaa taabu (magonjwa, dhiki, umasikini kila kitu). Atavukaje hapa?

Sasa mtu atashangaa mwezi ndoa imevunjika aanze kulalamika.
 
Hili tukio limethibitisha hisia zangu toka mwanzo kuwa uhusiano wao unakitu ndani yake, yule bint namuonea huruma kwa kweli.
 
Back
Top Bottom