Quote:-
"Sidhani kama kuna mtanzania anayefurahia kuona mambo yanayotokea Kenya."
Hizi ni label za kawaida hapa inapotokea mijadala mikali ya ishus, mkuu nina documentary ya Mobutu-The King Of Afrika, a very shameful thing to watch, kilicho nishangaza humo ndani ni just two years baada ya Mobutu kumuuua Lumumba, Mwalimu alikwenda kutembelea huko tena yeye na Mobutu wako kwenye gari la wazi wakiwapungia mikono wananchi, tena kwa furaha sana, sasa ina maana Mwalimu alikuwa ana-support yale mauaji ya Lumumba?
Jawabu ni hapana, lakini life has to go on, wa-Tanzania tuliwa-support Biafra, baadaye tukajirudi na kuwa friends na Federal government of Nigeria, ndio maana ya siasa na kuganga yajayo badala ya kulalia yaliyopita, Kibaki, ameshaapishwa kuwa the next president wa Kenya for the next Five years, leo nilikuwa ninaaangalia TVT jinsi viongozi wetu wa upinzani walivyojitokeza kukosoa uchaguzi huo, lakini mwishoni wote wamekubali kuwa baada ya kuapishwa kwa Kibaki, haitakuwa rahisi kubatili matokeo, na wamewaomba wananchi wa Kenya kuweka taifa lao mbele zaidi ya special interest zao, je ina maana hawa nao wanam-support Kibaki? Jawabu ni hapana isipokuwa kama politicians wanaelewa kuwa rais aliyekwisha apishwa labda kuna uwezekano wa 25% kuwa anaweza kubadilishwa,
Hatupendi yaliyotokea huko kwenye mchakato mzima wa uchaguzi wao, lakini pia tunaelewa kuwa imekuwa ni kawaida yao kuwa vurugu wakati wa uchaguzi, tunakumbuka Moi kila wakati alikuwa akishinda kwa ujanja huu huu na damu kumwagika, na bado tukaendelea kuwa marafiki naye kama taifa,
Kuna some of us ambao to put a side mambo ya vurugu za demokrasia kupindishwa, tungependa pia kujua elimu yake ya siasa yaani uchaguzi mzima, na pole pole tumeshaanza kujifunza yaliyojiri na yale ambayo hayakujiri kutoka pande zote mbili kufuatia political strategies zao, inaonekana kuwa so far Botswana ndio peke yao wenye uchaguzi wa halali katika Afrika, sasa what that says about the rest of us Afrikans, kwamba tunafurahia yanyoendelea kwenye nchi zetu?
Kama hatufurahii tumefanya nini so far? Je does that gives us a platform kuwa-label wengine kuwa wanafurahia yalliyotokea Kenya jana?