Kibaigwa; Muokoeni mtoto Filemon anayeteswa na mama yake

Ilivyokuwa ni kwamba nilikuwa napita nikafika maeneo hayo jioni jioni sasa mara nikasikia mtoto analia sana nikauliza wenyeji wale wakanambia huyo anachapwa na mama yake nilipotaka kujua zaidi kwanini amechukua muda mrefu sana kumuadhibu ndipo nikapewa stori zote hizo. Nikawahoji kama wamewahi kulifikisha popote wakasema laa! Ndipo nikawaelekeza namna ya kufanya kisha nikaondoka kuendelea na safari zangu
 

Kweli mna matatizo Na elimu inabidi mfunzwe; unashindwaje kutoka hapo Na Kwenda Police? Nipe maelekezo zaidi Mimi nitakuja maeneo hayo! Nipe hata namba ya jirani au chochote
 
Nyumbani kwangu naishi na mtoto aliekumbwa na madhira ya aina hio,anaundugu na yf,nilifika ustawi wa jamii, nimemchukua dogo anaendelea na shule.

Wapo watoto wanapitia changamoto nyingi sana na wanakosa wakuwasaidia.

Dogo alipofika alikua ananieleza mambo yakuogopesha Sana kwamba babu yake alikua anamfundisha uchawi (kuwanga),mara kadhaa usiku anakurupuka anapiga kelele kama mtu aliepagawa na pepo anasema Babu amemfuata.

Siku moja usiku dogo akapagawa akawa analia hovyo badae akapitiwa usingizi,asubuhi kulipokucha nikamuuliza dogo kulitokea nini,dogo akaniambia Jana Babu yake alikuja akawatoa wanangu wote nje kichawi,anasema badae akawarudisha baada ya mmoja mdogo kuamka,dogo anasema watoto wadogo wanawaona wachawi hivyo mototo alipostuka wakawarudisha ndani haraka.

Dogo anaweza amka asubuhi analia anasema babu ameniambia ataniua kwasababu ametoa siri.

Kama una moyo mwepesi na huna imani dogo ninaeishi nae ungemrudisha Kijijini.Niliapa kumsaidia dogo kwa lolote japo kule Kijijini yule babu anatoa vitisho kwetu.

Nashukuru Mungu kunakikundi cha wanamaombi wameondoa kabisa hio hali dogo sasa kaacha hali ya kupagawa mapepo usiku.

Nakushauri jitahidi umsaidie huyo mtoto.
 
Ujue kuna watu wanaweza kujiona wao ndo wao wengine wote mafala, wao ndo wana akili na uchungu sana kuliko wengine!

Hivi hushangai kwanza tukio nimeambiwa tangu Jumamosi lakini naandika leo? Hivi hujiulizi ilikuwaje kuwaje mpaka mimi nikafika hapo wakati nilikuwa kwenye safari zangu tu? Hivi hushangai mtoto hajapata msaada tangu mama alipoanza kumnyanyasa mpaka hivi? Hivi unajua nilikuwa na mambo gani yanayonikabili mpaka nikaishia kutoa mwongozo tu na kuondoka?

Kikubwa mimi nimetekeleza kipande changu nilichojaaliwa hayo mengine mnayoleta hapa tambueni mimi siyo Masihi
 
Usipanic JF,achana na maneno yasiohusu mada yako ya mtoto, to focus kwenye kumsaidia dogo
 
Mimi siku zote huwa namwomba sana Mungu anisaidie nisije kutokea kuishi mazingira ambayo kuna mtu wa aina hii!
 
Au alimuiba huyo mtoto.
Dauti yangu pia ilikuwa ni hiyo lakini wanasema ni mwanae kabisa wa kumzaa na wakienda wanatukanwa huku wanaulizwa kama walimsaidia kuzaa...

Eti hela hiyo dogo alinunua chakula (kitu kama ndizi hivi if I'm not mistaken) akala ili kupoza njaa ndo kosa lenyewe!
 
Kuna watu wa ajabu saana dunia hii



Mi nilitegemea uje na stori konki
Hasa uzi useme hivi
"Niliemshtaki kwa kumfanyia ukatili mwanae afungwa miaka........."

Au
Ongezeeni wadau kichwa habari hata wewe kingekukosha

Niliemtwanga kwa ukatili dhidi ya mwanae azinduka
 
Hilo ni la ustawi wa Jamii kamripoti police dawati la jinsia atapimwa akili yake, wanawake wengine huwa ni vichaa kasoro makopo
 
Watoto walioteswa utotoni wakaunga unga shule vyuo wakipata uongozi huwa ni madikteta.
Madikteta wote ni zao la mateso utotoni thus wenzetu huwezi ukapewa uongoze watu bila kuchunguza ulilelewaje Ili kuepuka viongozi type ya Sabaya.
 
Please nitumie Ana information kamili Mimi nitamsadia huyo mtoto; yani watu wazima mnashindwaje msaidia huyo mtoto?
mkuu akikupa mawasiliano ukienda uje na mrejesho nimehuzuniaka sana Huyo mama ana frustrations sio Bure,ningekua pande hizo ningeenda kuliona Tatizo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…