Kiasili kila mwanadamu ni mfanyabiashara huwezi kuikimbia asili, ukistaafu utairudia tu

Kiasili kila mwanadamu ni mfanyabiashara huwezi kuikimbia asili, ukistaafu utairudia tu

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Biashara ni kitendo cha kubadilishana vitu.

Mfumo wa ajira ulikuja ili kupata watu wa kusaidia kazi watu wengine ambao wanafanya biashara fulani.πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Kama sikosei mfumo ulianza kipindi cha zamani huko watu walipoanza kutawala wengine. Kunazuka wanadamu wajanja ambao wanawazidi wengine akili kisha wanawachukua wawafanyie kazi zao.

Wanadamu hao wanafanya kazi za watu huku wakiwa wananawiri na kung'aa. Umri wao unasonga na kukosa nguvu kisha wanaachishwa kazi na kurudi kwenye asili yao na kuanza kukongoloka na kufa kwa presha. Zile kazi wanapewa watu wengine wenye umri mdogo na nguvu.

Hapo nina maana ya kwamba kujiajiri ni kazi endelevu ambayo mwanadamu hawezi kustaafu kwasababu yupo kwenye asili aliyoumbiwa.

Hivyo ndivyo jinsi Mungu alivyotuumba ili kila mtu afanye shughuli zake kisha tubalishane vitu, kila mtu aweze kupata kile anachohitaji. Hiyo ndiyo asili. Na hiyo asili mwanadamu hawezi kuikimbiaπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€. Atarudi tu.

Kwasababu ajira inamwisho.
Mwisho wa ajira ni pale unapostaafu.

Mwisho wa ajira ni pale unapotumbuliwa au kufukuzwa kazi.

Mwisho ukifika utakuwa unakula nini usiporudi kwenye asili yako?

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€Lazima utarudi kwenye asili tu ila utakua umechelewa na kufa kwa presha.

Hata uwe waziri mwisho wa ajira yako ukifika utarudi kwenye asili.

Hata uwe mwalimu, dakitari, mkufunzi, mhadhiri, mhandisi, mwanasiasa mwisho wa ajira ukifika utarudi kwenye asili. Na utaanza kutonawiri tenaπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Ama utaingia shambani kulima, πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ au utatafuta fremu ya biashara kwa udi na uvumba.

Lakini huyo aliyekuajiri mwenye kampuni atazidi kunawiri na kustawi maana yeye yupo kwenye asili yake.

Jamii Forums huu utakua uzi wa mwakaπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ. Nasuburi zawadi yangu mwakani.
 
Job:Ni Ile kazi unayofanya kutokana na ulichosomea.
Work: Ni Ile kazi uliyoumbwa kuja kuifanya hapa duniani. Kwenye hii kazi hakuna kustaafu.
Watu wengi wakiwa kwenye ajira huwa hawana muda wa kufanya biashara maana muda wao wote wameshau exchange for paycheck. Ila wakishastaafu, huwa na muda mwingi zaidi kuliko paycheck ndio hao huanza kukurupukia kila biashara wanazoziona, na kwa vile hawana experience inayotokana na ku FAIL mara kadhaa huangukia pua.
 
Kuajiriwa ni Utumwa mambo leo(Modern Day Slavery), kwa sababu miaka nenda miaka rudi, utakua unamtajirisha alie kupa kibarua...hapo hapo kama kuna hasara pia wewe utapata chako bila kutathmini hasara.

Mfanya kazi siku zote atakua mlia hoi kwa sababu hata kazini anapofanya kuwe bora yeye pato lake litakua lile alilokubaliana na tajiri..! Maisha yanavyozidi kupanda ndio utumwa unavyozidi.

Kifikra, mfanya kazi huwa mawazo mengi ni kuboresha kazi aliopewa na mwajiri na hana mawazo yeyote ya kujitoa kwenye huu utumwa, kwani biashara nayo huwa ina changamoto nyingi nazo pia huwa ni mafunzo. Ndio hapo unapata mtu ulimwacha kidato ukaenda chuo ukamaliza baada ya kufanya kazi miaka mingi humfikii kwa sababu amesomea kupitia changamoto alizopitia, na wewe baada ya kustaafu ndio unaanza chekechea kibiashara.
 
Huo ndio ukwel mtupu kuhusu ajira
 
Back
Top Bottom