Katika hali ya kushangaza na kustaajabisha, wananchi kijiji cha misufini wilaya ya kibaha wamezuiwa na RUWASA kutumia maji ya kisima walichochimba kwa nguvu zao wenyewe kisa RUWASA kutaka kuingiza kisima hicho kwenye mradi wa maji vijijini.
Kisima hicho ambacho kilishaanza kuwanufaisha wanakijiji hao kwa zaidi ya miezi 6 kilikuwa pia kinahudumia wanafunzi wa shule ya msingi misufini pamoja na zahanati mpya iliyoanza kazi mwishoni mwa mwaka jana.
Kwa sasa kisima hicho kimefungwa zaidi ya miezi miwili na hatma ya lini kitawanufaisha wanakijini ipo chini ya maamuzi binafsi ya RUWASA japokuwa hawajahusika kutoa ata senti moja kugharamikia uchimbaji wa kisima hicho. Jambo kama hili utaliona Tanzania tuu [emoji3].
Wakati mama Samia anahangaika kupambana wanachi wapate huduma, kuna viongozi wanakwamisha makusudi maendeleo.
@dawasco
Wizara Maendeleo ya Jamii