Kibaki amerudi Ikulu


Ngoja kwanza mkuu, yaani sisi hapa ni kwamba ni principle, kwa hiyo kama Kibaki ali-champion mageuzi na kama leo amebadilika kubaka mfumo na principles zilizotufanya tumuunge mkono lazima tumkome nyani gladi. Kwa maneno mengine hapa hapendwi mtu, ni principle tu. Ndio kusema hata shujaa wetu Zitto akitugeuka kesho akaanza kuleta za kuleta tutamkoma nyani gladi hapahapa mkuu, tena wewe ndio umetufundisha huu msemo.
 
Kitila Mkumbo,

Kibaki 2002 tulishangalia sana- kama mkombozi- je kwa nini 2002 hakuonekana mwizi? Chiluba 1991 tulishangilia tu sana!

Kuna tatizo na democracy in general in Africa- imetumika kulinda the elites (both in Afrika and West) and those in power- siku zote nasema we need a different form of democracy- ktkk ya Wachina na West!

Institutions zote za haki ni za West- sasa hata Raila akienda Mahakamani- anaweza ashishinde- this is weakness of institutions we have 'copied and pasted' - so it could be taabu iko ktk institutions za haki- which are weak and in Africa are currently evolving!
 



Sources:

http://www.law.cornell.edu/supct/html/00-949.ZPC.html
 
wakati pekee ambapo Rais mpya anatakiwa aapishwe mara moja ni pale inapotokea Rais aliye madarakani anapofariki au kupoteza sifa zake za kuwa rais.


Na hii ndio sababu hasa imebidi wa-declare na kumwapisha harakaharaka, huyu aliapishwa tarehe 30/12/2002 kwa hivyo urais wake ulikuwa unaishi effectively leo; maanake ingefika kesho nchi ingekuwa haina Rais na Kibaki angekuwa tena hana nguvu za kulazimisha alicholazimisha!

Pengine the best system ni Uganda. Kule ukichaguliwa unabaki president elect for 60 days ili kutoa nafasi kama kuna watu wana-appeal against your election.
 
MKuu FMES,

nimeanza kukuwekea maamuzi ya kesi toka Cornell university maana inaoenekana unataka hata kubisha kuhusu sheria ya uchaguzi.

Anza na post yangu number 63
 
hivi maana ya kumkoma nyani gladi nini?? mie sielewi ila naunganisha sentensi kupata maana
gladi ni nini?
 

katika hili fuata link hii uone vile unavyokosea katika hili

[media]http://www.presidency.ucsb.edu/docs/florida2000/12-10_bushbrief.pdf[/media]

soma pia post yangu number 63 uone kuwa hakuna sheria inayosema kuwa recount lazima ifanyike state nzima na badala yake sheria inasema the other way around na Bush alishinda kwa kuargue the other way aroud


Kwa hiyo ni kwa sababu makabila mengine hayakuungana walio wengi wa kabila moja wakashinda wakaishia kuwa wengi na kushinda,

Makabila mengine yameungana mkuu na yakashinda ila Kibaki akaiba. Raila kapata kura toka kwa waluhya, kalenjin, wacoast na wengine kama 40 hivi. Kibaki ameiba na wala hakuna spin nyingine hapa.


Unajua mkuu wewe hapa unaheshimika ila hii tabia yako ya kudai kujua majina ya watu wengi hapa umekosolewa na kina Icadon, kisura nk lakini bado unaendelea. Hii issue ya majina unaitumia sana ukiona unazidiwa. Hilo jina lingine ninalotumia ni lipi na inanisaidia nini kutumia majina mengi. Hii inakudhalilisha mzee maana kila wakati unadhani unawajua watu hapa kumbe unakosea.


Tafadhali usiniwekee mambo ambayo sijasema


The same talking point ya kutetea status quo


Watu wengi wanaangalia future - kumbuka ule mfano wa Mkandara niliouweka somewhere hapo juu.
 
Kitila Mkumbo,

Kibaki 2002 tulishangalia sana- kama mkombozi- je kwa nini 2002 hakuonekana mwizi? Chiluba 1991 tulishangilia tu sana!

Wewe hauonekani kabisa kama mtu aliyeshangilia Chiluba au Kibaki maana argument zako zinaonyesha tofauti kabisa.


Usihamishe lawama kwa wengine. Tatizo letu ni wanasiasa tulio nao hapa ambao ni walafi na wasiotaka kuachia madaraka hata kama wangekuwa na strong system bado mambo ni yale yale tu ya kushindwa na kuiba kura huku wakileta viroja vya kuita watu majina.
 

Hii ni nyingine toka kwa Kenyan-Tanzania
 

i)Soma jibu langu kwenye post niliyom-quote FMES

ii)Whatever form of government we adopt, the key is this, people's will and decision have to be respected. Pale ambapo matokeo yataibwa kutazuka fujo tu! Hakuna shortcut zaidi ya kuheshimu maamuzi ya watu.
 
Kwa kweli haya yaliyotokea yameiharibu Africa. Sasa kila kiongozi aliopo madarakani watakuwa na kila sababu ya kuiba uchaguzi. Tena sasa hivi M7 na mwenzake Mugabe watakuwa wanacheka sana, wanajua sasa wameongeza member katika club yao ya kuchezea sanduku la kura chini ya ukurugenzi mahiri katika hili CCM.
 
Inadhiirisha kuwa kweli madaraka matamu, miaka 5 iliyopita huyu Kibaki alikuwa mpinzani leo hataki kukubali kushindwa, watu wa namna hii ndio wanawakatisha tamaa wapiga kura wengine wanaishia kuchagua vyama tawala kila chaguzi zinapofika. Changamoto kwa wapinzani wa nyumbani.
 
La kutafakari hapa nini raia wafanye, baada ya mtu wasiemtaka kujisimika katika uongozi wa nchi bila ya ridhaa yao? Sishauri watu waingie msituni. Kwani hatua kama hiyo, inaweza kuwa moto juu ya moto na matokeo yake hayamsaidii yeyote katika jamii. Na kukaa kimya bila kufanya kitu cha kuukomesha mchezo huu, ndio dhambi kubwa kabisa isiyoweza kusameheka. Nashauri viongozi wa ODM na wafuasi wake, pamoja na wapenda haki wajiandae kupanga na kutekeleza migomo baridi (civil disobedience) mpaka Kibaki na serikali yake ishindwe kufanya kazi kabisa (total paralysis). Najua kuna maumivu mengi yatakayopatikana kutokana na hatua kama hii. Lakini, kama hakuna maumivu, hakuna faida itakayopatikana (no pain, no gain).
 
The question before the Court is not whether local entities, in the exercise of their expertise, may develop different systems for implementing elections. Instead, we are presented with a situation where a state court with the power to assure uniformity has ordered a statewide recount with minimal procedural safeguards. When a court orders a statewide remedy, there must be at least some assurance that the rudimentary requirements of equal treatment and fundamental fairness are satisfied.

Mkuu umesema maneno mengi sana, lakini la muhimu ni hili hapa tu kwamba sheria za Florida State, zinaruhsu kuhesabu kura lakini za Federal haziruhusu, mengine you can say as much as you want heshima yangu huezi kuipunguza wala kuiongeza na mabishano yako mkuu yasiyokuwa accademically guided, halafu mimi siwezi kuwa wewe hata siku moja, umejaribu kuupindisha mjadala wa Mama Mongella, umeshindwa tena vibaya sana, sasa unajaribu kutafuta kwa kulazimisha mabishano kwenye huu lakini kama kawaida, na siku zote ni lazima uwe na maneno ya heshiam yangu na uzito wa jina langu, maana siku zote vinakusumbua sana unaoneakana ungependa sana kuwa kama mimi, kumbe FD alikuwa right maana ndiye wa kwanza kusema hivyo kuwa kuna watu wangependa kuwa kama mimi, siku zote unaonekana kuamini kuwa huenda one day unaweza kuliharibu jina langu na hii mijadala isiyokua na kichwa wala miguu, uchaguzi ufanyike Kenya, wewe unishupalie mimi what do I have to do na Kenya? Unajaribu kusema nini kwamba Odinga akishinda na upinzani Tanzania utashinda?

Hivi sio Odinga huyu aliyewakanusha upinzani bongo pale maelezo kuwa yeye na chama chake wana mahusioan na CCM, maana wao sasa ni watwala sio wapinzani? Siku Kenya akigombea a new candidate nitaelewa lakini hawa kina Odinga, kibaki, Saitoti na the rest, hata siku moja hakuna lolote jipya!

Kama ni kesi Gore alishindwa kwa sababu Supreme Court, ilisimamisha recount ya majimbo machache ambayo Gore alijua kuwa ni democrat, Supreme walisema kama anataka recount iwe kwa State nzima, kuhusu uchaguzi wa Kenya, binafsi simuamini anyone kuanzia Odinga, mpaka Kibaki, wote ninawaona kuwa ni wasaniii watupu, not worthy of masikitiko, mpaka labda nitakapopata facts zaidi, maana sitashangaa kuwa Odinga pia amehusishwa na matokeo,

Otherwise, ninakutakia mjadala mwema ila kwa sasa inabidi nikuachie ushindi, kuhusiana majina mengi hata siku moja sijawahi kukosea wewe niwekee tu nitakutajia nani ni nani yaani wale wote wanaotumia majina mengi kuharibu mijadala, it is a shame act, lakini for some reason ni tabia iliyokubaliwa hapa forum, lakini sijawahi kukosea mkuu,

Uchaguzi umefanyika Kenya, hauhusiani kwa lolote na Tanzania mpaka kuanza kupigizana makelele, Kenya ni Kenya na siasa za ukabila, Tanzania hatuna hizo siasa, isipokuwa tuna wananchi wsioelewa siasa yao na sheria zao.

Good night mkuu!
 

Mkuu inaonekana umeanza kashfa so kwa hiyo ngoja nikuache upate upper hand mkuu. ulichosema kuhusu Florida unakijua na kama ukisoma sheria utaona ukweli. So ngoja niache wasomaji waaamue


Kama wewe unahitaji mambo ya kushinda au kushindwa basi endelea mkuu maana mimi uko sipo kabisa. Ukijaribu kunitafutia majina na kudhani kuwa mimi nataka ushindani nawe utakuwa unakosea kabisaa.
Sijali kabisa majina ya watu hapa na hujaona nikijaribu kutafuta nani ni nani hapa kama wewe. Endelea na sifa zako na ushindani wako kwani mimi siko huko kabisaaa.


Mkuu heshima yako hapa forum ni kubwa sana na wala usiwe na paranoid kuwa kuna watu wanataka kukuharibia sifa hapa. Watu wanajali issues tu na ukiangalia nilichofanya hapa ni kukusahihisha tu pale ulipokuwa unakosea kama ambavyo wewe huwa unasahihisha watu kwenye thread za malecela au za mambo ya nje na husikii wakisema kuwa wewe unataka kuwaharibu majina yao binafsi.


Haya ni ya kwako na mpaka pale utakapoleta evidence kwenye hili utaonekana unabluff tu mkuu.


Ukinionesha sehemu yoyote niliyokulazimisha uamini kile ambacho ninachoamini basi nitakuomba msamaha hapa forum. Soma tu kesi ya Gore na facts za Kenya ili next time uwe na facts zote.


FMES, mimi sikujui wewe ni nani na wala sitaki nikufahamu. Nina hakika kuwa wewe hunifahamu na watu wengi hapa huwafahamu maana huwa unakosea mara kwa mara. Kuzani kuwa mimi ni fulani hapa ni makosa maana huna idea kabisa of the guy behind this computer.

Heshima kwako zaidi mkuu ila nakuhakikishia kuwa sina mpango wa kukushinda wewe maana una jina kubwa hapa JF. Nimekusahihisha tu kwa yale uliyokosea kama ilivyokawaida ya JF. Pole kwa misundestandings ila nakuhakikishia kuwa umekosea sana kudhani kuwa mimi natumia hayo majina mengine.
 
According to the dataz ambazo nimezipata few minutes ago, ila sijui how good au bad they are, lakini nitawachia wananchi waamue,

Odinga, alikuwa warned mapema na wanaofahamu zaidi siasa za Kenya, kwamba kusingekluwa na uwezekano wa yeye kushinda akiwa Orange, badala yake aliambiwa arudi KANU na kuwavuta Mudavadi, na Kilonzo, kwa sababu aliambiwa Orange ni tawi tu la NARCO ambayo toka ishike power haikuwa na a good record zaidi tu ya kukimbilia Ikulu, kwa hiyo akaombwa kuwa kujiweka sawa na angalau Wakikuyu ingawa sio wote basi ajiunge na KANU, lakini akakataa kata kata, ingawa alibembelezwa sana na the powers!

Habari za huko zinasema kuwa jeshi zima la Kenya ni wa-Kikuyu, GSU ni wa-Kikuyu ndio wengi sana, na hata kama Odinga angeshinda wao wangeingia msituni, maana Mkikuyu hawezi kukubali kutawaliwa na Mjaluo, kwa kweli it very sad, lakini ndio siasa zetu Afrika, sasa what is next, nasikia Odinga amepewa warning kali sana kuwa asimamishe fujo ama sivyo, yatamkuta ya Bhutto! What a shame!

US wanasema in private, shetani wanayemjua ni Kibaki, ni better kuliko shetani wasiyemjua Odinga, it is over, huko SA nako nasikia moto unawaka, Mbeki anataka kumzima Zuma, nasikia Makaburu walishasema kuwa Zuma hawezi kuwa rais wao, lakini Mandela na Mbeki sawa, wakati Zuma yuko jela ya Makaburu, Mbeki alikuwa akizunguka tu nje, sasa anajaribu kumzima a Freedom Fighter,

Sasa nasikia the first task ya Kibaki, sasa ni kutumia anymeans necessary ili atambuliwe kwanza na sisi Tanzania, maana the rest will follow, sasa tusubiri tuone msimamo wa viongozi wetu ulipo!

Only in Afrika!
 
Haya matatizo ya Kenya ni makubwa , nashindwa kuelewa hawa wakina Zito wanaokimbilia kutaka federation ni kwa manufaa ya taifa au kuna position ambazo wameahidiwa ?
 
Quote:-

"nashindwa kuelewa hawa wakina Zito wanaokimbilia kutaka federation ni kwa manufaa ya taifa au kuna position ambazo wameahidiwa ?"

Mkuu Rufiji,

Heshima mbele, hebu fafanua kidogo hapa wengine hatujakuelewa vizuri?
 
Unfortunately hiyo ni sehemu ya miscarriage of justice. Ilitokea Marekani mwaka 2000 na 2004 kiasi kuwa imechukua miaka minane kuachana na kiongozi aliyeingia madarakani kwa wizi wa kura. Zawadi iliyotokana na kiongozi wa namna hiyo ni kuongozwa na "the worst President in American History," worse that Taft, na kuiacha nchi ikiwa almost muflisi.

Kibaki ajiandae kuona image yake aliyojenga miaka mitano iliyopita inafutika kabisa, na vile vile ajiandae kuiona Kenya ikiharibika kiasi kuwa hata yale makampuni multinationals yaliyokwisha jijenga pale yataanza kukimbilia Tanzania au Uganda: Kufa Kufaana.
 
Habari na salaam toka Kiserian Kenya . Afrika Mashariki imeingizwa katika mgogoro mkubwa sana .Kulazimisha kwa Kibaki kuwa Ikulu kunaleta shida kubwa sana Kenya . Tanzania sijajua JK kaupokea vipi huu ushindi wa Kibaki lakini Kenya sim shwari. Natembea na Passport yangu nje na nina polisi 2 wa Kenya maana hali si tulivu.Wamevaa kiraia na silaha ili kupata habari kidogo kidogo .Hali ni tenge na kila mtu ni muoga hapa .Nitawapa zaidi maana nategemea kujivuta kuingia Jiji senta kabisa baadaye leo .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…