Kiba ampigia debe Diamond

Kiba ampigia debe Diamond

Yawezekana dili la sony kafanikisha diamond so jamaa anashukuru
 
Achana na huyu mfa maji.... Kachochezi ka-bifu haka katoto wewe acha tu, kacheki nyendo zake utagundua sitanii
Nyendo neno pana bro, usimtafutie mwenzio balaa bure...
 
CEO? Wabongo wanachekesha sana, mtu kumiliki keyboard, computer na microphone nne unamwita CEO.
Basi waingiza nyimbo pale Aggrey wote ma-CEO? Kiba ni mlezi wa Chibu kimuziki, Godfather...
 
Hahahaa!!
Ila sku hizi naona mademu wa bongo movie wanakomaa na waimba nyimbo.. Hata madansa au hata katoto kakiwa na tunyimbo tumoja bongo muvi hawaoni shida kupanua upaja
Watu wameanza kupanuliana mapaja zamani sana, bila kujali umaarufu au kazi. Kujali sasa hivi Lisa Bongo Fleva wanaruka na mama wa Bongo Movie ni wivu tu...
Waache wavaa milegezo wajilie vyao, mmewasimanga sana!
 
sijui wanachanganyikiwa na nini haki ya Mungu!! ila me nadhani wanaume ndiyo wenye matatizo, mfano diamond alipotoka tu kaanza kukomaa na wema,mara jokate mara Wolper....huyu Idris nae kapiga hela tu huyo kwa wema,huyu Harmonize nae ameona akomae na Wolper,tena huyu Harmonize inawezekana kabisa alikuwa anataka aende kwa wema basi tu amemuonea aibu diamond...nashindwa kizielewa akili za hawa watu kwakweli
Mie nashindwa kuelewa akili zenu, watu wakirukana nyie akina nani hadi mpange na kuamua kama hawa wanafaa au la...
Ukipata hela hata ndugu unabadili wakati fulani, kubalini tu kwamba Bongo Movie kuna akina Dada wakali... Na sio Bongo Fleva tu, na wabunge wenu na mawaziri.
Wapi Sadifa?
 
Alikiba amewaomba watanzania kumpigia kura Diamond anayewania tuzo ya BET zitakazofanyika, Juni 26 Los Angeles, Marekani.
Wiki iliyopita Diamond alitangazwa kuwania tuzo ya BET kwa mara ya pili kwenye kipengele cha Best International Act: Africa akiwa ni msanii pekee kutoka Afrika Mashariki huku tuzo hiyo ikiwaniwa na wasanii wengine kama Wizkid, Yemi Alade, AKA, Cassper Nyovest, Black Koffie, MZVEE na Serge Beynaud.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Alikiba aliwaomba watanzania wampigie kura Diamond kwenye tuzo anazoshiriki za BET na kusema kuwa yeye ndiye msanii pekee anayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo hivyo watanzania wampigie kura ili aweze kushinda.
“Of course nawasupport wote ndiyo, vote for Diamond kwenye tuzo za BET kwa sababu yeye ndiyo anayetuwakilisha,” alisema Alikiba.
Alikiba kwa sasa ni msanii aliye chini ya label ya Sony Music na wimbo wake mpya ‘Aje’ unafanya vizuri kwenye TV na Redio japo una siku tano tu tangu utoke, May 19.

 
UGOMVI NI KWA MASHABIKI TU, ALIKIBA NA DIAMOND NI PEACE AND LOVE
 
Kuna habari mesikia mahali kuwa Kiba ameomba Watanzania wampigie kura Chibu, Baba Tiffah, Nasibu Abduli, Diamond Platinumz, kwenye tuzo Fulani za kimataifa, kwenye Kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
ALIKIBA AKIMUOMBEA KULA DIAMOND
 
UGOMVI NI KWA MASHABIKI TU, ALIKIBA NA DIAMOND NI PEACE AND LOVE


Safi sana, Ally kajibu vizuri japo kale kadada kashambenga shambenga kalitaka kuchafua hali ya hewa, ila kwa kua KingKiba amejaa busara na hekima, kajibu vizuri tu.

#GoKibaGo#
 
Back
Top Bottom