Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Huu ni ukweli ambao wengi hawaujui kwani umejificha ya kuwa lugha ya kiarabu ndio lugha iliyotumika kuufikishia ulimwengu elimu karibu zote.
Lugha ya kiarabu ambayo ndiyo lugha iliyoteremshiwa Qur'an imetoa fursa za wazi kwa walimwengu dunia nzima na kuwapa ujanja wa kuishi na kuifaidi dunia.
Kwa ufupi kabisa ufunguzi wa ulimwengu kielimu ulianzia Baghdad wakati wa utawala wa bani Umayya na baadae utawala wa Abbasiya chini ya utawala wa Haroun Alrashid.
Tawala hizo ndizo zilijenga maktaba kubwa sana iliyoitwa baitul Hikma ambayo ilidumu kwa karne nyingi kabla kubomolewa katika vita kutoka watawala wa kikristo waliopitia bara hindi.
Chanzo cha maktaba hiyo ilikuwa ni wakuu wa koo za kiarabu waliopenda kuhifadhi Qur'an na hadithi za mtume Muhammad saw pamoja na mashairi mazuri ya koo zao.
Mara maktaba hiyo ikaanza kuweka vitabu vyengine vilivyopatikana katika tawala ambako majeshi ya waislamu yalikuwa yakienda wakati wa vita na kutoka misafara ya kawaida ya kibiashara.
Maandishi hayo hayakuwa katika mfumo wa vitabu vya kisasa yalipatikana kutoka tawala za kirumi,kigiriki na kihindi.Maandishi hayo yailetwa hapo na kutafsiriwa kuingizwa lugha ya kiarabu.
Maktaba hiyo kila miaka ilivyoongezeka ikapanuliwa na kuongezwa vitengo vya matawi mbali mbali ya kielimu ukiongezea na kitengo cha uchapishaji.
Hatimae teknolojia ya uchapishaji na uandishi kwa njia nyepesi uliochukuliwa kutoka mbali kama vile China ukaingizwa kwenye maktaba hiyo na kuongeza kasi za uandishi na tafsiri.
Vitengo vilivyonawiri zaidi katika kituo hicho ni vile vya elimu ya tiba,elimu ya anga na hesabati chini ya mwanahesabati Alkhwarizm ambaye ndiye mwandishi wa kitabu cha aljebra alichokiandika katika kutafsrii mahesabu yaliyomo ndani ya Qur'an juu ya mirathi.
Umaarufu wa maktaba hiyo ambao uligeuka kuwa kama chuo cha elimu uliwavuta watu wengi sana kutoka maeneo ya jirani ikiwemo Iran na majimbo ya Urusi kuja kujisomea au kwa kazi maalumu. Kulikuwa na wafanyakazi wa kila fani na kutoka maeneo mbali mbali.Walikuwepo waliokuwa na asili za kiyahudi na makabila mengineyo ya jirani.
Kituo hicho kilipobomolewa na kuchomwa moto,mto wa dijla ambao unajulikana sasa kama euphrates uligeuka rangi kuwa mweusi kutokana na wino wa vitabu hivyo.
Wakatokea baadhi ya wasomi na waliokuwa wafanyakazi wa kituo hicho wakachagua baadhi ya nakala walizoweza kuziokoa na kwenda nazo maeneo yao.Miongoni mwa hao ni Nasrudin Al tulsi wa Azerbajan ambaye alikwishajenga kituo chake cha anga huko kwao.Yeye alifanikiwa kuokoa vitabu zaidi ya 40,000 ambavyo alikuwa akivibeba kidogo kidogo kwa kutumia farasi na ngamia.
Pamoja na kupigwa vita,waislamu nao kwa fitna walikuwa na ugomvi baina yao wenyewe.Wako walionusurika vifo na kuamua kukimbilia maeneo ya mbali ambako tayari athari za tawala za kiislamu zilikwishatangulia.
Maeneo hayo ni kama vile kaskazini ya Afrika,Libya,Tunisia,Aljeria na Morocco mbali na maeneo ya ndani ya kama vile MalimChad na Niger.
Kwa upande wa Ulaya ya sasa waislamu walikwishatangulia Spain zamani. Mmoja ya waliofanikiwa kuhama na kuendeleza mfano wa tawala za Baghdad ni Abulrahmaan ambaye alikwenda kufanya makazi yake Cordoba chini ya himaya ya Ummawiyah. Miji mingi sana ndani ya Spain iliyojulikana wakati huo kama Andalus ilijengwa kwa nidhamu za tawala za kiislamu ambapo lazima kuwe na maktaba.Miji michache kati ya hiyo ni Granada,Sevile na Toledo.
Kwa mfano papa Sylvester (Gerbet) ni miongoni mwa wakristo wa mwanzo kusoma kwenye chuo kikuu cha kiislamu cha Granada na aliwahi kuhudhuria mafunzo chuo kikuu kikongwe zaidi duniani cha Alqarawiney ambacho kiko Fez nchini Morroco ambacho bado kinaendeshwa kwa mfumo ule ule maarufu kama madrasa.
Papa Syvester ambaye alivutiwa sana na utamaduni wa waislamu na elimu zao alipenda sana somo la hisabati na ndiye wa mwanzo kuingiza elimu hiyo nchini Italy wakati wa utawala wake ambapo mwenyewe alikuwa ni mwalimu pia pamoja na kazi za upapa (1095).
Maktaba ya Toledo ndiyo maarufu zaidi kwani hapo ndipo makabila mengi ya Ulaya kuanzia Ureno, Ufaransa,Italy na kote kwengineko walisoma na kutafsiri kazi hizo kutoka lugha ya kiarabu na kuingiza kwenye lugha zao za asili. Katika maktaba hiyo pia walikuwepo wafasiri walioweza kuingiza elimu hizo kwenye lugha ya kiyahudi ya kiebrania.
Ikumbukwe wakati ulimwengu wa kiisalamu ukiwa unairithisha dunia elimu kwa lugha zao kutoka kiarabu lugha maarufu za sasa kama vile kiiengereza na kifaransa hazikuwepo au ndio muda zilikuwa zinazaliwa na kuanza kujulikana.
Vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya kiarabu na kutumika kwenye vyuo vikuu vingi vya ulaya walivyojenga wenyewe ni vingi sana.Ngoja tutaje baadhi tu ya vitabu hivyo.
1. AL HAW. Ni kitabu cha tiba kiliandikwa na Abubakr Al Razi (864 -935)AD.Kinajumuisha vitabu vidogo (volumes) 23.Kilitafsiriwa kuingizwa lugha ya kilatin na myahudi aitwaye Faraj ben Salim kutoka visiwa vya Sicily mnamo mwakka 1276.
2. AL QANON FIY TTIB cha tiba kwa kiiengereza kinajulikana kama The canon of medicines. Kiliandikwa na Ibn Sina (980 -1037)AD.Kitabu hicho kimetumika kama rejea kubwa kwenye vyuo vikuu vya Ulaya mpaka mwaka 1650.Kilikuwa kikitoa ufafanuzi wa tiba na madawa kwa kutumia michoro kufahamisha vizuri.
3. KITAB AL TASIF cha Abul Qassim (936-1013)AD.Ni mkusanyiko wa vitabu vidogo 30.Abulcasis ndiye mvumbuzi wa vifaa zaidi ya 200 vinavyotumika mpaka leo kwenye vyumba vya upasuaji na vitabu vyake vimetumika kufundishia Ulaya kwa zaidi ya miaka 500.Aliishi na kufia mjini Cordoba ndani ya Spain.Nyumba yake mpaka leo ipo na imepewa thamani ya juu katika utalii wa majengo.
4.AL KITAB AL MUKHTASAR FIY HISAB ALJABR WAL MUQABALA.Kiliandikwa na Muhammad bin Mussa Alkharizm (780-850).Alikuwa ni mmoja ya wafanyakazi mashuhuri wa kitengo cha kutafsiri maandishi kwenye jengo la Baitul Hikma na baadae akawa ndiye mkurugenzi wa kituo hicho.
Pamoja na kazi nyingi alizozifanya alisoma na kutafsiri maandishi ya Euclid, mwanafalsa wa zamani wa kigiriki.Hata hivyo maandishi na hesabu zake za Aljebra ambazo ndizo zilizozalisha ujanja wote wa hesabu duniani haujaonekana kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na michoro ya maumbile ya Euclid.
Nakala halisi ya kitabu cha Alkhwarizm katika hati zake za kiarabu kinapatikana kwenye maktaba ya chuo kikuu cha Oxford nchini Uiengereza.