Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo bungeni mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde amemvaa vikali kiongozi mkuu wa ACT, Zitto Kabwe kwa kumsema Hayati Magufuli. Kibajaji amemuita Zitto muoga kupitiliza kwani wakati Magufuli yupo hai hakusema mpaka ameondoka.
Pia Kibajaji amesema wote wanaomsema Magufuli ni wanafki na hata Samia akiondoka nae watamsema vilvile. Amemsifu Nyalandu kwa kusema kwa vitendo hawezi kufanya kazi na Magufuli wakati yupo hai na kuachia nafasi yake ya ubunge.
========
Kibajaji: Nchi yetu imeweka vizuri sana masuala ya utawala bora kisheria lakini kuna baadhi ya vyama kwa mfano pale Zanzibar, ACT tunashirikiana nacho kwenye utawala bora, sisi tuna Rais, tuna Serikali wao wana makamu wa kwanza wa Rais lakini mmesikia kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto anamnanga mheshimiwa Magufuli kana kwamba Zitto hashiriki kwenye Serikali.
Magufuli aheshimiwe, Zitto aelewe kwamba suala la kufiwa ni suala kubwa. Haiwezekani kwenye utawala bora tuache suala la Magufuli kuzungumzwa vibaya na mimi sitaacha.
Leo nnapoongea Waislamu mmefunga, dini inawakataza kuwasema vibaya marehemu, Zitto ni muislamu anajua.
Mheshimiwa Zitto anatutaka tunaompenda mheshimiwa Magufuli tukazikwe nae. Zitto amewahi kufiwa na mama yake, mimi sitaki kufika huko, mama wa Zitto ni mama yangu mimi. Mimi nimewahi kufiwa na baba yangu lakini ACT wamewahi kufiwa na makamu wa kwanza wa Rais, Zitto anatulazimisha sisi tuanze kumsema vibaya Maalim Seif, hatuwezi.
Inakuwaje watu mnakuwa waoga, viongozi wakiwepo hamsemi wakiondoka ndio mnasema, huu ni uoga uliopitiliza. Mtu mmoja tu alisema kwa vitendo kwamba yeye hawezi kufanya kazi na Magufuli, Nyalandu.
Aliachia ubunge akaondoka lakini watu tuliobaki hapa ni watu wa Magufuli na tumefanya nae kazi na tulikuwa tunamsifu.
Hawa watu ambao sasa wanamsema Magufuli ni wanafiki wakubwa, Samia akiondoka watamsema vibaya hivyohivyo, ni bora mimi Lusinde ambae niko wazi na siwezi kuacha.
Pia, soma => Zitto: Wanaompenda Magufuli wakazikwe naye Chato, alikuwa Rais fisadi zaidi kuwahi kutokea Tanzania