Kibaigwa; Muokoeni mtoto Filemon anayeteswa na mama yake

Kibaigwa; Muokoeni mtoto Filemon anayeteswa na mama yake

Huyu mtoto anaishi na MAMA YAKE MZAZI pale Kibaigwa sehemu inaitwa Mbagala, anasoma chekechea. Mama huyo anamtesa sana mtoto huyo na haambiliki hata kwa mbali mpaka majirani wameamua kuwa wakimya na kubaki kuangalia tu jinsi mtoto huyo anavyoteswa. Wanasema mama huyo ana 'mdomo mchafu' sana pindi utakapojaribu kumuonya/ kumsihi juu ya unyanyasaji wake kwa mwanaye.

Habari kwa ufupi...

Baba na mama Filemon wana watoto wawili yaani Filemon na mdogo wake mdogo zaidi. Walikuwa wakiishi Morogoro mara huyu mwanamke akamshauri mumewe wakajenge Kibaigwa.

Baada ya kujenga mwanamke akaja kukaa hapo na akakataa kabisa kurudi Moro. Maelezo mengine hapo ni marefu ila kwa ujumla baada ya kuanza kuishi mwenyewe hapo ndipo mateso kwa mtoto yalipoanza nataja mifano kadhaa.

Chakula mama anapika kutwa mara moja yaani kama ni saa kumi jioni ugali basi mpaka kesho saa kumi jioni tena ndipo wale halafu siyo kwamba hakuna chakula ndani, laa! Hakuna shida kihivyo ya kuwafanya wale mlo mmoja.

Akianza kumpiga anapiga kama sio mtoto tena kosa lenyewe unakuta ni limetokana na yeye mwenyewe mama.

Kubwa kuliko ni hivi juzi sasa wakati napita hapo mpaka kupewa mikasa yote hiyo. Ni kwamba dogo alishutumiwa ameiba hela ndani aisee akapigwa kisha akakamatwa mkono na kuingizwa kwenye kama siyo majivu ya moto basi mafuta ya moto akaungua mkono.

Majirani wanahisi ni mafuta kwa sababu inaonesha amechomwa mkono wa kwanza kisha kutaka kuchomwa wa pili akacholopoka akakimbia ila katika kukung'uta mkono basi mafuta yakarukia na matone matone kudondokea mkono wa pili nao ukapata majeraha kadhaa.

Binafsi niliwashauri majirani hao washtaki kwenye ofisi yoyote ya serikali iliyopo karibu lakini walionesha kutokujua lolote kuhusu ofisi hizo.
Na hao majiran ni wauaji kwa nn vitendo Kama hivyo vinatokea wasiripoti police
 
Upo karibu mkuu na hapo kwenye tukio? Au ulipita unaishi maeneo tofauti? Kama upo hapo toa maelekezo zaidi yakuweza kufika apo ili mtoto apate msaada..... kuna mdau ameomba location yako akupitie muende pamoja toa ushirikiano mkuu!!!!
 
Mkuu nikuombe sana nenda mwenyewe kituo cha polisi waeleze habari kamili uambatane nao hadi kwa huyo mama na bahati nzuri majirani watakuwa mashuhuda wazuri.

Mtoto hawezi kujitetea mwenyewe bali watu wazima ndo watetezi wao. Usipofanya hivyo huyo mtoto akiendelea kuteseka nawewe utakuwa kwenye mnyororo wa dhambi hiyo.

Inauma sana. Kwasababu nipo mbali tu kikazi otherwise ningekuwa nyumbani ningekuja hapo Kibaigwa kumalizana na huyo mama kisheria ili iwe fundisho kwa wajinga wengine.

Ningekuwa vizuri kwa muda huu ningekutumia hata hela kidogo ya kutwa ili uache shughuli zako ufuatilie jambo hili polisi.
Mi siamini kama ni mama yake mzazi
 
Ilivyokuwa ni kwamba nilikuwa napita nikafika maeneo hayo jioni jioni sasa mara nikasikia mtoto analia sana nikauliza wenyeji wale wakanambia huyo anachapwa na mama yake nilipotaka kujua zaidi kwanini amechukua muda mrefu sana kumuadhibu ndipo nikapewa stori zote hizo. Nikawahoji kama wamewahi kulifikisha popote wakasema laa! Ndipo nikawaelekeza namna ya kufanya kisha nikaondoka kuendelea na safari zangu
Sawa mkuu,
Hata hivyo umefanya vyema kupost humu.
Natumai wapo watu wana connection zitakazosaidia mtoto Filemon kupata msaada.
Kuna wakati kulikuwa na taasis fulani ilikuwa na uzi wake humu na namba ya dharura ya kuripoti matukio ya unyanyasaji watoto.

Tatizo sikumbuki jina la ule uzi wala ile namba.
 
Duuh nimehizunika sana kwa akili zangu mimi ningemchukiua huyo mtt hadi kituo cha police na kumpeleka hospital kama mbwai mbwai yani ninge nunua kesi!
 
Sasa ndio umefanya Nini he ukipita siku ukasikia amekufa kwa kipigo kikali utakua na amani kweli moyoni mwako???
 
Toa anuani kamili mkuu
Kama una nia mbona anuani hiyo inatosha sana mkubwa!!?

Nimekwambia Mbagala-Kibaigwa-Kongwa-Dodoma... ni Kaskazini mwa soko la mboga na matunda la Kibaigwa fika huko uliza details hizo utampata tu mbona
 
Back
Top Bottom