BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Huku kwetu maeneo ya Kibaha hasa Kibaha Kwa Mfipa kuna matukio ambayo ni hatari sana kwa usalama, kwani kuna vibaka wanatusumbua na wanafanya matukio yao majira ya Saa 11 alfajiri wakiwalenga wale watu wanaodamka asubuhi mapema kwenye kwenye majukumu yao.
Vibaka hao wanakaba na kuwapora kwa kutumia mapanga Wananchi wanaopita na hata wale wanaopanda Bodaboda, tunaomba ujumbe huu ufike kwa Jeshi letu la Polisi, hao watu wanaelekea kutuzidi nguvu Wananchi na kutukosesha amani.
Wengi wao wanatumia Pikipiki huku wakiwa na silaha za jadi ikiwemo mapanga, bisibisi na marungu.
Kinachouma zaidi ni kuwa viongozi wa Serikali za Mitaa wengi nao ni kama wanaogopa kuwachukuliwa hatua watu hao, kwani ukizungumza na baadhi ya Bodaboda wema wanasema wanawajua wanaofanya matukio hayo ila hawawezi kuwataja kwa kuwa nao wanahofia usalama wao.
Hili jambo linatakiwa kuchukuliwa hatua kabla mambo hayajafika mbali na tabia kukomaa ikiwemo watu kupoteza maisha pia.