Highlander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 3,093
- 1,075
Maras kumbe nao hawavumi........
Mpaka sasa Intelijensia ya Kova imeshindwa kumkamata?
Hiyo mali ya 1.5M aliyoikwapua ni nini just incase kama atataka kuiuza inaweza ikasaidia.
Tukiwaonesha alipo kwenye hizo million 1.5 utatugawia bei gani???
View attachment 80109
UBK/RB/119/2013: WIZI
Kibaka anayeonekana katika picha hii ni mwizi mzoefu wa maofisini, ambako
hudokoa vitu mezani baada ya kuwapoteza malengo wafanyakazi kutafuta chenji.
Anatafutwa kwa wizi wa kifaa cha thamani ya Tsh. 1.5 million/- maeneo ya Ubungo.
Tafadhali sana Kama unajua anaishi wapi, au nyendo zake, ni PM mimi au waoneshe Polisi wamkamate na kumpeleka Kituo cha Polisi Ubungo Kibangu. Tunatanguliza shukrani kwa ushirikiano tarajiwa.
AK48, Dar es Salaam.
Mbona mnaliharibu hili jukwaa? hapa sio mahali kwa kutangaza wahalifu nendeni huko polisi wakafanye kazi hii. Ukiendekeza mchezo huu mchafu iko siku utakuta picha yako pia unatafutwa kwa uasherati wako.
Mkuu Distazo unatafuta kulinda uhalifu katika jamii. Kama unao ushahidi wa uasherati wangu kafungue RB polisi yenye maelezo kamili kuhusu uasherati huo na kwa vipi nimekufanyia jinai. Weka simu yako watu wakueleze nipo wapi. Weka picha yangu.
Jukwaa hili ni sawa tu na foleni kubwa ya majirani. Kuna ubaya gani kuwaambia majirani nimeibiwa kitu jamani na mwizi wangu namjua wala simkisiii! Nisaidieni kumkamata.... Mbona unataka kumsadie huyu mwizi? Au ndugu yako?
Sasa nikwambie kitu. Huyu hatajificha katika Tanzania hii. Nitampata tu na hii mali atarudisha kwa gharama yoyote....
Tangu lini Tanzania tumeacha kuomba msaada kwa majirani?
Sitaki malumbano, kama kushirikiana na huyo mwizi itakuwa ni wewe umeshirikiana naye kwa sababu imekuwaje umepata picha yake kama sio mshirika wako?
Ndugu Distazo, katika Tanzania hii tuna Hulka nyingi za watu.
Usidhani kila ofisi inakosa utaratibu wa usalama kazini.
Kama huyu mwizi ni ndugu yako mshauri arudishe kifaa chetu kwa amani na yataisha kwa amani.
Anajua alikipata kifaa hicho wapi tarehe 19 Januari, 2013, saa 9.00 kamili Alasiri.
Akirudishe kwa amani na sisi tutamwacha.
Jibu swali kwanza ili upate ushirikiano zaidi. Picha ya mwizi umeipata wapi? ulimuajiri? ulikuwa unamlipa mshahara wake ipasavyo? ushahidi upo?