Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ilivyokuwa ni kwamba nilikuwa napita nikafika maeneo hayo jioni jioni sasa mara nikasikia mtoto analia sana nikauliza wenyeji wale wakanambia huyo anachapwa na mama yake nilipotaka kujua zaidi kwanini amechukua muda mrefu sana kumuadhibu ndipo nikapewa stori zote hizo. Nikawahoji kama wamewahi kulifikisha popote wakasema laa! Ndipo nikawaelekeza namna ya kufanya kisha nikaondoka kuendelea na safari zanguMkuu nakuomba timiza wajibu wako kwa kusaidia kufikisha taarifa za unyanyasaji wa huyo mtoto kwa serikali ya mtaa husika au polisi.
Jukumu la kuhakikisha watoto wanalelewa kistaarabu ni la jamii nzima kwa kuwa akiachwa akaishi katika ukatili huo baadae atakuwa na roho na tabia za ajabu ambazo zinaweza hatarishi kwa jamii nzima,kwako, kwangu au kwa watoto wetu.
Tabia nyingi mbaya tuzionazo au tufanyiwazo na watu tusiowajua ama tunaowajua ni matokeo ya jamii kupuuza matukio kama haya.
... aione Joyce Kiria.Feminists wajitokeze katika hili
Huyu mtoto anaishi na MAMA YAKE MZAZI pale Kibaigwa sehemu inaitwa Mbagala, anasoma chekechea. Mama huyo anamtesa sana mtoto huyo na haambiliki hata kwa mbali mpaka majirani wameamua kuwa wakimya na kubaki kuangalia tu jinsi mtoto huyo anavyoteswa. Wanasema mama huyo ana 'mdomo mchafu' sana pindi utakapojaribu kumuonya/ kumsihi juu ya unyanyasaji wake kwa mwanaye...
Usipanic JF,achana na maneno yasiohusu mada yako ya mtoto, to focus kwenye kumsaidia dogoUjue kuna watu wanaweza kujiona wao ndo wao wengine wote mafala, wao ndo wana akili na uchungu sana kuliko wengine!
Hivi hushangai kwanza tukio nimeambiwa tangu Jumamosi lakini naandika leo? Hivi hujiulizi ilikuwaje kuwaje mpaka mimi nikafika hapo wakati nilikuwa kwenye safari zangu tu? Hivi hushangai mtoto hajapata msaada tangu mama alipoanza kumnyanyasa mpaka hivi? Hivi unajua nilikuwa na mambo gani yanayonikabili mpaka nikaishia kutoa mwongozo tu na kuondoka?
Kikubwa mimi nimetekeleza kipande changu nilichojaaliwa hayo mengine mnayoleta hapa tambueni mimi siyo Masihi
Mimi siku zote huwa namwomba sana Mungu anisaidie nisije kutokea kuishi mazingira ambayo kuna mtu wa aina hii!Huyu mtoto anaishi na MAMA YAKE MZAZI pale Kibaigwa sehemu inaitwa Mbagala, anasoma chekechea. Mama huyo anamtesa sana mtoto huyo na haambiliki hata kwa mbali mpaka majirani wameamua kuwa wakimya na kubaki kuangalia tu jinsi mtoto huyo anavyoteswa. Wanasema mama huyo ana 'mdomo mchafu' sana pindi utakapojaribu kumuonya/ kumsihi juu ya unyanyasaji wake kwa mwanaye.
Habari kwa ufupi...
Baba na mama Filemon wana watoto wawili yaani Filemon na mdogo wake mdogo zaidi. Walikuwa wakiishi Morogoro mara huyu mwanamke akamshauri mumewe wakajenge Kibaigwa.
Baada ya kujenga mwanamke akaja kukaa hapo na akakataa kabisa kurudi Moro. Maelezo mengine hapo ni marefu ila kwa ujumla baada ya kuanza kuishi mwenyewe hapo ndipo mateso kwa mtoto yalipoanza nataja mifano kadhaa.
Chakula mama anapika kutwa mara moja yaani kama ni saa kumi jioni ugali basi mpaka kesho saa kumi jioni tena ndipo wale halafu siyo kwamba hakuna chakula ndani, laa! Hakuna shida kihivyo ya kuwafanya wale mlo mmoja.
Akianza kumpiga anapiga kama sio mtoto tena kosa lenyewe unakuta ni limetokana na yeye mwenyewe mama.
Kubwa kuliko ni hivi juzi sasa wakati napita hapo mpaka kupewa mikasa yote hiyo. Ni kwamba dogo alishutumiwa ameiba hela ndani aisee akapigwa kisha akakamatwa mkono na kuingizwa kwenye kama siyo majivu ya moto basi mafuta ya moto akaungua mkono.
Majirani wanahisi ni mafuta kwa sababu inaonesha amechomwa mkono wa kwanza kisha kutaka kuchomwa wa pili akacholopoka akakimbia ila katika kukung'uta mkono basi mafuta yakarukia na matone matone kudondokea mkono wa pili nao ukapata majeraha kadhaa.
Binafsi niliwashauri majirani hao washtaki kwenye ofisi yoyote ya serikali iliyopo karibu lakini walionesha kutokujua lolote kuhusu ofisi hizo.
Kama hiyo website wewe mwenyewe unaijua, chukua link ya thread hii uipost huko wataiona na kusoma taarifaIngia website ya polisi kuna sehemu ya kuripoti uhalifu eleza vizuri hatua zitachukuliwa upesi
Napeleka Polisi immediately, halafu kama kuna ghrama ya kesi nitajitoleaInaonekana ungeua mtu mjumbe!
Dauti yangu pia ilikuwa ni hiyo lakini wanasema ni mwanae kabisa wa kumzaa na wakienda wanatukanwa huku wanaulizwa kama walimsaidia kuzaa...Au alimuiba huyo mtoto.
mkuu akikupa mawasiliano ukienda uje na mrejesho nimehuzuniaka sana Huyo mama ana frustrations sio Bure,ningekua pande hizo ningeenda kuliona Tatizo!Please nitumie Ana information kamili Mimi nitamsadia huyo mtoto; yani watu wazima mnashindwaje msaidia huyo mtoto?