DOKEZO Kibaha: RUWASA yakataza kijiji kutumia maji ya kisima kwa zaidi ya miezi miwili

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Awa jamaa wa kusomea alubadili
 
Mkuu, tuweke Kumbukumbu sawa. Mlichimba wenyewe au Wafadhiri ndo waliwachimbia maji?

Je, Makusanyo ya Maji nani anapokea hela, RUWASA au wenyewe Wanakijiji? Kama Wanakijiji, Mwezi mnakusanya kiasi gani?

Je, Kijiji chenu kimejiunga na Jumuia za Maji vijijini? Nani anapima Usalama wa maji?
 
Mmh! Makubwa. Ushaambiwa mleta mada ni muongo kadanganya.
 
Sheikh, kisima tulichimba kwa ushirikiano kati ya kijiji na mfadhili (mtu binafsi na sio serikali), kijiji kikitowa eneo, nguvu kazi kiasi, baadhi ya matirio na kikiendesha mradi kwa gharama zake.

Kabla ya kusimamishwa, makusanyo yalikuwa yakichukuliwa na mwenyekiti ya kijiji na fedha kuingizwa kwenye mfuko wa kijiji (japo taarifa za mapato haya hazipo wazi sana).

Ndipo sa ghafula tukapokeya taarifa kutoka kwa uwongozi wa kitongoji kuwa ruwasa wamezitisha mradi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…