Kibaka mzoefu anatafutwa na polisi

Kibaka mzoefu anatafutwa na polisi

Highlander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
3,093
Reaction score
1,075
View attachment 80109

UBK/RB/119/2013: WIZI

Kibaka anayeonekana katika picha hii ni mwizi mzoefu wa maofisini, ambako
hudokoa vitu mezani baada ya kuwapoteza malengo wafanyakazi kutafuta chenji.

Anatafutwa kwa wizi wa kifaa cha thamani ya Tsh. 1.5 million/- maeneo ya Ubungo.

Tafadhali sana Kama unajua anaishi wapi, au nyendo zake, ni PM mimi au waoneshe Polisi wamkamate na kumpeleka Kituo cha Polisi Ubungo Kibangu. Tunatanguliza shukrani kwa ushirikiano tarajiwa.

AK48, Dar es Salaam.
 
Maras kumbe nao hawavumi........

Aise huyu kibaka ni mwizi fundi kwelikweli wa saikolojia ya watoto--hasa wa kike. Victims wake wengi wasichana. Kuna mahali alikwapua Steplar ya steshenali yaani bila jasho. Nii HB wa kiaina aina vibinti vinamuamini haraka kumbe jizi la kutupa. Jamani tusaidieni tumpate huyu mtu

View attachment 80112
 
Ukimwona huyu mwizi tafadhali tutonye kwa namba yetu ya kazini: 0716224944
Au Mkabidhi polisi utayemwona jirani. Kesi ya mtuhumiwa ipo Ubungo Kibangu
View attachment 80115
 
Mpaka sasa Intelijensia ya Kova imeshindwa kumkamata?
Hiyo mali ya 1.5M aliyoikwapua ni nini just incase kama atataka kuiuza inaweza ikasaidia.
 
price tag iliyowekwa kwa hicho kichwa ni Tsh. ngapi? halafu anapendelea kutembelea maeneo gani?
 
Mpaka sasa Intelijensia ya Kova imeshindwa kumkamata?
Hiyo mali ya 1.5M aliyoikwapua ni nini just incase kama atataka kuiuza inaweza ikasaidia.

Tuna Production House ambayo huwa inapiga Still Pictures pia.
Huyu Mwizi habeba NikonD40 Mpya. Hii Camera inatuuma sana mkuu...
 
View attachment 80109

UBK/RB/119/2013: WIZI

Kibaka anayeonekana katika picha hii ni mwizi mzoefu wa maofisini, ambako
hudokoa vitu mezani baada ya kuwapoteza malengo wafanyakazi kutafuta chenji.

Anatafutwa kwa wizi wa kifaa cha thamani ya Tsh. 1.5 million/- maeneo ya Ubungo.

Tafadhali sana Kama unajua anaishi wapi, au nyendo zake, ni PM mimi au waoneshe Polisi wamkamate na kumpeleka Kituo cha Polisi Ubungo Kibangu. Tunatanguliza shukrani kwa ushirikiano tarajiwa.

AK48, Dar es Salaam.

Mbona mnaliharibu hili jukwaa? hapa sio mahali kwa kutangaza wahalifu nendeni huko polisi wakafanye kazi hii. Ukiendekeza mchezo huu mchafu iko siku utakuta picha yako pia unatafutwa kwa uasherati wako.
 
Mkuu Distazo unatafuta kulinda uhalifu katika jamii. Kama unao ushahidi wa uasherati wangu kafungue RB polisi yenye maelezo kamili kuhusu uasherati huo na kwa vipi nimekufanyia jinai. Weka simu yako watu wakueleze nipo wapi. Weka picha yangu.

Jukwaa hili ni sawa tu na foleni kubwa ya majirani. Kuna ubaya gani kuwaambia majirani nimeibiwa kitu jamani na mwizi wangu namjua wala simkisiii! Nisaidieni kumkamata.... Mbona unataka kumsadie huyu mwizi? Au ndugu yako?

Sasa nikwambie kitu. Huyu hatajificha katika Tanzania hii. Nitampata tu na hii mali atarudisha kwa gharama yoyote....

Tangu lini Tanzania tumeacha kuomba msaada kwa majirani?
 
Sitaki malumbano, kama kushirikiana na huyo mwizi itakuwa ni wewe umeshirikiana naye kwa sababu imekuwaje umepata picha yake kama sio mshirika wako?
 
Ndugu Distazo, katika Tanzania hii tuna Hulka nyingi za watu.
Usidhani kila ofisi inakosa utaratibu wa usalama kazini.

Kama huyu mwizi ni ndugu yako mshauri arudishe kifaa chetu kwa amani na yataisha kwa amani.
Anajua alikipata kifaa hicho wapi tarehe 19 Januari, 2013, saa 9.00 kamili Alasiri.
Akirudishe kwa amani na sisi tutamwacha.

Jibu swali kwanza ili upate ushirikiano zaidi. Picha ya mwizi umeipata wapi? ulimuajiri? ulikuwa unamlipa mshahara wake ipasavyo? ushahidi upo?
 
Distazo huyu mwizi hakuwa mwajiriwa katika ofisi yetu. Alikuja ofisini kwetu akiwa kama mteja. Kamera aliyoiba ndiyo tuliyoitumia kumhudumia. Mhudumu aliingia chumba cha ndani kufuata chenji akiwa kamwacha huyu mwizi front office. Ndani ya sekunde kama 20 hivi huyu mwizi alitokomea kusikojulikana akiwa na kamera tuliyoitumia kumhudumia. Ilitokea tu bahati nzuri tulikuwa tumekwisha itoa ile picha yake kutoka katika kamera hiyo.

Imetokea tu bahati nyingine kwamba tumepata taariza za ziada kutoka ofisi nyingine ambako aliiba kifaa kwa ujanja kama huo. Kama unamfahamu tafadhali mshauri arudishe Kamera yetu.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mkuu AK48

Kuna mtu kama huyo nimekutana nae Sinza anatokea kwenye geti moja hivi (nyumba kama hakuna waakiji vile) niliposimama
kumwangalia vizuri alirudi nyuma na kusita kutoka getin hadi niliposogeza gari ndio akatoka. Nyumba yenyewe ipo karibu na makutano ya barabara ya Kwa Remmy kuelekea Sinza E na barabara inayotokea sinza lion hotel kupitia kanisa katoliki sinza. Hiyo nyumba ipo karibu na kampuni ya uchimbaji wa visima.

Jana niliona hii picha so leo asubuhi nlivyokua napita nakumwona nikakumbuka. Kwa muonekano wa huyo bwana ni kama alivyo kwenye picha ila kavaa kofia but rasta zinaonekana. Unaweza kuwatumia Polisi kufanya inteligency zaidi kubain ni yeye au la.
 
Innocent until proven guilty labda ungesema mtuhumiwa wa wizi.., (unless kama ameshahukumiwa na kukubali kosa)
 
Nimemuona ila sina vocha kwenye simu,kama vipi niPM vocha
nikupe ma details,am serious
 
Back
Top Bottom