Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Kibaka Ajaribu Kuchomoka na Zawadi za Harusi ya Mtoto wa Sumaye
Wananchi wenye hasira wakijaribu kumuadhibu kibaka aliyejaribu kuchomoka na zawadi za harusi ya mtoto wa SumayeMonday, May 25, 2009 4:31 AM
Katika kuonyesha kwamba vibaka wa Tanzania wanatumia mbinu mbali mbali za ajabu, kibaka mmoja aliyejifanya mgeni mualikwa katika harusi ya mtoto wa Sumaye alipewa kipigo cha nguvu baada ya kukamatwa akijaribu kuchomoka na zawadi za maharusi.Wizi katika kumbi za sherehe hasa katika hoteli kubwa jijini Dar es Salaam umezidi kushamiri kwa kasi ya ajabu.
Katika harusi ya mtoto wa Sumaye iliyofanyika jumamosi kijana mmoja ambaye alijifanya kuwa ni mmoja wa wanandugu wa waziri mkuu wa zamani Fredrick Sumaye alipata kipigo cha nguvu baada ya kukamatwa akiwa amebeba kifurushi kilicho kuwa kimejaa zawadi za maharusi akijaribu kuondoka nazo kutoka katika ukumbi wa Hoteli ya Ubungo Plazza.
Katika kumbi nyingi hivi sasa kumekuwepo na vijana wasichana kwa wavulana ambao huwa wanavalia kinadhifu na bila kujua utadhani ni miongoni mwa wageni waalikwa, na pindi unapofika wakati wa kwenda kuchukua chakula wengi wa wageni huacha simu zao na zawadi zao mezani na vibaka hutumia nafasi hiyo kuzichukua na kuondoka nazo.
Kijana huyu aliyekamatwa alikuwa tayari kishaanza kutafuta tax kwa ajili ya kuondoka na mizigo aliyoiba.
Mizigo aliyoiba ilikuwa ni zawadi za maharusi na kama angefanikiwa kutoweka nazo basi angefaidika sana maana kulikuwa na vitu vingi vya thamani sana.
Katika sakata hilo hata walinzi wa Ultimate Security hawakumshitukia kibaka huyo kwani walidhani ni miongoni mwa wahusika katika sherehe hiyo.