Kibajaji amvaa vikali Zitto Kabwe kumsema Magufuli, amuita muoga kwani wakati yupo hakusema?

Mimi naunga na Kibajaji kulaani Viongozi wa Ajabu kama Zitto Kabwe na genge lake lote.

Hakuna mwenye haki naaliyepewa Mamlaka kuwahukumu wengine hata siku moja.
 
Lisu alimsema akiwa hai akataka kumuua, sasa unategemea nini?
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli tuu.
Magufuli aliharibu kila kitu. Zitto haja kosea. Mnao mpenda Magu mfuateni huko aliko. Kwisha hiyo!!!
 
Tusifikiri kumsema vibaya Magufuli kutasaidia kitu, hayupo na hawezi kujibu kitu, kama una tatizo naye maliza utakuja kukutana naye kwa Mungu.

Mtu akishatangulia kitabu chake kinafungwa, tunamuachia Mungu kuja kutoa hukumu.
Stop that nonsense, aliowapotezea ndugu zao unadhani wanakubaliana na ujinga huo. Watapenda lifukuliwe lipigwe majiwe
 
Kibajaji mjinga tu. Mbona zito amemuita lissu chiba yeye anakenua?
 
Lisu,Mbowe,wafuasi wa Jiwe etc..

Kwani mumekatazwa kumkosoa au hamna hoja?
Sasa kwani Mbowe na Lissu waliacha kumkosoa Jiwe? Mbona walikuwa wanamkosoa na hata huyo Zitto alikuwa anakosoa ila sasa hivi hamkosoi Samia. Ila wale wa kijani wakiwashwa kumkosoa Samia yatawakuta kama yaliyomkuta Ndugai.
 
Lisu alijaribu akaishia kupigwa Lisasi,Mbowe alibaki kuigiza ukosoaji akatenguliwa mguu,akaporwa bilicans etc akaufya na asingekuwa Samia Mbowe angefia jela.
 
Lisu alimsema akiwa hai akataka kumuua, sasa unategemea nini?
Ila Lissu hakuacha kumsema Magufuli.

Sasa ukijakumsema wakati kafa ndio tutegemee atajirekebisha huko kaburini au ndio kupunguza hasira tu?
 
True!! Mpaka leo Hitler anasemwa! Mitume wanasemwa. Ndio je huyu tu??

Ninadhani kuna namna wanatafuta jambo lolote kutosemwa eti kwa kuwa amekwishatangulia!! Badala ya kuzuia asisemwe, wajikite kusema alichokifanya ni sahihi!! Sio “aachwe apumzike”. Nani aulizwe sasa au wana maana “yaliyopita si ndwele tugange yajayo”. Sasa naona kwanini walipotisha sheria ya Rais, Spika na Jaji Mkuu wasishtakiwe. Walimaanisha waliyofanywa na watu hao yasihojiwe wakishatoka madarakani.
 
Lisu alijaribu akaishia kupigwa Lisasi,Mbowe alibaki kuigiza ukosoaji akatenguliwa mguu,akaporwa bilicans etc akaufya na asingekuwa Samia Mbowe angefia jela.
Tuelewane hapa kwamba Mbowe na Lissu hawakuacha kumkosoa Magufuli waliendelea. Et asingekuwa Samia! Mara ya kwanza huyo Samia alipoulizwa kuhusu kesi ya Mbowe alijibu nini? Msinge mshinikiza mngemuacha atende haki pasina kushinikizwa kama alivyowaachia wazanzibari wenzie hakufanyiwa mashinikizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…