BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
Kwa miezi kadhaa nadhani ni tangu mwishoni mwa Mwaka 2025, Wananchi wengi wa Kibaha Maili Moja, Mtaa wa Muheza tulipiga kelele kuhusu ukosefu wa huduma ya maji. Tatizo hilo lilitufanya tupate changamoto kubwa katika shughuli zetu za kila siku, lakini tunashukuru kwa sababu kilio chetu hatimaye kimesikilizwa.
Tumeanza kupata maji, ingawa bado hayatoki kila siku. Angalau tunayaona kila baada ya siku mbili, jambo ambalo ni nafuu ikilinganishwa na hali tuliyokuwa nayo awali.
Tunaelezwa kuwa tatizo lilikuwa kwenye pumpu inayovuta maji, ambayo imefanyiwa marekebisho na kuanza kufanya kazi. Tunashukuru kwa hatua hiyo, lakini tunaomba mamlaka husika kuhakikisha huduma inakuwa ya uhakika na endelevu, ili tusirudi tena kwenye hali ya kukosa maji kwa muda mrefu.
Pia soma:
~ Kibaha Maili Moja Kwa Mbonde tumeshasahau huduma ya DAWASA, tukiwauliza wanasema maji hayana presha
~ Janga la uhaba wa maji ni kubwa kwa wakazi wa MailiMoja – Kibaha (Pwani), shida ni kubwa mno