Leo nilikuwa naangalia marudio ya tunzo za CAF kule nigeria,Diamond na wanamuziki wote walikuwa waki perform live ,kweli Diamond pamoja na mafanikio yake makubwa kimziki live performance bado sana. Nimemwangalia Yemi Alade,Mr flava, Femi kuti na kundi moja la South Africa yaani wako vizuri ile mbaya kwenye ku perform live,yaani instruments zinapigwa live na back vocals wapo na wapiga kazi. Diamond ilikuwa kama show ya kudance.
Najua matani-mind,lakini ushauri wangu kwa Platinum wetu ule mwaliko wa kuperform kwenye award kubwa kama ile si kitu cha mchezo so maandalizi ni muhimu ili siku nyingine ukumbukwe kwenye tukio kubwa zaidi. Diamond alitakiwa kupiga live, let's say nyimbo alizoimba kwa kushirikiana na wanamuziki wengine alitakiwa kuwa amemwandaa mmoja wa wanamuziki wake kucover nafasi hizo kama alivyofanya Yemi Alade kwenye wimbo johnny. Ni ushauri tu.