Kiatu cha Diamond Platnumz chakatika mahakamani

Kiatu cha Diamond Platnumz chakatika mahakamani

So what? Acheni kumpa kiki huyo Domondi wenu! Ameshabuma
_20170720_215946.JPG

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wakili MSOMI
 
Kiiiruuuu! Hivi kukatikiwa sandal nayo ni habari kumbe!!!!
 
Maalimu sabalaheri.
Yule binti wa usa naona anamdhalilisha sana sheikhe wetu.
Mambo yetu yaleee tunayoyapenda yote yanaandikwa bila aibu.
Sijui twelekea wapi sheikh.
Lakheri sheikh...

Yule sheikh namshauri aje kwa nabii wetu mpendwa Titto. Hakika ya kale yatakuwa mapya sheikh wangu
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mkuu umekaa umefikiriaaaa mpaka akili yako ndo ikaishia hapo ukaamua uposti vya Ajabu Sio..! But anyway sio mbaya nakumbuka Nilikuwa O level Mwalimu wangu wa civics aliwai kusema "MJINGA AKITOA WAZO LA KIJINGA YAPASWA KULIHESHIMU WAZO LAKE ILA USILIFUATE" Sio Mimi nimenukuu mkuu
 
Ndio maana ustaa ni mzigo wa miba. Kwa sasa akipanda daladala ni habari, akila kwa mama lishe ni habari. Diamond ni star. Kwa hiyo hata jambo la kawaida ni habari!
🙁🙁Hii nayo habari!!
 
SOURCE: MWANANCHI
Waswahili wanamsemo wao usemao ajali kazini. Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond ambaye amewasili katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Kisutu lakini amekutana na balaa baada ya kiatu alichovaa kukatika.

Kwa ufupi
Msanii huyo alianza kuchechemea kuonyesha mguu wake wa kushoto kulikuwa na tatizo. Ghafla alibadili mwelekeo na kwenda kwenye gari. Kilichotokea hapo ni kwamba ‘sendozi’ yake ilikuwa imekatika.

Hadija Jumanne
Dar es Salaam, Waswahili wanamsemo wao usemao ajali kazini. Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond ambaye amewasili katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Kisutu lakini amekutana na balaa baada ya kiatu alichovaa kukatika.

Msanii huyo alianza kuchechemea kuonyesha mguu wake wa kushoto kulikuwa na tatizo. Ghafla alibadili mwelekeo na kwenda kwenye gari. Kilichotokea hapo ni kwamba ‘sendozi’ yake ilikuwa imekatika.

Msanii huyo alionekana kuendelea na shughuli iliyompekeka mahakani hapo huku akiwa amekaa nje kwenye bechi pamoja na wakili wake kusubiri utaratibu.

Diamond ambaye aliambatana na mwanasheria wake, akiwa katika gari aina ya Land Cruiser Prado rangi ya bluu mpauko.

Mara baada ya kuwasili katika viunga vya Mahakama ya Kisutu alipitiliza moja kwa moja hadi Mahakama ya Watoto iliyopo ndani ya viunga vya Mahakama ya Kisutu.


Kwani ww ujawahi kukatikiwa na viatu?
Sasa hapo ni kitu gani cha ajabu
 
Back
Top Bottom